KWA NINI NGURUWE (WHY PIG)

KWA NINI NGURUWE (WHY PIG)
Katika viumbe vinavoliwa na binadamu ambavyo Mwenyezi Mungu (swt) ameviharamisha ni Nguruwe. Japokuwa nyama ya Nguruwe inaliwa kwa kiwango kikubwa sana katika nchi za Ulaya, Amerika, Asia na baadhi ya nchi za Afrika. Bado Nguruwe ataendelea kuwa ni mnyama aliye najisi kubwa kabisa. Hasa katika jamii za waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) kwenye Qur'an anasema hivi:

Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na Nyama ya Nguruwe,
Na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ā€¦
Qur'an 5:3

Kwa nini basi Nguruwe awe ni haramu kwa waislamu na kwa baadhi ya watu wengi?
Kwa waislamu jibu lake ni rahisi mno. Kwani hiyo ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Na waislamu hatuna budi kuitekeleza kwa hali na mali.
Lakini je, ukiamua kuila kwa sababu ni nyama inayo onekana kuwa imenona sana, ili uweze kujipatia afya iliyo bora. Je unafikiri takuwa umefaidika? Jibu lake ni kuwa utakuwa ni mwenye kuikharifu amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa kukataa kuitekeleza amri yake, kwa hali iyo atakuadhibu hapa duniani na kesho akhera.
Pili utakuwa ni mwenye kujitia hasara kubwa katika afya yako. Kwani katika uislamu kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha tulitekeleze au tusilitekeleze basi linafaida kimwili na kiroho.
Wataalamu wa Lishe baada ya kufanya uchunguzi wa muda mrefu kuhusu nyama za aina mbalimbali, ikiwemo nyama ya Nguruwe, wakaja kugundua kuwa nyama ya nguruwe si nzuri kabisa kuitumia. Kwani imeonyesha kuwa inaongoza kuwa na vijidudu vya maradhi yasiyo tibika. Japokuwa nyama za Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo na nyinginezo zimeonekana kuwa na vijidudu kiasi Lakini vijidudu hivyo vya wanyama wengine wanaoliwa kihalali vinaweza kutibika bila matatizo yoyote, kulinganisha na nguruwe. Kwani nyama ya nguruwe hata ukiichoma na kuwa majivu bado baadhi ya vijidudu havitakufa kabisa. Kwani baadhi ya vijidudu hujitengenezea kinga au Cyst. Cyst ni kinga ambayo baadhi ya vijidudu hujitengenezea ili visidhurike.

MARADHI NA VIJIDUDU KTK NGURUWE:
Nguruwe ni chanzo kikubwa sana cha maradhi ya aina mbalimbali yasiyo tibika, nguruwe ana vijidudu vya maradhi aina zaidi ya 20,000. Hebu na tuangalie baadhi tu ya vijidudu ambavyo vinapatikana kwenye nyama ya nguruwe.

Protozoan Ciliate. (Balantidium Coli):
Hiki ni kijidudu chenye chembe hai moja, na kinaishi katika utumbo mpana wa nguruwe. Kijidudu hiki licha ya kusambazwa kwa kupitia ulaji wa nyama ya nguruwe pia husambazwa kupitia kinyesi chake. Pale kinapotumika kama mbolea. Mdudu huyu anasababisha maradhi ya kuhara damu. Maradhi haya yanapatikana sana katika nchi zile ambazo watu wana mahusiano makubwa na nguruwe.

Trichinella Spiralis (Trichina):
Vijidudu hivi hukaa katika misuli ya nyama ya nguruwe, na pale inapoliwa husababisha udhaifu mkubwa sana kwenye mwili wa binadamu, kwa sababu si mkazi asilia katika mwili wa binadamu. Mdudu huyu anauwezo wa kuishi hadi kufikia miaka arobaini (40) akiwa mwilini mwa binadamu. Hupendelea kukaa kwenye utumbo mdogo wa binadamu, baadae ujipenyeza na kuingia katika mzunguko wa damu na kusambaa mwili mzima na kushambulia maeneo mbalimbali ya mwili wa binadamu. Mfano hushambulia mishipa ya damu na husababisha kuvuja kwa damu, ndani kwa ndani (Internal Bleeding), hushambulia kioo cha jicho (Retina) na kusababisha upofu (Blindness), hushambulia mapafu na mafuta yaliyoko kwenye mifupa, na misuri ya moyo, pia husababisha Baridi yabisi (rheumatism), kupooza kwa misuri (Muscular Paralysis), ugonjwa unao sababisha upungufu wa damu mwilini yaani saratani ya damu (Anaemia).

Taenia solium (Pork tapeworm): Tegu. Tegu ni minyoo anayosababisha mwili kukosa lishe na kupelekea kupata utapia mlo, na pia hushambulia sana ini, husababisha kuhara (Diarrhoea), uleta ugonjwa wa uzuni (Melancholia) na kushindwa kwa usagaji wa chakula (Digestive Disturbances). Na kuharibu uti wa mgongo (Spinal cord).

Roundworms: Kuna aina zipatazo 12,000 za Roundworm, wakiwemo hookworms au Filarial ambao uleta maradhi ya matende. Pia husababisha maradhi ya homa ya Manjano (Jaundice) kutosagwa vizuri kwa chakula (Digestive Disturbances), kuziba kwa kidole tumbo (Appendicitis).

Hookworms:
Zaidi kusababisha maradhi ya saratani ya damu (Anaemia) na magonjwa ya homa ya matumbo yaani kuharisha (Typhoid), pia husababisha utapia mlo, na maradhi ya moyo (Heart Failure), safura, Mtindio wa ubongo au utaahira (Mentally Retarded). Na hali ya kutojali (Apathy). Pamoja na kifua kikuu TB (Tuberculosis)

Faciolopsis Buski: Ni vimelea ambavyo hukaa katika utumbo mdogo wa nguruwe pia husababisha kuharisha damu kutosagwa vizuri kwa chakula (Digestive Disturbances).

Paragonimus: Ni kimelea kinacho ishi kwenye mapafu ya nguruwe na kinasababisha maradhi ya Pneumonia na kuvuja kwa damu katika mapafu.

Clonorchis Sinesis:
Husababisha magonjwa mabaya sana ya kuvimba Ini na kifua kuchoka, ulegevu na kupata ugonjwa wa uzuni (ulio kama aina ya wazimu hivi).

Erysipelothrix: Mdudu huyu husababisha maradhi yanayojulikana kwa jina la Erysipelas, ugonjwa huu husababisha kuharibika kwa ngozi ya mwili, kuwa na mabaka mabaka yakiambatana na homa kali. Vile vile nyama ya nguruwe husababisha ugonjwa wa kutoa mimba unaoitwa Brucellosis (Malta fever).

The pig is full of pus: -
Pus ni majimaji ya njano (yanayo fanana na Usaha) ambao husababishwa na kuharibika kwa tishu na kufa kwa chembe chembe nyeupe za damu (white blood cell), na hii husababishwa na aina ya bacteria, protozoan pamoja na kufu (fungal) na uharibu ngozi, fizi, mifupa, na baadhi ya viungo (Organs) kama vile ini, mapavu, na ubongo. Maeneo yalioathirika uvimba na kuwa mekundu, na husababisha maumivu makali na kusababisha joto la mwili kupanda, na kumsababishia muathirika kupata homa kali. Na hii huweza kumsababisha kifo kwa mgonjwa kama hatawahi kutibiwa.
Vile vile nguruwe husababisha maradhi mengi yanayo ambukiza, yanayotokana na bakteria na virusi (Bacterial and viruses Diseases). Kama vile kifua kikuu (Tuberculosis), kipindupindu (Cholera), pepopunda (Lockjaw), kuoza kwa sehemu za mwili (Gangrene), ukoma (Leplosy), na ugonjwa wa Tauni (Plague). Kaswende (Syphilis), ugonjwa wa donda koo (Diphtheria)
Kwa bahati mbaya sana matibabu ya magonjwa yanayotokana na nguruwe hayajapatiwa dawa ya kuyatibu au kuponyesha kabisa, isipokuwa ni kutuliza tu kwa muda. Dawa hapa ni kuacha kutumia nyama ya nguruwe.

TABIA YA BINADAMU NA ULAJI WA NYAMA YA NGURUWE

Binadamu ameumbwa katika hali ya kimwili, kiakili na kiroho. Makazi ya akili ni katika ubongo. Ubongo ambao hupata lishe na chembe hai (cell) mpya kutokana na vyakula tunavyokula. Vyakula tunavyo kula husaidia sana kuzalisha chembe hai mpya katika mwili wa mwanadamu ili kuchukua nafasi ya zile zilizo kufa. Cell ambazo baadhi yake ndizo hizo zinazo tengeneza cell za ubongo. Ambamo humo kwenye ubongo ndimo kunapopatikana Akili. Unapokula nyama ya ngururwe jua kuwa mafuta yake huwa hayatumiki mwilini, kinachofanywa na mwili wa binadamu ni kuyarundika mafuta hayo chini ya ngozi, na kwenye mishipa ya damu, na kwenye chemba za moyo na kwenye ini. Na hii baadaye husababisha ongezeko la mwili kupita kiasi, kuwa na wasiwasi, kutojiamini, maradhi ya moyo, na mwili kukosa nguvu. Na kutoweza baadhi ya viungo yaani ogani kutofanya kazi vizuri. Pia protini inayopatikana kutokana na nyama ya nguruwe ndio inayo kwenda kurutubisha DNA zako na hapo ndipo unapoanza kurithi tabia na mienendo ya nguruwe. Kwani katika DNA ndimo kunapo patikana kila kitu kinacho muhusu binadamu. Kuanzia tabia, umbo lake na kila kitu kuhusu binadamu. Na sasa hebu fikiria kuwa DNA inakwendwa kubadilishwa kulingana na unachokula na chakula chenyewe ni nguruwe je unafikiria itakuwaje na sisi sote tunakuwa hivi tulivyo, kulingana na tunavyokula.
Tufahamu kuwa chakula kilicho safi na halali, na kilichopatikana kwa kheri na kuliwa kwa mawazo ya amani ujenga athari njema katika mwili na akili ya binadamu. Lakini chakula kichafu au kiliwacho katika machafuko ya kiroho hudhuru mwili na akili.
Nguruwe japokuwa anapendwa kuliwa na watu wengi, bado anakuwa ni alama ya uchafu, ufisadi, uasherati na ulafi wa kupapia visivyo halali. Nguruwe amekuwa ni chanzo cha uharibifu wa tabia za watu walio wengi. Watu wengi huathiriwa polepole na tabia za nguruwe pale wanapokula nyama hii bila ya wao kujua. Mambo ya uasherati ukosefu wa adabu watu kukosa haya na huruma ni vitu vya kawaida sana katika jamii inayokula nguruwe, na unyoofu wa maadili huwa ni kama jambo lisilowezekana au lililopitwa na wakati. Watu huwa na tabia mbaya za ubinafsi na ukatili usio na sababu ni jambo la kawaida mno. Hebu leo hii Angalia vichwa vya habari vya magazeti mengi hapa nchini mengi yao habari wanazopenda kuziandika ni zile za ngono na za waendao uchi. Leo hii zinaa ni jambo la kawaida sana mfano tendo la kubaka linaonekana ni sawa na kumpiga mtu kofi la shavu tu, nao wanadai waonewe huruma kwani jambo walilolifanya ni la kawaida tu halihitaji adhabu kubwa. Huu ni msiba mkubwa katika jamii zetu hizi. Mambo ya kubadilishana wake, watu kuishi na vimada kuingiliana kimwili kwa makundi (group sex), kutembea uchi (Nudism) na kadhalika haya yote yanapatikana pale tu ulaji huu wa nyama ya nguruwe unaonekana kama ni jambo la kawaida katika jamii. Hebu angalia nchi za Amerika na Ulaya zilivyo haribika kitabia. Watu wake wengi si wastaarabu hata kidogo, ukilinganisha na nchi ambazo hakuna ulaji wa nyama za nguruwe. Sisemi kuwa katika nchi ambazo ulaji wa nyama za ngurwe ni mdogo au hakuna kabisa kuwa hakuna uasherati la. Sisemi hivyo ila katika nchi ambazo ulaji wa nyama hii ni mdogo au hakuna kabisa matendo ya uzinzi na ukahaba ni matendo ya aibu sana kwa wana jamii, tofauti na nchi zinazokula nyama ya nguruwe. Kwani katika nchi hizo za ulaji wa nyama hii kwa wingi tendo la kucheza au kutembea uchi ni kitu cha kawaida na huitwa kuwa ni sanaa, na wala si utovu wa maadili. Kwani matendo hayo ya kutembea uchi yanapata baraka za wanajamii na serikali kwa ujumla.
Mambo haya yanapozidi na kuendela na kuonekana ni mambo ya kawaida katika jamii. kidogokidogo jamii huharibika na kurithisha tabia hizi chafu hasa kwa watoto wanaochipukia. Na kwa wale wanaopenda kuiga kila jambo linalopigiwa debe na vyombo vya habari. Kwani wakubwa wao tayari wamekwsha athirika na tabia hizi za uasherati na uzinzi.

Ndugu msomaji kwa ili unaweza kufanya utafiti mdogo tu, kwa kulinganisha maeneo au watu wanaokula nyama ya nguruwe na wale wanao pendelea kutokula nyama ya nguruwe. Hususani watu wanokula samaki au mboga za majani (vegetarian). Au walaji wa nyama za ng'ombe na mbuzi.
Mwenyezi Mungu kwenye Qur'an anasema hivi;

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.
Q57: 4-5

Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu,
wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake.
Ni machache mnayo yakumbuka
.
Q.7: 3

0 comments/Maoni: