PASAKA

YALIYOMO:
• Utangulizi
• Ukweli wa Pasaka kama alivyofundisha Mungu
• Utaratibu aliouweka Mungu wa kumla Pasaka
• Siku na muda aliouweka Mungu wa kuchinja na kumla Pasaka
• Lengo sahihi la Mungu kuweka sikukuu ya Pasaka
• Dhana ya kufa na kufufuka kwa Yesu si mafundisho ya Mungu
• Misalaba
• Yesu mwenyewe aliwahi kumla Pasaka
• Mapinduzi ya Paulo dhidi ya Pasaka aliyefundishwa na Mungu!
• Azma ya Paulo dhidi ya mafundisho ya Mungu tangu awali
• Hitimisho

Utangulizi
Pasaka ni mnyama anayechinjwa kukumbuka kukombolewa Waisraeli Misri, siyo 'kufa' kwa Yesu. Ilikuwepo kabla hata Yesu hajazaliwa, Yesu mwenyewe alikula Pasaka.

Kinyume na ukweli wa mambo, hivi sasa sikukuu ya Pasaka imegeuzwa na Wakristo duniani kuwa ni siku ya kukumbuka "kufa na kufufuka kwa Nabii ama Yesu (a.s.)". Ambapo tangu kuasisiwa kwa dini ya Kikristo miaka michache baada ya Yesu (a.s.) kuondoka, dhana hii (ya kufa na kufufuka) imefanywa na Wakristo kuwa nguzo kubwa na ya msingi wanayoitegemea kusimamisha Ukristo. Fuatana nami ili uweze kuangalia kwa undani ukweli wa sikukuu hii (ya Pasaka) na dhana nzima ya kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu (a.s.).

Ukweli wa Pasaka kama alivyofundisha Mungu
Kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia, Pasaka ni mnyama ambaye wana wa Israeli waliamrishwa na Mungu wamchinje na wamle kwa kufuata utaratibu aliouelekeza Mungu na kwa lengo maalum. Maandiko yafuatayo yanathibitisha ukweli huu:
"Hapo ndipo Musa aliwaita wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana kondoo kama jamaa zenu zilivyo, mkamchinje Pasaka". (Kutoka 12:21),

"Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake". (Kumbukumbu la Torati 16:2),

"Usimchinje Pasaka ndani ya malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, ila mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinja Pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri". (Kumbukumbu la Torati 16:5-6).

Kulingana na maandiko hayo juu, tunaona hapa Biblia inafundisha wazi kuwa Pasaka ni kondoo au ng'ombe ambaye Mungu aliwaamuru wana wa Israeli wamchinje kisha wamle. Aidha, maandiko hayo yanaonyesha wazi pia kuwa amri hiyo (ya kuchinja na kumla Pasaka) haikuwahusu watu wa mataifa mengine isipokuwa Waisraeli peke yao.

Utaratibu aliouweka Mungu wa kumla Pasaka
Pamoja na wana wa Israeli kuamriwa na Mungu kumchinja Pasaka, Mungu pia aliwawekea utaratibu (sheria) wa kumla (Pasaka) kama tunavyosoma katika maandiko yafuatayo:
"BWANA akamwambia Musa na Haruni, Amri ya Pasaka ni hii;
mtu mgeni asimle; lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla Pasaka. Akaaye kwenu hali ya ugeni, na mtumishi aliyeajiriwa, wasimle Pasaka. Na aliwe ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote; wala msivunje mfupa wake uwao wote. Na wafanye jambo hili mkutano wa Israeli wote. Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia BWANA Pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya Pasaka, naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle. Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini. Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyowaagiza Musa na Haruni; ndivyo walivyofanya".
(Kutoka 12:43-50)

"BWANA akanena na Musa, akamwambia, mtu wa kwenu, au vizazi vyenu, yeyote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA; mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; wasisaze kitu chake chochote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake, kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. Lakini mtu aliyesafi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atakataliwa mbali na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake. Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi". (Hisabu 9:9-14).

Kwa kifupi, kama maandiko hayo yanavyoeleza, huo ndio ulikuwa utaratibu wa kumla Pasaka, ambao Mungu aliwawekea wana wa Israeli. Aidha, maandiko hayo nayo pia bado yanatuonyesha kuwa Pasaka ni mnyama ambaye Mungu aliwaamuru wana wa Israeli (peke yao) wamchinje kisha wamle.

Siku na muda aliouweka Mungu wa kuchinja na kumla Pasaka
Pamoja na Mungu kuwatajia wana wa Israeli watu wanaoruhusiwa kumla Pasaka (kama tulivyoona katika maandiko yaliyotangulia), Mungu pia aliwapangia siku na muda maalum wa kuchinja na kumla Pasaka, kama maandiko yafuatayo yanavyoeleza:

"Kisha BWANA akanena na Musa katika bara la Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri, akamwambia, Tena wana wa Israeli na washike sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. Siku ya kumi na nne kwa mwezi huu, wakati wa jioni, mtaishika kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoishika. Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waishike sikukuu ya Pasaka. Nao wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai, vile vile kama haya yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli".
(Hesabu 9:1-5)
"Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni Pasaka ya BWANA".
(Hesabu 28:16)
"Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA". (Mambo ya Walawi 23:5)

"Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo na mbuzi. Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchnija jioni". (Kutoka 12:5-6) Kulingana na maandiko hayo juu, tunaona kwamba siku ya Pasaka ambayo Mungu aliwapangia wana wa Israeli kuishika ilikuwa ni kila ifikapo tarehe 14 mwezi wa kwanza wa mwaka wa kutoka kwao nchini Misri. Aidha, kama maandiko mengine ya Biblia yanavyofundisha (tazama Kumbukumbu la Torati 16:1) mwezi huo uliitwa "Mwezi wa Abibu" ambao ulianza kuhesabiwa kabla hata Nabii Issa au Yesu (a.s.) hajazaliwa (B.C.). Ni wazi kuwa shuhuda hiyo peke yake inadhihirisha kuwa Pasaka kuwekwa tarehe 2 mwezi wa nne wa mwaka wa kuzaliwa Yesu (A.D.) kama wanavyofanya Wakristo leo, kwa kweli hiyo si katika mafundisho sahihi ya Mungu, bali ni uzushi mtupu uliobuniwa na wanaadamu!

Lengo sahihi la Mungu kuweka sikukuu ya Pasaka
Sambamba na Mungu kuwawekea wana wa Israeli utaratibu maalum wa jinsi ya kutekeleza amri yake ya kuchinja na kumla Pasaka, vile vile Mungu hakuacha kubainisha lengo hasa la kutoa amri hiyo kwa wana wa Israeli, kama maandiko yafuatayo yanavyobainisha hapa chini:

"Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako, Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake. Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku zote za maisha yako". (Kumbukumbu la Torati 16:1-3).

Kufuatana na maandiko hayo juu, tunaona kuwa lengo la Mungu kuwawekea wana wa Israeli sikukuu hiyo ya Pasaka, ilikuwa ni kwa ajili ya kukumbuka siku aliyowakomboa kuwatoa nchini Misri chini ya utawala ya Farao (Firauni). Ambapo maandiko ya Biblia yamearifu kuwa wana wa Israeli walikaa nchini Misri katika hali ya utumwa kwa muda usiopungua miaka 430 (tazama Kutoka 12:40-42)).
Aidha, maandiko hayo yanaonyesha lengo lingine la Mungu kuwawekea wana wa Israeli sikukuu hiyo (Pasaka) ilikuwa kama desturi yake kujenga uhusiano mzuri baina yake na wanaadamu endapo watatii amri zake.

Dhana ya kufa na kufufuka kwa Yesu si mafundisho ya Mungu
Kwa kweli, zaidi ya masimulizi ya Wainjilisti na wanaadamu wengine kwa ujumla, hakuna kamwe mafundisho sahihi ya Mungu yanayothibitisha kufa na kufufuka kwa Nabii Isa au Yesu (a.s.). Kinyume chake, tunaona maandiko mengi ya Mungu yanashutumu vikali tendo zima la mtu kusulubiwa kwa kutundikwa mtini, kama lile linalodhaniwa kufanyika kwa Bwana Yes (a.s.)
Na ndio maana sambamba na kutoa amri ya Pasaka kabla ya kuzaliwa Yesu, tendo hilo (la mtu kutundikwa) mapema Mungu alilishutumu vikali kwa kusema:

"...kwa aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu..."
(Kumbukumbu la Torati 21:22-23).

Aidha, kabla ya shutuma hiyo (ya Mungu) dhidi ya mtu aliyetundikwa (aliyesulubiwa), Mungu alieleza bayana wasifu wa laana kwa mtu, kwa kusema:

"Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizapo leo; na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine".
(Kumb. 11:26-28)

Kuhusu laana, Mungu pia hakuacha kuelekeza mahali ambako laana yake hupatikana kama tunavyosoma maandiko yafuatayo:
"Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki". (Mithali 3:33).

Kwa shuhuda hizo, tunachojifunza hapa ni kwamba yeyote aliyetundikwa (aliyesulubiwa) basi anahesabika kuwa amelaaniwa, asiyesikiza maagizo ya Mungu na kukengeuka njia yake, mshirikina (anayemuabudu Mungu pamoja na miungu mingine) na kwa ujumla mtu huyo ni mwovu. (rejea Mithali 3:33).

Zaidi ya hivyo, kwa maandiko hayo, yaonyesha wazi Mungu hafurahishwi na kwa ujumla hapendi tendo la mtu kusulubiwa. Kwa mantiki hiyo, ni dhahiri kuwa dhana ya kusulubiwa Yesu ingelikuwa sahihi iwapo tu Mungu asingelishutumu tendo la mtu "kusulubiwa" kwa kiwango hicho, hasa unapolinganisha shutuma hizo (za Mungu) na hadhi, utukufu na ucha Mungu kwa ujumla wa Bwana Yesu (a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu. Isitoshe, Mungu asingeacha kueleza tukio zito na 'muhimu' kama hilo kwa ufasaha, kwa uwazi na kwa maelezo ya kukinaisha.
Aidha, dhana hiyo ya kusulubiwa Yesu pia ingelikuwa ni sahihi na tendo la wokovu, iwapo tu Yuda Iskariote angeliitwa "Mwokozi wa kwanza" kwa 'kuharakisha' wokovu wa walimwengu, kinyume na anavyoitwa mpaka sasa kwamba ni "msaliti" aliyemsaliti Yesu! (tazama Mathayo 26:25). Kwani inasimuliwa kuwa ndiye aliyewaonyesha maadui wamuue Yesu baada ya kuahidiwa fedha (tazama Mathayo 26:14-15). Ni ajabu watu wa timu moja wamshutumu mtoa pasi kwa mchezaji aliyeifungia goli timu yao!
Vile vile dhana hiyo (ya kusulubiwa Yesu) ingekuwa sahihi na tendo la "ukombozi" wa wanaadamu, iwapo tu Yesu asingemkemea mapema yule atakayemsaliti kwa kumwambia:
"...Lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa". (Mathayo 26:24)

Kinyume na andiko hilo juu, dhana ya kusulubiwa Yesu ingekuwa sahihi na nzuri iwapo Yesu angelimpongeza yule atakayemsaliti, kwa kumwambia:
"Lakini pongezi zake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Imekuwa heri kwake mtu yule amezaliwa".
Na kubwa zaidi, masimulizi ya Mwinjilisti Mathayo ya kudai kuwa eti Yesu alipokuwa msalabani alisema: "... Eloi, Eloi, lamasabakhtani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" (Tazama Mathayo 27:46) yanapingwa vikali na mwenyewe Bwana Yesu (a.s.) kwa kusema:
"Naye aliyenipeleka yu pamoja nami; hakuniacha peke yangu, kwa sababu nafanya siku zote yale yampendezayo". (Mathayo 8:29).

Kwa kauli hiyo peke yake ya Yesu inadhihirisha wazi kuwa yule aliyekuwa akilalamika kuachwa na Mungu hapo msalabani hakuwa Yesu. Yesu hawezi kuachwa na Mungu kwa sababu kama mwenyewe anavyoeleza katika andiko hilo hapo juu kwamba siku zote hufanya yanayompendeza Mungu.
Na kwa ujumla ukombozi wa wanaadamu kamwe haupatikani kwa njia ya laana (kusulubiwa) ambayo i katika nyumba ya waovu. (Mithali 3:33).

MISALABA
Wakristo wengi hafahamu kuwa, alama za kwanza kabisa za ukristo zilikuwa ni alama ya samaki kwa kumaanisha ndie kristo. On sacramental cups, seals, and lamps na roho mtakatifu akapewa alama ya njiwa (huwa - dove) (perhaps because at the time, fish was one of the elements of the sacred meal), au kwa alama ya mchungaji aliyebeba kondoo mabegani. (Luke 15:3-7) na si misalaba kama tuonavyo ivi leo. Misalaba ilikuja kupatikana miaka michache baada ya kuondoka Nabii Yesu. Na hii ni baada ya kuasisiwa na bwana Paulo. Kwa kusema laana ya kusurubiwa kwa Yesu ndo ilotukomboa kutoka kwenye dhambi. (Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya Sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: "Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa (Galatians 3:13).

Historia inatufahamisha kuwa, alama za kutumia misalaba zilikuwa ni alama za dini za kale za kipagani. Miaka mingi kabla ya kuja Nabii Yesu. Mfano mmoja wapo ni kule India, wao walitumia misalaba kwa kumnasibisha na mungu wao mpendwa aitwae Agni (" Agni light of the world."), na msalaba huu ulikuwa unawekwa mikononi mwa miungu hii ifuatayo, Siva (Śiva tamka ‘Shiva), Brahma, Vishnu, Krishna, Tvashtri, na Jama.

Misalaba haitumiwi na wahindu tu, hata hii dini ya kibudha, huitumia kama miongono mwa alama zao za kidini. Na haswa wafuasi wa Lama of Thibet. Wamiisri wa kale (The ancient Egyptians) walitumia misalaba kwenye dini zao za kipagani. Alama nyingi nyingi zilizo ifadhiwa kule Misri zinaonyesha miungu yao wakiwa wamekamata misalaba mikononi. Mmoja wa miungu hiyo ni huyu aitwae “Mkombozi Horus” (the Egyptian savior Horus). Vile vile uonyeshwa kwenye michoro na masanamu yao ya mtoto aliye pakatwa na mama yake na huku amekamata msalaba. Mslaba ulokuwa maalufu ukitumika sana kipindi hicho cha dini za kipagani huko misri ulijulikana kwa jina la the CRUX ANSATA. Msalaba huu baadae ulirithiwa na wakristo. Vile vile mkombozi Osiris (OSIRIS.)mungu wa wa Kimisri, ajulikanae kama mungu wa mauti na wafu walioko kuzimu, naye pia huchorwa akiwa amekamata, au kushika msalaba, huku akimuonyesha mtu kwa kumaanisha kuwa binadamu huyo siku zake za kuisho zimekwisha na anatakiwa kuzimu. Misalaba mingine ilifukuliwa kule Ireland. Misalaba iliyokuwa ikiabudiwa na Wairani wa zamani. Ikimuwakilisha Mithra (angalia Mithraism) akiwa na Dubu. (god of the sun). Wagiriki na Warumi wa kale nao waliitumia misalaba kwenye dini yao karne nyingi kabla ya kuja ukristo. Misalaba mingi ya dini za kale unaweza kuipata kwenye mapango ya mfalme Midas kule Phrygia. (the tomb of king Midas in Phrygia)The great luminary of the Church, Saint Augustine (354-430 C.E.), amenukuliwa akisema:"The same thing which is now called CHRISTIAN RELIGION existed among the ancients. They have begun to call Christian the true religion which existed before."Bwana James Bonwick alisema maneno haya;"Our love for what is old, our reverence for what our fathers used, makes us keep still in the church, and on the very altar cloths, symbols which would excite the smile of an Oriental, and lead him to wonder why we send missionaries to his land, while cherishing his faith in ours". Na ndio sababu, kutokana na uzito wa shutuma za Mungu dhidi ya mtu anayesulubiwa (kama tulivyoona hapo awali), Mwenyezi Mungu katika Qur'an Tukufu akaeleza wazi kwamba:

"Hawakumwua wala hawakumsulubu."
(Qur. 4:158).

Kwa maandiko haya na mengine mengi niliyo kwisha yaeleza kabla ni dhahiri kuwa dhana ya kufa na kufufuka Yesu katu haimo katika mafundisho ya Mungu. Na kwa mantiki hiyo, Pasaka iliyofundishwa na Mungu haina uhusiano wowote na dhana ya kufa na kufufuka kwa Yesu hasa ukizingatia kuwa Pasaka hiyo (ya Mungu) imekuwepo kabla ya Yesu kuzaliwa, na pia kufa na kufufuka kwa Yesu ni jambo lililozuliwa na wanaadamu baada ya Yesu kuondoka kama tutakavyokuja kuona hapo baadae, Insha’Allah.

Yesu mwenyewe aliwahi kumla Pasaka
Ili kuonyesha zaidi kwamba Pasaka haina uhusiano wowote na dhana potofu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, maandiko ya Biblia yanaeleza wazi kuwa Bwana Yesu naye kabla ya kuondoka aliwahi kumla Pasaka. Maandiko yafuatayo yanathibitisha ukweli huu.

"Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile Pasaka? Akatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji; mfuateni; na popote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, ki wapi chumba cha wageni, niile Pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu? Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni. Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka. Basi ilipokuwa jioni yuaja na wale Thenashara, wakila, Yesu alisema, Amin, naawaambieni, mmoja wenu, naye anakula pamoja nami atanisaliti".
(Marko 14:12-18)

Kufuatana na maandiko hayo juu, tunaona hapa kwamba Bwana Yesu aliwatuma wanafunzi wake wakaandaa mahali atakapomla pasaka na wala haielezwi kwamba aliwatuma wakaandaa mahali "yeye atakapokufa kwa pasaka". Aidha, haielezwi kwamba wanafunzi wake walipochinja, walimchinja Yesu kuwa Pasaka. Lakini tunaona kuwa baada ya kupatikana hicho chumba na maandalizi kwa ujumla kukamilika, naye Yesu pia alimla Pasaka. Hii yote ni kudhihirisha kuwa Pasaka ni mnyama anayechinjwa na kuliwa na siyo binadamu. Na kwamba Pasaka ilifanyika mwenyewe akiwa hai na wala hajafundisha kwamba Pasaka ni kufa na kufufuka kwake.

Mapinduzi ya Paulo dhidi ya Pasaka aliyefundishwa na Mungu!
Pamoja na Mungu kufundisha wazi kwamba Pasaka ni mnyama (kondoo, ng'ombe au mbuzi) anayetakiwa achinjwe na kuliwa kwa utaratibu na kwa lengo maalum kama tulivyoona hapo awali, lakini Paulo hakukubaliana kabisa na mafundisho hayo ya Mungu. Yeye alikuja na mafundisho mapya kabisa. Tofauti na Pasaka yule aliyefundishwa na Mungu, Paulo alikuja na Pasaka wake, kama mwenyewe anavyosema hapa chini:
"Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani Kristo".
(1 Wakorintho 5:7)

Kulingana na maelezo yake hayo juu, mbali na kuwataka watu waache kufuata anavyokiri kuwa ni kuishika sheria za Torati (angalia Wagalatia 3:10-13 na Warumi 7:14), katika juhudi zake hizo za kupindua mafundisho ya Mungu, Bwana Paulo amejaribu kumgeuza Yesu kuwa ndiye Pasaka badala ya mnyama (kondoo, ng'ombe au mbuzi) aliyefundishwa na Mungu, na Yesu mwenyewe kabla hajaondoka!
Kwa shuhuda hiyo, ni dhahiri kuwa Bwana Paulo ndiye muasisi mkuu wa dhana ya kuchinjwa (kusulubiwa), kufa na kufufuka kwa Yesu. Vinginevyo asingethubutu kumwita Yesu kuwa ni "Pasaka" kwani hilo siyo fundisho la Mungu.

Azma ya Paulo dhidi ya mafundisho ya Mungu tangu awali
Hapo juu tumeona jinsi Bwana Paulo alivyogeuza Pasaka wa kweli aliyefundishwa na Mungu. Pamoja na mapinduzi yake hayo, Bwana Paulo tangu awali hakuficha azma yake juu ya Bwana Yesu. Mara tu alipofika hakuhofu kuutangazia wazi umma kwa kusema:
"Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulubiwa". (1 Wakorintho 2:1-2).
Kwa maelezo yake hayo, kikubwa alichoazimia Paulo kukieneza kwa watu si kingine isipokuwa "kusulubiwa tu kwa Yesu"! Ambapo msingi wa kusimamisha dhana yake hiyo aliona aanze kumwita Yesu kuwa ni pasaka. Dhamira yake ikiwa ni kupotosha mafundisho sahihi ya Mungu kuhusu pasaka apate kumchinja Yesu kinadharia ili dhana yake (ya Yesu kusulubiwa) isimame!

Hitimisho
Kama tulivyoona shuhuda nyingi za maandiko ya Biblia, jambo la kusisitiza hapa ni kwamba, sikukuu ya Pasaka iliwekwa na Mungu kwa ajili ya kumbukumbu ya kukombolewa wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri (tazama Kumbukumbu la Torati 16:3); na siyo kufa na kufufuka kwa Yesu kama inavyodaiwa na Wakristo. Aidha, tumeona kuwa dhana ya kufa na kufufuka kwa Yesu haimo kabisa katika mafundisho ya Mungu, bali ni katika mafundisho ya Paulo ambayo mara nyingi amekuwa akieleza wazi kuwa mafundisho yake ni ya kibinadamu (tazama Wagalatia 5:15)
Aidha, dhamiri ya Bwana Paulo kuibua mafundisho yake hayo kama tulivyoona ilikuwa ni kufanya mapinduzi dhidi ya mafundisho ya Mungu.
Kwa mantiki hiyo basi, ni wazi kuwa imani hiyo (ya msalaba) haitomsaidia kitu mwanadamu hasa kwa kuwa lengo lake ni kutaka watu waache kufuata amri na sheria za Mungu (kama atakavyo Bwana Paulo), badala yake wategemee damu bandia ya Yesu!
Umefika wakati wa wanaadamu kujiepusha na imani potofu (kama hizo za kusulubiwa Yesu) na badala yake waanze mara moja kufuata maamrisho ya Mungu kwani hata Yesu mwenyewe alipoulizwa na mtu mkubwa mmoja "nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?" Yesu hakumwambia "nitakaposulubiwa na kufa ndiko kutakakofanya upate uzima wa milele", hapana! Lakini Yesu alimwambia hivi:
"...wazijua amri; usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo... Viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate".
(Luka 18:18-22)

"Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake."
Al -An'am 6.93

0 comments/Maoni: