Miungu Ya Kipagani


Dini ya Kiislam inatafautiana sana na dini nyengine katika kila Nyanja, hususan kwenye swala zima la ibada. Dini ya uislam inakataza suala zima la shirk na kumshirikisha Allah (SWT).

Swala la shirk ni dhambi iliyo kubwa kabisa kuliko dhambi nyingie yoyote, na MwenyeziMungu hasamehi dhambi ya kumshirikisha kwa yeyote anayemshirikisha na uku anajuwa kuwa hili jambo ni shirki.

Waislam wengi tunajuwa mambo mengi ya shirki na athali zake, na Alhamdulillah tunajitahidi kuwa mbali na kila shirki. Lakini washirikina nao hawachoki kutuletea bidhaa na mambo mengi ambayo yana asili ya kumshirikisha Allah (SWT) na kwa bahati mbaya waislam wengi hatufahamu ili. In-sha-Allah basi na tuangalie baadhi ya alama na majina ambayo aidha tunayajuwa na tumeamua kuyadharau kwa sababu ni ushirikina unao tokana na dini ambazo hatuzijui au hatujui kwa sababu hatufahamu kama ni ushirikina, au kwa sababu ushirikina huo umekubalika kimataifa na unatumika katika mambo ya kawaida na hatuoni athari zake.

NIKE

Miongoni mwa alama za kikafiri na kishirikina ukiondoa misalaba ya kikristo, ambazo zinapingana na Qur’an ni lile jina na alama inayo tumika kwenye viatu vya NIKE.
Jina ili ni miongoni mwa miungu ya kike ya kiyunani (yaani Wagiriki), wa zamani. Na huyu ni mungu mke wa ushindi. Wenyewe walikuwa wanaamini kuwa mungu huyu mke anauwezo wa kukimbia na kuruka na ana huwezo wa kwenda kasi kuliko kiumbe yoyote yule duniani.

Wapagani wa kileo wanamuona mungu NIKE kama ni mleta bahati katika mambo mengi hususani kwenye michezo mbalimbali.

JANUARY

Jina jingine ambalo huwa tunalitumia bila kujuwa ni jina la mwenzi wa kwanza ktk kalenda ya gregorian (Gregorian Calendar) nalo ni January. Ili ni jina linalotokana na Janus mungu wa kirumi mwenye vichwa viwili wakati mwingine huwa na vichwa vinne. Na alikuwa akiabudiwa katika msimu wa mavuno. Ni mungu wa lango kuu au mwanzo. Na ndio mana jina lake likawekwa kuwa la kwanza ktk kalenda tunazo tumia sasa. Na miongoni mwa wake zake ni Juturna na Jana.

MARS

Jina jingine ambalo huwa tunalitumia bila kujuwa ni jina la mwenzi wa tatu ktk kalenda ya gregorian nalo ni March. Ili ni jina linalo tokana na jina Martius na hili ni jina la Mungu wa kirumi wa vita au kwa jina lingine ni MARS.

Mars pia ni moja ya sayari ktk ulimwengu huu tulio nao, na pia ni jina la chocolate maarufu sana ulimwenguni.

APRIL

Jina jingine ambalo huwa tunalitumia bila kujuwa ni jina la mwenzi wa nne ktk kalenda ya gregorian nalo ni April. Ili ni jina linalo tokana na jina aprillis (Latin). Na hii si ajabu kwa sababu baadhi ya majina ya wiki na miezi ktk kalenda yanatokana na kuwaenzi miungu au watawala aidha ya kiyunani ama kirumi. Jina hili kwa kiyunani ni Aphrilis au kwa kigiriki ni Aphrodite na huyu ni mungu wa mashujaa.

MAY

Jina jingine ni la mwezi watano. Nalo ni mwezi MAY, jina hili linatokana na jina la mungu wa kike wa kigiriki aitwaye Maia. Na huyu ni mungu wa kurutubisha uzazi.

JUNE

Jina jingine ni la mwezi wa sita June huyu ni mungu wa kike wa kirumi aitwae Juno mke wa mungu jupiter (kwa bahati mbaya nyingine jupiter ni moja ktk sayari kubwa kabisa ulimwenguni) na Juno alikuwa anahesabika nguvu zake sawa na mungu mke wa kigiriki aitwae Hera.

JULY

Jina lingine ni la mwenzi wa saba July, ili ni jina la mtawala wa kirumi aitwae Julius Caesar. Kabla ya hapo mwezi huu ulikuwa unajulikana kwa jina la Quintilis kwa kilatini.

AUGUST

Jina lingine ni la mwenzi wa nane August, ili jina linatokana na jina la mtawala wa kirumi aitwae Augustus Caesar. Kabla ya hapo mwezi huu ulikuwa unajulikana kwa jina la Sextilis kwa kilatini. Augustus Caesar baadae naye alidai uungu kabla ya kifo chake.

MAJINA YA WIKI

Monday au juma tatu kwa Kiswahili ni jina linalotokana na mungu wa mwezi (moon) aitwae Mani na limetokana na asili ya kiscandinavian 

Tuesday ni jina linalotokana na mungu aitwae Tyr ni mungu wa mapambano ya watu wawili tu yaani single combat. Pia tyr ni mungu wa kiscandinavian.

Wednesday ni jina linalotokana na neno Wodnesdæg (kiingereza cha zamani). Na hili ni jina la mungu wa kijerumani aitwae Woden.

Thursday ni jina linalotokana na neno Þunresdæg au siku ya Thor (Þunor) kwa kiingereza cha zamani. Huyu ni mungu wa radi kwa imani ya dini ya kirumi. Na kigerumani.

Friday ni jina linalotokana na neno frigedæg au Frige ni mungu mke wa kigerumani, huyu ni mungu wa urembo na kwa kirumi alikuwa anajulikana kwa jina la venus. Venus ni moja katika sayari ulimwenguni.

Saturday (Saturn) ni mmoja wa miungu katika dini ya kale ya Kirumi. Yeye ni mungu wa kizazi, vifo, utajiri, kilimo, na harakati za ukombozi. Katika maendeleo ya baadaye alikuja kuwa ili ni jina la mungu wa wakati (time).

Sunday ni jina la mungu mke, jua aitwae sunna au sunne huyu ni mungu wa kigerumani 

Majina haya ya wiki yametokana na majina ya miungu iloletwa na watawala wa anglo saxon (Northern Europe).

MAJINA YA SAYARI

Jupiter ni mungu wa kirumi sawa na zeus na alikuwa anajulikana kama Jupiter Optimus Maximus (Jupiter Highest, Greatest). Pia jupiter ni sayari ya tano kutoka kwenye jua.

Uranus ni mungu wa anga wa kigiriki. Pia ni sayari ya saba toka kwenye jua.

Neptune ni mungu wa kirumi wa bahari na ni kaka yake na Jupiter, vilevile ni sayari ya tisa toka kwenye jua.

Mercury ni mmoja ya miungu mikubwa ya Kilatini na Kirumi. Yeye ni mlezi na mwenye kufanikisha upatikanaji wa fedha kwenye biashara, ufasaha kwenye ushairi, ujumbe / mawasiliano, pamoja na uaguzi, kulinda wasafiri, mipaka, kusaidia bahati pamoja na wezi; yeye pia ni kiongozi wa roho kwa wafu.

Venus ni miongoni mwa miungu mikubwa ya kirumi na huyu ni mungu mke. Amabye ni mungu wa upendo na urembo (love and beauty). Na inafikiriwa na warumi kuwa ndio chazo cha warumi

Pluto ni miongoni mwa sayari zinazo lizunguka jua ulimwenguni. Na jina ili linatokana na jina la mungu wa kirumi. Wakigiriki wao wanamwita Hades. Na huyu ni mungu wa wafu. Na kwa asili ya jina lake ni Ploutos au mali (wealth). Mgawa zawdi za dhahabu na fedha. Alilaanika baada ya kumteka mama yake na kutaka kumuoa.

MIUNGU WENGINE:

Hestia au Vister mungu mlinzi wa majumbani. Kampuni ya Microsoft imalitumia jina ili katika moja ya operating system zake (Windows Vista)  

Demeter au Ceres mungu wa nafaka. Kwa watumiao cerelac watambue kuwa jina hilo limetokana na mungu huyu. Vilevile ni moja ya sayari ndogo zilizoko katika utawala wa jua… Ceres pia ni mungu wa uzazi na mahusiano ya watu. 

Hephaestus au vulcan kwa warumi huyu ni mungu wa mioto na wahunzi. Na kutokana na jina hili tumepata neno volcano.

Mazda ni jina la mungu wa kiajemi na jina lake haswa ni Aura mazda, pia ni jina la aina ya gari.

Apollo ni mungu wa kigiriki na kirumi. Huyu ni mungu wa utume na na matibabu vile vile ni mungu wa jua.

Hypnos au Somnus mungu wa usingizi, kutokana na neno ili ndio tunapata neno hypnotize kwa Kiswahili chepezi tunaweza kusema (hypnotize – hali ya kupumbaza akili)

Gaia au Terra Mater ni mama wa ardhi, vilevile ndio mpaji watu uzazi na mrutubishaji ardhi.
Kwenye ulimwengu wa computer limetumia neno Terabyte 


Allahu yaalam

0 comments/Maoni: