Voyeurism:

Voyeurism ni maradhi ya kisaikolojia ambapo mwenye maradhi haya anakuwa na tabia ya kupenda kuangalia watu wasio na nguo. Mtu mwenye maradhi haya huitwa kitaalamu Voyeur (inasomwa vouya). Kwa Kiingereza cha kawaida, mtu huyu huitwa Peeping Tom, Waswahili humwita kozimeni.

Mara nyingi Voyeur huwa na tabia ya kuchungulia watu walio kwenye faragha, na yeye roho yake hufurahi kuwaona watu walio wazi bila nguo, na furaha yake hufikia kilele kama atawaona mke na mume wako katika kitendo cha ndoa.

Katika jamii yetu leo, maradhi haya yameingia kwa kasi. Tunao watu wengi waliozama hapa, na iko haja ya kupambana na maradhi haya, na hakuna anayeweza kupambana nayo bali Waislamu. Siku hizi, wenye maradhi haya huwezi kuwakuta wanachungulia madirishani au sehemu nyingine, kwa sababu wanaweza kushikwa na kuchomwa moto kwa kudhaniwa wezi. Kuna mbinu mpya za kukidhi haja ya wenye maradhi haya. Zamani kulikuwa na magazeti ya X. Siku hizi kuna kanda za video, DVD na Internet. hawa akina Peeping Toms hujifungia ndani na kuanglia website za ngono au kuangalia kanda. Hawa ni wagonjwa mahututi.

Kuna wagonjwa wengine ambao sio mahututi, lakini nao pia ni ma Voyeur. Kwa mfano, binti wa Kiislamu anaweza akaomba avae hijabu shuleni, lakini wapo watu hawakubali binti huyu afunike viungo vyake.

Utamkuta mwalimu anakuwa mkali kabisa, kwani na yeye ni miongoni mwa watu ambao roho zao haziridhiki mtu, hasa mwanamke anapojihifadhi. Hawa ndio wale wale ambao huandaa kile kinachoitwa "mashindano ya uzuri" na kuwapitisha mabinti waliovaa "vichupi" mbele ya kadamnasi, na mwisho huwapa zawadi. Kwa bahati mbaya sana, wenye maradhi hawa ni pamoja na viongozi wa nchi. Wao hufungua na kushiriki katika mambo haya ya kukodolea macho watu walio uchi.

Mtume amesema: "Jinsi mlivyo, ndivyo mtakavyotawaliwa", kwa hivyo, kama viongozi wetu ni ma Peeping Tom na ma Voyeur, au Makozimeni, je wanaoongozwa watakuwaje!?

Kiboko ya maradhi haya hakuna zaidi ya Uislamu kwani ndio unaotekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu yasemayo:
"Wala msiikurubie zinaa hakika hiyo ni uchafu na njia mbaya kabisa".
Qur. 17:32

0 comments/Maoni: