Yesu Ndani Ya Qur’an Wakristo Hawalijuwi Hili

Mkristo hajuwi kuwa ile imani ya dhati ya wema ambayo Muislamu anaionesha kwa Yesu na mama yake inatokana na msingi mkuu wa imani yake Qur’an Tukufu. Mkristo hajuwi kuwa Muislamu halitaji jina la Yesu (Isa) bila kuongeza duwa ya amani juu yake-kwa Kiarabu, Isa alai-hiss-salaam- Kwa Kiingereza-Jesus, peace be upon him (Kwa Kiswahili-Yesu/Isa, amani iwe juu yake).
Kila mara Muislamu anapolitaja jina Isa bila maneno haya ya kumtakiya amani, basi huonekana mtovu wa Adabu (Akhlaq). Mkristo hajuwi kuwa katika Qur’an Tukufu Yesu (as) anatajwa kwa jina mara nyingi zaidi kuliko jina (Muhammad saw). (utajo wa jina Isa ndani ya Qur’an unauzidi mara tano (5x) utajo wa jina Muhammad) Kwa idadi halisi-Yesu anatajwa mara ishini na tano wakati Muhammad anatajwa mara tano. Kwa mfano:

"....na Tukampa ISA, mwana wa Mariyamu ( Yesu mtoto wa Maria) hoja zilizo wazi wazi, na Tukamtia nguvu kwa Roho mtakatifu'' .
(Qur’an 2:87)

".....Ewe Mariyamu! Mwenyezi Mungu anakupa khabari njemaza neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi, ISA mwana wa Maryamu..."
Qur’an (3:45)

..Masihi ISA bin Maryamu ni Mtume wa MwenyeziMungu....
(Qur’an 4:171).

Na Tukawafuwatishia (Mitume hao) ISA bin Maryamu...”
(Qur’an 5:46).

“Na Zakaria na Yahya na ISA na Ilyas, Wote (walikuawa) ni miongoni mwa watu wema.
(Qur'an 6:85).

YESU NA MAJINA YAKE:
Ingawaje Yesu anatajwa kwa jina mara ishirini ndani ya Qur’an Tukufu, piya kiheshima anaitwa “Ibni Maryam” (Mwana wa Maryam); Masihi (Messiah kwa Kiebrania) ambalo hutafsiriwa kama Kristo “Abd-ullah”- mja wa Allah; “Rasul-ullah”-Mtume wa Allah.Anaelezewa kama “neno la Mungu” , “kama Roho wa Mungu”“ishara ya Mungu”, na sifa nyingine kemkem za utukuzo zilizotolewa katika zaidi ya sura kumi na tano. Qur’an inampa heshima Mtume huyu mkubwa wa Mungu, na Waislamu hawajafanya kinyume na hivyo kwa miyaka elfu moja na miya nne.

Hakuna hata neno moja la dharau katika Qur’an yote ambalo wale Wakristo wenye hiyana zaidi wanaweza kulitafutiya dosari.

1 comments/Maoni:

RGM 24HRS said...

Amina sana ndugu, Mungu akubariki kwa somo zuri