Mataya 10:26-27
Walaka huu Insha'Allah nitaongelea alama mojawapo kuu na kongwe ya mojawapo ya dini yenye wafuasi wengi. Tutajitahidi kuonyesha chanzo hata uwongo unaozunguka uwepo, ujio, matumizi na maana nzima ya alama hii ya MSALABA.
Kama zilivyo alama mbali mbali, msalaba ni alama kuu (religious symbol) na muhimu ya dini ya kikristo. Wakristo wengi ukiondoa wale wa Mashahidi Jehova Msalaba kwao ni alama muhimu sana katika imani zao. Kwani inaaminiwa kuwa Bwana Yesu aliwahi kutundikwa na kufa msalabani. Alama hii ni sawa na bendera ya nchi kwa ukristo. Hivyo ni alama muhimu na yenye thamani kubwa.
Matumizi ya misalaba na aina nyingine za masanamu zilipigwa marufuku na kuonekana kuwa ni upagani, lakini mnamo mwaka ca. 675-ca.749 mtakatifu Yohana Damascene akakubali kwamba yafaa matumizi ya masanamu na aina nyingine za alama zinazo wakilisha ukristo,kwa maana ya kusurubiwa kwa Yesu pamoja na watakatifu wengine kutumika kwa kufundishia. Kikao cha mara ya pili cha Nicea 787 kikarejesha rasmi matumizi ya alama na taswira. Mnamo mwaka 814 - 43 matumizi ya masanamu na alama zingine ziliondolewa makanisani kwa kuona kuwa watu walishaanza kuziabudu. Adhabu kali ziliwafika zikiwemo kuuawa kwa wale wote walikuwa wakitumia masanamu na alama zingine zilizokuwepo wakati ule. Matumizi haya ya misalaba na masanamu yalikuja kurejeshwa tena kati mwaka 759-826 na mtakatifu Theodore.
Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la mungu-mtu Yesu wa Kikristo akiwa amebebwa na mama yake (Madona) ambaye amepewa cheo cha umama wa mungu. Yaani Theotokos (“Mother of God ca.185-ca.254”), na kwenye sanamu lingine akiwa amekufa msalabani, sanamu la "Bikira Maria", sanamu la malaika na masanamu mengine mengi ya watakatifu wa Kikristo waliokufa!
Kama maandiko ya Biblia tukufu yafundishavyo, ibada hii (ya sanamu) ifanywayo na Wakristo, kiasili imetokana na watu wa mataifa (wapagani). Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandiko yafuatayo:
"Bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao.Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao".
(Zab 106:35-36).
Kwa uchache, maandiko hayo juu yanathibitisha wazi kuwa waasisi na wahusika wakuu wa ibada hiyo (ya sanamu) ni watu wa mataifa, yaani wapagani.
Sambamba na ukweli huo, Biblia haikuacha pia kubainisha jinsi Yehovah alivyowakemea wanadamu tangu mapema kujaribu kuchonga (kufanya) na kuabudu sanamu, kama ifuatavyo:
"Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao".
(Kumb 5:8-9).
Mwandishi ya kikatholiki Adolphe-Napoleon Didron ambaye pia ni mtaalamu wa mambo ya kale (archaeologist) anasema: “The cross has received a worship similar, if not equal, to that of Christ; this sacred wood is adored almost equally with God Himself.” Some say that the cross makes them feel closer to God when they pray. Others use it as an amulet, thinking that it protects them from evil. But should Christians use the cross as an object of veneration?
Je Alama hii inastahiki kupata heshima na umuhimu huu? Hilo ndilo swali kuu la kushughulika nalo.
Ushahidi wa kwanza kuwa msalaba una chimbuko na maana kwenye dini za awali za kipagani unapatika kwenye katiba yenyewe ya ukristo yaani biblia wanayoiita wao takatifu. Soma waebrania 12:2 kwa ufafanuzi zaidi.
Pia kuonyesha ujio na uwepo wa msalaba na mkanganyiko wa jamii ya waumini inayoifuata biblia, waweza kusoma 1wakorintho1:17-18 ambapo mitume wanatukuza tendo lililofanyika kwenye msalaba na siyo msalaba kama ilivyo sasa.
Kabla ya kwenda mbali lazima tukiri kuwa uchambuzi wetu utaonyesha jinsi msalaba ulivyokuwepo kama alama ya dini za kipagani hata kabla ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu mwenyewe. Tutajaribu kufanya hivyo ili kuonyesha upagani ulivyopaganisha ukristo huku na ukristo ukikiristisha upagani na kufanya ndoa ya mashaka inayoendelea hadi leo.
Katika kamusi ya Expository of new tastment words, yaani kamusi fafanuzi ya maneno ya agano jipya, inasema kuwa msalaba kama alama ya kipagani ilianzia kule Ukaldayo (ambapo pia ndiko chimbuko la Ibrahimu). Kamusi hii inasema kuwa wapagani wa eneo hili waliitumia alama ya msalaba kama heshima yao kwa muungu wao wa kipagani aliyeitwa Tammuz ambaye kimsingi ni Nimrodi muwindaji na mwanzilishi wa himaya ya Babeli (Babylonian) iliyolaaniwa kuliko hata firauni.
Tammuz kwa ufupi aliitwa «Tau» akitumia alama ya T kama alama yake kuu au sahihi tuseme. Alama hii ya T kama ishara ya Tammuz pia ilitumika si ukaldayo tu bali hata Misri na asia wakati ule ikizingatiwa kuwa Tammuz aliweza kuabudia karibia maeneo hayo yote wakati wa himaya yake. Ezekiel 8:12-16,
Msalaba pia unaweza kupatikana katika jamii za Kimisri za kipagani za hapo mwanzo. Ushahidi huu unapatikana kule kwenye jengo la Amenopolis IV kule Tabes nchini Misri. Msalaba huu unajulikana maarufu kama « Msalaba wa Misri au Msalaba wa tau. Hii ni kutokana na baadhi ya kazi za wanahistoria maarufu wa zama zile. Msalaba huu ulikuwa na mduara upande wa kichwani ukiashiria alama ya Tammuz akiwa kama muungu jua hapo baadaye.
Pia katika maeneo ya Ufoenike, China na Mexico inapatikana dhana nzima ya matumizi ya kidini ya msalaba kama alama yao kuu. Ikumbukwe kuwa yote hii ni kabla ya kuzaliwa kwa Yesu hivyo kabla ya ukristo.
Jamiii nyingine unapopatikana msalaba kama alama shufaa ni maeneo kuanzia nchi ya Niger ya sasa hadi mto Nile. Kwani ngao za mashujaa wa eneo hili zilichorwa alama hii kama ishara ya utaua na ukuu. Vile vile kwenye dini ya Uhindu unajulikana kama The swastika, wagiriki wao wana msalaba unao itwa crux gammata, composed of four Greek uppercase gammas (Γ),
Ushahidi madhubuti waweza kupatikana pia nchini Mexico ambako msalaba maarufu wa Palengue unapatikana. Kwa anayetaka ushahidi zaidi juu ya hili aweza kusoma kwenye

“The catholic encyclopidia“ ambayo licha ya kuuita msalaba wa Palengue inauita msalaba wa kabla ya ukrist wa Palengue.
Msalaba huu nchini uliitwa pia Tota ama baba kama ambavyo baadaye uliitwa kwenye biblia. Soma Yeremia 2:27 hii imebainika kuwa upotofu mkubwa kuanzia lugha hata matumizi ya neno baba kumaanisha msalaba.
Nchini Misri inapatikana pia michoro au picha ya Muungu Amon akiwa ameshikilia msalaba wa Tau.
Pia kwenye hekalu la serapis kule Alexandria lilibeba alama ya msalaba.
Hata kwenye vita baina aya Alexander Mkuu (Alexander the great), na waajemi, waajemi walibeba msalaba kama alama yao ya ushindi. Pia hapa ikumbukwe kuwa utumizi wa alama ya msalaba kwenye vita ilianzishwa na akina Nebkadneza na wenzake kama alama ya ushindi.
Kwa ufupi angalau msomaji anaweza kuona utamaduni huu wa kuutukuza na kuutumia msalaba ulikotoka kuwa ni kwenye dini za kipagani za kale. Hiki ndicho tulichomaanisha tuliposema kuwa upagani umepaganisha ukristo na ukristo umekristisha upagani na kufanya ndoa kuu ya uwongo na mashaka.
Hebu tuhame twende nchini Italia ambako ndiko chimbuko hasa la ukristo chini ya himaya ya kiroma. Mwaka 46 kabla ya kuzaliwa Yesu, kunapatikana sarafu za muungu jupiter zikiwa na alama ya msalaba ambao kwa wapagani wa kiitaliano ulitumika kama hirizi au sihiri kama unavyotumiwa na baadhi ya madhehebu ya kikristo kwa sasa.
Hata ukiangalia sarafu aliyoletewa Yesu alipe kodi ilikuwa na Maandishi Partem max yaani baba mkuu ambaye alikuwa ni kaizari, ilikuwa na alama ya msalaba. Hilo leo siyo mjadala wetu hivyo tutalitumia kwenye ushahidi huu tu.
Hata kule Ugiriki ulichorwa msalaba kwenye vibanio na nembo ukiwa ni alama ya mfalme wao aliyefanana sana na Tammuz.
Tusiwachoshe na rejea na ubukuzi na uchokonozi. Hebu tujiulize swali rahisi. Je msalaba hadi hapa ni alama ya Kimungu au kimiungu? je inaingia akilini hadi leo mtu kuendelea kuutukuza na kuuvaa shingoni ikiwa ni kama kinga au hirizi kwake? je kama mtu atategemea kulindwa na msalaba huyo Mungu atafanya kazi gani!?
Je inaingia akilini kuendelea kuutumia msalaba kwenye mahekalu ya Mungu, nyumba zetu, makaburi yetu, kuuchora kwenye vipaji vya uso kila mtu aingiapo kanisani na mengine kama hayo? Je ni nani mwehu huyo awezaye kuivaa shingoni bastola au kisu kilichotumika kumuua mpendwa wake kama kinga au japo kumbu kumbu tu? kama hata akili nyepesi ingetumika basi bastola ingeogopewa kiasi cha kutisha kwani ndiyo iliyouchukua uhai wa mpendwa wako. Je ni nini mantiki ya wakristo kuvalishwa kongwa bila wenyewe kujua asli?
Je inaingia akilini kwa mtu ambaye amejua maana na chimbuko la msalaba kuendelea kuivaa hiyo kongwa na alama ya laana? kazi kwenu. Je anayefanya hivyo anaendelea kuwa mkristo wa kweli au mpagani wa kawaida tu hata akijiita mkristo?
Hatulengi kudhalilisha imani za wenzetu wala kuwaonyesha kama majuha lakini ni ujuha kutumia alama ya kipagani ambao kimsingi ndiye adui mkubwa wa dini. Tunaandika haya kwa kuzingatia ushauri wa bure lakini wa maana. Yesu Alisema kuwa mkiitafuta kweli itawaweka huru kweli kweli. Kama hivyo ndivyo kwanini nasi tusiwaweke huru kweli kweli ?
Kwa taarifa yako msomaji msalaba umekuwa nongwa hasa kwa wakatoliki. Kwani huchora alama ya msalaba kila waingiapo kanisani, kunywa au kula, wakati wa kulala wakati wa kuamka n.k Pia msalaba huchorwa kwenye mwili wa mtu tangu siku ya kuzaliwa (kubatizwa) hadi kuzikwa huku kaburi lake likiubeba milele !
Kwa waroma msalaba uko kila mahali. Kwenye meza, makanisa, hata tumbo la kanisa limejengwa kwa ishara ya msalaba, hata kwenye vikombe wanavyotumia kanisani hufunikwa kwa kitambaa chenye alama ya msalaba. Kwa taarifa yako ni kwamba padre hufanya alama ya msalaba mara 16 wakati akiendesha misa huku akiongeza mara 30 za kuibariki altare!
Kama kweli msalaba ni alama ya laana na ya kipagani huku ni kufanya nini kama siyo kuwalaani waumini hata madhabahu yao. Je hapa kunaweza kuepukika kwa mabalaa na majanga yanayolikumba kanisa kama vile ulawiti na uzinzi wa mapadre wake?
Imekuwa ni jadi kwa mkristo kujilaani kwa kila afanyalo. Hali wala hanywi bila kujitia alama hii ya laana.
Hata tukiambwa kuwa msalaba unatumiwa kama alama ya kusulubiwa kwa Yesu ambaye ni alama ya ukombozi wa kinjozi, bado haiingii akilini kwani zana na nyenzo hii ilianza kutumika kabla ya kuzaliwa na kusulubiwa kwake.
Je ni wapi ukiachi siku ya kusulubiwa ulipoona Yesu na wanafunzi wake wakiongozana na msalaba kwenye shughuli zao za kueneza injili?
Tuhitimishe. Huko Misri, Ugiriki , Syria na Karthago, Palestina na Roma msalaba pia ulitumika kuwaadhibia wahalifu waliokuwa wametenda maovu makubwa kama alama ya kulaaniwa kwao.
Kimsingi msalaba na matumizi yake vimepotoshwa sana kama ilivyo kwa dhana kuu ya ubaba. Soma Matayo 23:9-11. tukiache magube ya kanisa, hili liko wazi kuwa msalaba hauna uhusiano na ukristo wala dini aliyoileta Yesu. Huenda tukikubali kusema kuwa Ukristo siyo dini aliyoleta Yesu twaweza kuyakumbatia na kuyakubali matumizi ya msalaba kwa raha bila ubishi.
Lakini si kosa la kanisa. Kwani kama hadi leo halijamjua Yesu mwenyewe litajuaje upogo na najisi ya msalaba kwa kazi ya Mungu?
Tuhitimishe kwa kumnukuu Bwana J. D. Parsons katika kitabu chake kiitwacho The Non-Christian Cross anaelezea kuwa:
“There is not a single sentence in any of the numerous writings forming the New Testament, which, in the original Greek, bears even indirect evidence to the effect that the stauros used in the case of Jesus was other than an ordinary stauros; much less to the effect that it consisted, not of one piece of timber, but of two pieces nailed together in the form of a cross.”
Nakaribisha hoja juu ya kuyavinjari haya tunayoletewa. Huu ndiyo wakati muafaka wa kuhoji na kuhoji na kuhoji hadi kweli ipatikane ili ituweke huru kweli kweli.
NB:
Ushahidi kutoka Encyclopedias Maarufu Katika nyanja za Elimu
Cross, ancient symbol found in many cultures, but especially associated with Christianity.
The cruciform design consists essentially of two lines that intersect to form right angles. There are many variations. The tau (Greek letter ‘t’) cross, for example, is T-shaped; the Saltire, or St. Andrew's cross, is X-shaped. In the Latin cross, the short horizontal member is near the top of the longer vertical member; in the Greek cross, the members are of equal length and intersect in the center. The Russian cross has two unequal horizontals set on the vertical member above a small slanting bar. The cross of Lorraine has two unequal horizontals; the papal cross has three unequal horizontals, with the shortest near the top end of the vertical member. The Maltese cross is a Greek cross with V-shaped members widening from the center and being notched at the ends. The crux ansata (Latin for “cross with handles”), or ankh, is a tau cross with a circular loop above the horizontal bar. The Celtic cross is like a Latin one with the addition of a circle surrounding the intersection. In the swastika (fylfot cross) the members, of equal length, are bent at the ends.
(Microsoft® Encarta® 96 Encyclopedia. © 1993-1995)
Cross forms were used as symbols, religious or otherwise, long before the Christian Era, but it is not always clear whether they were simply marks of identification or possession or were significant for belief and worship. Two pre-Christian cross forms have had some voguein Christian usage. The ancient Egyptian hieroglyphic symbol of life—the ankh, a tau cross surmounted by a loop and known as crux ansata—was adopted and extensively used on Coptic Christian monuments. The swastika (q.v.), called crux gammata, composed of four Greek capitals of the letter gamma, is marked on many early Christian tombs as a veiled symbol of the cross.
There are four basic types of iconographic representations of the cross: the crux quadrata, or Greek cross, with four equal arms; the crux immissa, or Latin cross, whose base stem is longer than the other three arms; the crux commissa, in the form of the Greek letter tau, sometimes called St. Anthony's cross; and crux decussata, named from the Roman decussis, or symbol of the numeral 10, also known as St. Andrew's cross. Tradition favours the crux immissa as that on which Christ died, but some believe that it was a crux commissa. The many variations and ornamentations of processional, altar, and heraldic crosses, of carved and painted crosses in churches, graveyards, and elsewhere, are developments of these four types.
(Encyclopaedia Britannica 2005 Standard Edition)
0 comments/Maoni:
Post a Comment