UTABIRI WA ISAYA

Isaya 7:14 …Tazama bikira atachukuwa mimba, atazaa mototo mwanamume naye ATAMWITA jina lake Imanueli. 

Wakristo upenda sana kutumia huu mstari kuonyesha kuwa Nabii Yesu alitabiriwa kwenye mstari huu, lakini ni kitu cha kushangaza sana kwa kushindwa kuangalia mstakabri mzima wa huo mstari ulipo anzia mpaka kufikia aya ya 14.

Ukisoma kuanzia Anza Isaya 7:10, utagunduwa kuwa utabiri ulikuwa unamuhusu Mfalme Ahazi au Isaya mwenyewe kuwa mkewe ndio atakaye zaa mtoto na ndio maana ukiendelea mbele mpaka kufikia Isaya 9:6, utakutana na maneno haya:

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Isaya 9:6

Mstari huu, umeandikwa kwa present past tense, yaani tukio ambalo limekwisha tokea, ila utokeaji wake si wa muda mrefu. Ndio maana ikaandikwa "...Tumepewa mtoto mwanamume..." Kuonyesha kuwa tendo limekwisha tendeka, si kuwa litatendeka kwa wakati ujao.

Hapa nanukuu kitabu kimojawapo ambacho ni mwongozo kwa walimu wa theologia (Teacher’s guides to religions education series) uliokubaliwa na Wanatheologia wote (Agreed Sylabases).

Kitabu hiki kinaitwa "The Rise of the Prophets" Senior lessons – Volume Six cha Norman J. Bull, M.A – Champlain and lecturer in Divinity Saint Luke’s College.

Mfululizo wa miongozo hii imetayarishwa na The Religious Education Press Ltd. Wallington Survey (1961) katika ukurasa wa 156 kikizungumzia "Imanuel"

Kinasema
"(b) Immanu-el. It was Isaiah’s Unwavering Conviction that Yahweh was with His people – Immanu-el (God with us) – If they would but put their whole trust in Him. The Prophet offered a sign of this to the weak and wavering Ahaz  (see above). A ‘Young woman’ – not ‘ a virgin’ – was with child, and would bear a son to be called Immanu-el. Before he was old enough to know good from evil, Israel and Syria will have been destroyed. This ‘sign’ is given in a concrete historical situation (7:14, 8:8,10 cf. Rom 8.31); it is not visionary future possibility. The ‘young woman’ may well have been Isaiah’s own wife (ef. 8:3) or even the wife Ahaz. From the point of view of Isaiah, there is no Prophecy here of a virgin birth".
Hicho ndicho wanachofundishwa Makadinali, Maaskofu, Mapadre n.k. kuwa huyo mwanamke hakuwa bikira (not a virgin) na tayari alikuwa na mtoto (was with child) na wala sio Maria bali mke wa Nabii Isaya au mfalme Ahazi. Na wanasisitiziwa kuwa hakuna utabiri wa uzazi wa mwanamke bikira hapo " there is no Prophecy here of a virgin birth".

Vilevile ukisoma Biblia ya Revised Standard Version (RSV) kuhusiana na Isaiah 7:14, wao wamelitafasiri neno la Kihebrania  (עַלְמָה) 'almāh{al-maw'}  kuwa ni "young woman" Mwanamke Kijana au kwa Kiswahili cha kawaida twaweza kusema Msichana (Kigori) na si kama wanavyotafasiri kwenye biblia zingine kuwa neno ilo lina maana ya "virgin" yaani Bikra au Bikira.

Neno Bikira au Bikra kwa Kihibrania ni  [בְּתוּלָה (bəṯūlāh)] limetumika mara 50 kwenye Septuagint.

Hapa chini kuna tafasiri mbalimbali kutoka baadhi ya Biblia

Revised Standard Version (American; RSV) 
Therefore the Lord himself will give you a sign. Behold, a young woman[a] shall conceive and bear a son, and shall call his name Imman'u-el
---

Tafasiri Nyingine:

The Jerusalem Bible (Koren Publishing; JBK). 
Therefore the Lord himself shall give you a sign: a maiden is with child and she will bear a son, and will call his name Immanuel.
---

New Jerusalem Bible (Catholic; NJB)
The Lord will give you a sign in any case:  It is this: the young woman is with child and will give birth to a son whom she will call Immanuel
---

New English Bible (NEB)
Therefore the Lord himself shall give you a sign: A young woman is with child, and she will bear a son, and will call him Immanuel.
---

New English Translation Bible (NET)
For this reason the sovereign master himself will give you a confirming sign. Look, this young woman is about to conceive and will give birth to a son. You, will name him Immanuel.

Waweza kupitia Rejea kwenye link hizi kujisomea zaidi
"Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana aendavyo" (Mithali 14:15).

Yaliyomo

Viungo za Kiswahili (Kiswahili Link) Viungo za Kiingereza (English Link)
Kwa Nini Uislamu What Does Qur'an Say About Terrorism
Uislamu Ni Nini? Propaganda Against Qur'an
Ukristo Ni Nini Revised Standard Version - RSV
Tofauti Qur'an Na Biblia When God Runs Away from His Creation
Kwa Nini Waislam Wanasoma Biblia Pedophilia and Killing Suckling Infants
Kwa Nini Tunasema Biblia Imechafuliwa Adam was Innocent
Mungu wa Biblia na Upagani Genealogies of Jesus Christ
Utapeli wa Wachungaji Makanisani Challange To Christians
Kisa cha Bi Diams Bible Contradictions
Jibu Letu Which versions Bible are inspired by Holy Spirit?
Paulo au Yesu Conflicting Accounts of Crucifixion
Nani Aliandika Biblia? Top 10 Missionary Tactics
Kutojijua Who are Dogs & Pigs
Je Yesu (as) Ndiye Nabii Iysa (as) Who Have No Faith
Kushamiri Kwa Ushoga na Ukahaba Pork and Its Harmful Effects On Health
Hakuna Sabato They'll Emerge From Their Graves
Uongo wa Kupewa Mabikira 72 Islam and Terrorism
Yvonne Ridley Nilivyokuja Kuipenda Hijab Human Rights in Islam
Alfa na Omega - Kuwepo kwa Yesu Kabla Creation In Six Days
Mapenzi na Maelewano Hearts Find Peace
Jina la Allah Ndani ya Biblia Why Christian tell Lie
Biblia na MwenyeziMungu New Testament
Picha za Mashetani Makanisani Where is Christ-in Christianity
Majini na Iymani Zetu They'll Emerge From Their Graves
Haki za Binadamu Kwa Mujibu wa Qur'an Chapel-Of All Saints In Kutna Czech
Trinity Utatu Why Darwin Was Wrong
Jinsia ya MwenyeziMungu Amazing Story of Arch Bishop
Miungu ya Kipagani Original Sin Part-1-of-2
Je Msalaba Siyo Alama yaUpagani Original Sin Part-2-of-2
Biblia Inasema Yesu Kaja Kwa Waisrail Tu Meaning of son of God
Uungu-wa Bikira Maria Lost Gospel Revealed; Says Jesus Asked Judas to Betray Him
Uungu Wa Yesu Mithra And Christianity
Pasaka en
Yesu Ndani Ya Qur’an Wakristo Hawalijuwi Hili en
Hukumu ya Pilato wa Uyahudi en
Kwa Nini Nguruwe Why Pig en
Nadharia ya Evolusheni en
Je Unajua - Do You Know en
Utabiri wa Isaya en
sw en
sw en
sw en

Adhan and Qur’an programs for computer and mobile phones

Science and usefully Articles

Qur'an

Mawaidha (sikiliza mawaidha mbali mbali hapa)

Contradictions and comparative Religions

Utapeli wa Wachungaji Makanisani

JICHO PEVU: Makri YA Injili - Bishop Dr. Victor Kanyari.


WOMEN, ALCOHOL, PARTYING, TO THE CATHOLIC MONASTERY TO ISLAM

Michael Decero is from Philadelphia Pennsylvania. he was born into a Sicilian family in South Philadelphia. Born a Roman Catholic Christian.


From the age of 13-17 my life consisted of very few things. Women, Alcohol, Marijuana, crime, and money. I quickly fell into a life of worldly pleasures and comforts. I quit school in the 9th grade and got a full time job doing landscaping.

I moved out of my house at 15 years old to live with a friend of mine who I got in trouble with, and we worked together and lived together. I really don't remember a lot of my teenage years because I was always so intoxicated and high. But then right when I would turn 17 something happened!

Read full story Here

Tofauti za kimsingi kati ya Qur’an na Biblia

Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu visivyo pungua 73 kwa mujibu wa madhehebu ya Wakatoliki na kuna yenye vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya Waprotestanti na Kuna ile yenye vitabu 81 kwa madhehebu ya Kanisa la Kiethiopia.

Vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40. Tofauti na Qur’an, yenyewe ni kitabu kimoja kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu mmoja na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.

Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno ya Mwenyezi Mungu, ya Mitume na maoni ya wanahistoria.

Qur’an ni neno la Mwenyezi Mungu tu peke yake. Hata maneno ya Muhammad (s.a.w.) hayamo katika Qur’an.

Katika Agano la Kale na Jipya yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya Mitume mbalimbali. Kumbukumbu la Torati (na Si Torati yenyewe), siyo tu ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu bali pia historia ya maisha ya Nabii Mussa (a.s).

 Injili ya Mathayo, Luka, Marko na Yohana zinaelezea historia ya Yesu kama ilivyosimauliwa na wafuasi wake.

Qur’an si historia ya Muhammad (saw) kama ilivyosimuliwa na maswahaba zake. Qur’an inataja habari za Mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.

Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu Mitume hao. Ndio maana wanazuoni wa kikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika hayo lini

Kwa mfano katika biblia iliyotolewa na Collins iitwayo "Revised Standard Version" ya 1971 uk. 12-17 imeandikwa kuwa Mwandishi wa Samweli hajulikani, pia hajulikani mwandishi wa kitabu cha 2Samweli, 1Wafalme, 2Wafalme, 1Mambo ya Nyakati, Esta, Ayubu, Yona na Habakuki.

Halikadhalika mpaka leo kuna wasi wasi kama kitabu cha Waebrania kiliandikwa na Paulo au na mtu mwingine. Encyclopaedia Britanica inakiri kuwa mpaka hivi sasa hakuna uhakika jinsi gani au ni wapi vitabu vinne vya Injili vilipatikana.

Kinyume chake Qur’an yote iliandikwa wakati wa uhai wa Muhammad na kuhifadhiwa na mamia ya watu.

Injili nne zilizomo katika Agano Jipya siyo Injili zote zilizoandikwa. Zilikuwapo Injili nyingine nyingi. Ila kwa amri ya Mfalme Constantine ilifanyika Sinodi (mkutano wa wawakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua Injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe.

Injili kadhaa zilikataliwa kama vile injili ya Barnabas, Injili ya Marcion, Injili ya Basilides, Injili ya Maryam, Injili ya Yuda, Injili ya Philipo, Injili ya Wahebrania, Injili ya Nazareti, Injili ya Bartholomew na nyingine nyngi (Fungua hapa kuona zaidi).  Na katika historia ya Kanisa viko vitabu vilivyokubaliwa na baadaye kukataliwa na kinyume chake. Ni binadamu waliokuja baadaye ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la Mungu na lipi lisiwe.

Katika uislamu hakukuwa na Ijitimai yoyote iliyokaa kuamua sura ipi iwe Qur’an na ipi isiwe.