Kuporomoka Kwa Maadili, Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba
Katika zama zetu za leo kuna janga kubwa linalohatarisha uhai wa jamii ulimwenguni. Mithili ya virusi vinavyoua mwili, janga hili linasababisha msiba mkubwa wa kijamii. Janga hilo ni mmomonyoko wa maadili ambayo husaidia kustawisha jamii ya Ushoga, Ukahaba na uhusiano haramu wa kijinsia kabla ya ndoa na nje ya ndoa, Filamu za ngono, Picha za ngono, unyanyasaji wa kijinsia na ongezeko la maradhi ya zinaa, mashindano ya kukaa uchi maarufu ulimbwende, uuzaji na utumiaji wa vileo na dawa za kulevya miongoni mwa vijana ni miongoni mwa ishara kubwa za kuporomoka kwa maadili.
Ushoga, usagaji, ubasha na ukahaba ni jambo baya na lisilokubalika kwenye jamii iliostaarabika, na karibia dini zote jambo ili linachukuliwa kuwa ni dhambi kubwa sana. Binadamu hapaswi kufuata mwendo huu ambao ni kinyume na maumbile aloumbiwa.
Mambo haya ndiyo yamekuwa yakizishughulisha jamii. Idadi kubwa ya watu haijali hatari hii inayozidi kuwa kubwa na wanaiona kama jambo la kawaida tu. Lakini takwimu zinaonesha kuwa kila siku ipitayo kiwango cha hatari kinazidi kuongezeka. Ongezeko la maradhi ya zinaa ni kigezo kikuu cha kusaidia kuonesha ukubwa wa matatizo yanayomkabili mwanadamu.
Kwa mujibu wa rekodi za Shirika la Afya ulimwenguni magonjwa yanayotokana na zinaa yanachukuwa sehemu kubwa ya maradhi. Ripoti zinaonesha kuwa kati ya kesi mpya za magonjwa ya zinaa zinazokadiriwa kufikia milioni 333 kila mwaka ulimwenguni kote, Ukimwi ndio tatizo kubwa zaidi.
Kuna ongezeko la idadi ya maambukizi ya ukimwi yanayofikia watu million 2.6 kila mwaka, na vifo vya watu visivyopungua milioni 1.8 kwa mwaka.
Takwimu za Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi tokea pale ulipoanza imefikia watu milioni 18.8. Ripoti za shirika hilo kwa mwaka 2000 zinaielezea hivi hali ya mambo: “Ukimwi una nafasi ya kipekee katika kuleta athari mbaya za kijamii, kiuchumi na katika mipango ya sensa ya maendeleo”.
Miongoni mwa mambo mabaya kabisa yanayozidi kushamiri ni ushoga. Katika baadhi ya nchi jambo hili limehalalishwa kama ndoa, linapewa heshima zote za ndoa na limeundiwa vyama na jumuiya. Duniani kote uovu huu unapingwa. Kushamiri kwa ushoga hivi leo kunatukumbusha hatima ya watu wa Lut waliokithiri katika uovu huu. Kama isemavyo Qur’an na Biblia, walipoukataa wito wa Lut kuiendea njia sahihi, Mwenyezi Mungu aliuangamiza mji na watu wake kwa maangamizi makubwa.
Ushoga wa aina yoyote ule ni Haramu kwa mujibu wa Qur'an na Biblia kwa kupitia mifano ya Kaumu Lut. Aya zifuatazo zinatufahamisha wazi kuwa Ushoga kwa jinsi yake umekatazwa kwa binadamu wote.
Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote! Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkwawacha wanawake? Kumbe nyinyi ni watu wafujaji!
Q 80-81
Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
Leviticus 18:22
"Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!"
Q 26:165-166
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti...
1 Corinthians 6:9
Mwenyezi Mungu amekataza mahusiano yoyote yale kati ya Mume na Mke, nje ya ndoa au mahusiano ya jinsia moja yaani wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake.
Mashoga wengi wakisaidiwa na wanasiasa, madaktari na wanaharakati kama vile TGNP (Tanzania Gender Networking Programme) uona ushoga kama hali ya kuzaliwa nao na ni uhuru wa mtu kuchagua aina ya maisha yake na jinsi ya kuyaendesha.
Madaktari wenye kushabikia hali hii ya ushoga, usema kuwa wengi wao mashoga wamezaliwa wakiwa na gene za ushoga kwa hali hiyo hawapaswi kwenda kinyume na matashi na matakwa ya nafsi zao kwa kuwa wameumbwa au kuzaliwa hivyo.
Swali la kuwauliza ni ili vipi wale wenye tabia ya wizi, ubakaji na uuwaji, je nao wamerithi au wamezaliwa na jene za tabia hizo za wizi na ubakaji!?
Je wale wanao waingilia wanyama (bestiality) na wanaotembea na watoto zao wa kuwazaa (incest), vipi nao wamezaliwa hivyo!?
Je madaktari wanatufahamisha nini kuhusianan na swala hili la kuzaliwa na gene zinazodaiwa kuwa zinasababisha ushoga?
Madaktari wanasema nini kuhusiana na Jambo hili:
William Byne, M.D., Ph.D., stated in his Journal of Homosexuality article "Science and Belief: Psychobiological Research on Sexual Orientation" (1995, Vol. 28, No. 3/4, pp. 303-344):
"While some authors have speculated about the existence of 'genes for homosexuality,' genes in themselves cannot directly specify any behavior or cognitive schema. Instead, genes direct a particular pattern of RNA synthesis which in turn specifies the production of a particular protein.
There are necessarily many intervening pathways between a gene and a specific behavior and even more intervening variables between a gene and a pattern that involves both thinking and behaving."
The term 'homosexual gene' is, therefore, without meaning, unless one proposes that a particular gene, perhaps through a hormonal mechanism, organizes the brain specifically to support a homosexual orientation.
Psychiatrist Jeffrey Satinover, M.D., wrote in his article "The Gay Gene?" published on the Campus Crusade for Christ International website Leadership U on 7/13/02:
"There is not any evidence that shows that homosexuality is 'genetic', and none of the research itself claims there is. Only the press and, sadly, certain researchers do-when speaking in sound bites to the public.
Homosexuality may run in families but you get viruses from your parents, too, and some bad habits. Not everything that is familial is innate or genetic."
Simon LeVay, Ph.D., stated in a 1994 interview that appears in an article entitled "Sexual Brain" published in Discover (Vol. 5, No. 3, pp. 64-67):
"It's important to stress what I didn't find. I did not prove that homosexuality is genetic, or find a genetic cause for being gay. I didn't show that gay men are born that way, the most common mistake people make in interpreting my work. Nor did I locate a gay center in the brain."
George P.A. Rice, Ph.D. et al., wrote in Science (1999, Vol. 285, p. 803a):
"We still contend that an X-linked gay gene could not exist in the population with any sizable frequency, due to the strong selection against it...
We agree with Hamer that our results do not exclude the possibility of genetic effects underlying male homosexuality. But with the use of similar methods of family ascertainment, phenotyping, and genotyping, we were unable to confirm evidence for an Xq28-linked locus underlying male homosexuality."
A. Dean Byrd, Ph.D., MBA, MPH et al. wrote in "The Innate-Immutable Argument Finds No Basis in Science," published in the May 27, 2001 Salt Lake City Tribune:
"What is clear, however, is that the scientific attempts to demonstrate that homosexual attraction is biologically determined have failed. The major researchers now prominent in the scientific arena-themselves gay activists-have in fact arrived at such conclusions.
There is no support in the scientific research for the conclusion that homosexuality is biologically determined."
Kwa ujumla madaktari wanasisitiza kuwa, jene huwa hazionyeshi kuwa mtu anaweza kuzaliwa na tabia Fulani kama vile ushoga, yaani hakuna bibadamu anayezaliwa na jene za ushoga na tafiti hazionyeshi kuwa tabia za kishoga zipo kwenye jene, bali ushoga ni hali ambayo binadamu ujifunza kutoka kwenye jamii anayoishi na si kuzaliwa nayo.
Maisha ya binadamu ni mitihani kila binadamu ana mtihani wake tofauti na mwenzake. kwa mfano kuna walozaliwa vipofu, kuna viziwi na vilema vya kila aina kuna walozaliwa katika familia za kimaskini na kuna walozaliwa kwenye utajiri, kuna walefu na wafupi wembamba na wanene... lakini licha ya ulemavu wao hali zao au maumbile yao kila mmoja anapaswa kuishi kulingana na sheria za Mwenyezi Mungu au zile tuliojiwekea wenyewe.
Kuna ambao wanaishi bila kuoa au kuolewa na kuna ambao wako mbali na familia zao wote hao hawapaswi kwenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu... Wanatakiwa wazishinde hisia zao za kingono na kufuata sheria za Mwenyezi Mungu.
Dhambi za kufanya ngono na ngono kinyume na maumbile ni moja ya mtihani mkubwa sana kuepukana nao, lakini kama utaamua kufuata matakwa na sheria za Mwenyezi Mungu kwa haki hautashindwa kuwa katika mwenendo mwema na haswa ukijikamatisha na swala/sala na dua/maombi ya kila mara basi Mwenyezi Mungu atakujaalia kushinda mitihani hiyo.
Ushoga una athari nyingi za kiafya, ni rahisi sana kuambikizana maradhi ya ngono vile vile kwa mwanamke ambaye ni shoga kutumia kwake njia za aja kubwa kujistarehesha, ujisababishia kuregea kwa kizazi na wakati mwingine ushindwa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua. Na hii ni hatari si kwa mtoto tu bali hata kwa mzazi mwenyewe.
Na kwa upande wa wanaume pia kuna athari nyingi zikiwemo kuziba mirija yake ya kiume kupungua kwa nguvu zake za kiume, na maambukizo rahisi ya maradhi.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu hakuumba mashoga na wasagaji. Hii ni hali ya tamaa ya kibinadamu, tabia hii anaipata aidha kwa kushawishiwa au kuiga kutokana na mazingira aliyokulia.
Na ujikuta baada ya mazoea ya kipindi kilefu maumbile yake na tabia zake zimebadilika na kushabihiana za upande wa pili. Athari unazozipata kwa kujifanya mke au mume yaani kuwa kinyume na maumbile yake ya asri, tabia hizo zinakupelekea kuharibika kwa mfumo wako wa kigene... Haya yanatokea baada ya kipindi kirefu cha kujifanya shoga...!
Hakujawahi kutokea mtoto alozaliwa leo akapimwa gene zake na matokeo yakasema kuwa kijana au msichana huyu atakuja kuwa na tabia za ushoga, usagaji, wizi au ubakaji...!!
Haya ni maisha ambayo binadamu anajitengenezea au kutengenezewa na wale walomtangulia au alowatangulia... Ushoga upo ndani ya uwezo wetu hiki si kilema cha kuzaliwa nacho...
Inafahamika kuwa kila binadamu ana sehemu mbili ndani ya nafsi yake yaani hasi na chanya (Positive & negative) wema na uovu. Hali hizi siku zote ushindana... Hapo ni juu yako kuamua ni kipi cha kukifuata kile ambacho unahisi kinakupendeza sasa na kikakuangamiza kesho au kile ambacho unahisi hakikupendezi leo lakini kikakuokoa kesho...
Leo hii nchi zilizoendelea kama Uingereza zimepitisha mitaala ya kufundishia mashuleni kuanzia shule za chekechea, mitaala hii ni ile ya kuwafundisha watoto wao kuwa suwala la ushoga ni jambo la kawaida tu, na kila mtu ana haki ya kuchaguwa jinsia aipendayo anapofika umri wa miaka 16.
Vitabu na vijarida vingi vimeandikwa katika kadhia hii ya kushabikia ushoga. Kuna vitabu vya watoto vyenye hekaya za kushawishi na kufundisha, kuwa kuishi na wazazi wa jinsia moja (homosexual) ni jambo jema na si jambo baya au la ajabu, kinachozingatiwa tu wewe mtoto anyanyaswi na wazazi hao wa kishoga.
Ni ngumu kidogo kuiwacha hii tabia, lakini ni jambo lililo ndani ya uwezo watu wa kuamua. Kuna masimulizi mengi ya watu ambayo walisha wahi kuwa mashoga kwenye jinsia zote mbili. Na wengi wao wamefanikiwa kuondokana na hali hii ya ushoga na wamewacha kabisa na wengi wao wameamua kuwemo kwenye ndoa za halali (ndoa ya mke na mume) na maisha yao ni ya furaha... haya hayaji tu kwa kusema mungu akipenda bali kwa kufanya jitihada za kweli na kumuomba Mwenyezi Mungu akupe wasaa na nguvu za kutotamani kurudi kwenye maangamizi...!
Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani,na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.
Q 16:90.
HAKIKA wamefanikiwa Waumini, Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao, Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,Na ambao wanatoa Zaka,Na ambao wanazilinda tupu zao...
Q 23:2
Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?
Q 16:72
Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.
Q 3:110
"Yeyote anayejinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu, na akafanya mambo mazuri, kwa hakika ameshika kishiko imara kisichokuwa na kukatika: na mwisho wa yote ni kwa Mwenyezi Mungu".
Q 31:22
Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Q 9:71
Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.
Q 3:104
Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo yachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingatoa kila fidia haitokubaliwa. Hao ndio walio angamizwa kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu.
Q 6:69
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
Q 87:9
0 comments/Maoni:
Post a Comment