HUKUMU YA PILATO WA UYAHUDI

(Zingatia vifupisho hivi: HKM=Hakimu, PLT=Pilato, MSM= Msoma Mashtaka).
Itapendeza zaidi ukiwa na biblia karibu

Ni asubuhi mida ya saa tatu na nusu katika mahakama kuu ya rufaa ya ulimwengu mzima. Mahakama imejaa watu wa mataifa mbali mbali, kwani hii ni kesi ya karne. Mshtakiwa ni bwana Pilato wa kipindi cha Bwana Yesu. Akishtakiwa kwa kushukiwa kuwa amesababisha mateso na kifo cha msalabani kwa Masii Yesu wa Nazareth .
Mashahidi wote wanne wapo mbele ya mahakama, wamesimama kwenye kizimba cha mahakama hii tukufu na takatifu kabisa kwa nidhamu ya hali ya juu sana. Mashahidi hawa inasemekana aidha ni miongoni mwa wanafunzi wake (?) au waliwezweshwa kuandika ushahidi wao kwa uwezo wa roho mtakatifu (!?), ambaye ni nafsi ya pili ya Mungu mkuu na kuita Injili, ktk ule utatu mtakatifu. Mshtakiwa Bwana Pilato naye yupo upande wa pili akitazamana na mashahidi wa upande wa mashtaka.

Cooooooourt! Sauti kubwa ya msimamizi wa mahakama ikasikika, na watu wote waliokuja kusikiliza kesi hii ya karne wakasimama, hili kumpa heshima hakimu.
Baada ya hakimu kukaa na kuwaamuru watu wote wakae. Bwana Hakimu akamwamrisha MSM asome shtaka lililo mbele yao.

MSM: Kesi nambari Y/2000/P/00 Dhidi ya bwana Pilato wa Uyahudu samahani bwana hakimu ni uyahudi, Bwana Pilato anashtakiwa kwa kusababisha maumivu na kifo cha mateso kwa bwana Yeheshua wa Nazareth (a.k.a Yesu kiristo, Jesus Christ au Yesus kristo,au Emmanuel) mtoto wa Mariam. Kitendo kilicho fanyika miaka 2000 hiyooo ilopita saa na wakati usio jurikana. Bwana Yeheshua aliye zaliwa bethlehemu ya uyahudi zama za mfalme Herode (Matt 2:1)
Bwana Yeheshua ambaye alikuwa fundi seremala stadi sana kwa kipindi kile, (Mark 6:3) ambaye alirithi ufundi huo kutoka kwa babaye mlezi (Matt 13:55). Kijana huyo ambaye inasemakna alikuwa akipenda kupanda punda na ndio ulikuwa usafiri wake maarufu (Matt, 21:5) na (John, 12:14), alikuwa akipenda kula na kunywa na wenye dhambi (Matt, 11:9; Luk, 7:34). Ni mtu ambaye hakuwa na anuani maalum kwa maana ya makazi na wala hakupenda kuzika watu (Matt 8:20 & 8:22). Ni mtu aliye kuwa maarufu sana kwa kipindi chake.
Bwana hakimu hayo ndio mashtaka yanayo mkabili bwana Pilato dhidi ya mtu wa mungu baba aliye juu. Mtu ambaye kwa kipindi chake aliitwa Nabii (Yoh 6.14).

Baada ya kusomewa mashtaka bwana hakimu akamuuliza mshtakiwa kwa sauti nzito na kakamavu huku amemkazia macho…

HKM: Mshtakiwa unakubali kosa au hunakana kosa?

Pilato: Ninakana kosa mheshimiwa hakimu. (Kwa unyenyekevu)

HKM: (Akimgeukia MSM) Je unao mashahidi wowote walio shuhudia haya yote, uliyoyaleta hapa mbele ya mahamani hii tukufu na takatifu?

MSM: Ndio bwana hakimu ninao na wapo humu ndani ya mahakama yako tukufu na takatifu. Kwa rukhsa yako naomba niwalete mbele yako…

HKM: Sawa walete na waanze kutoa ushahidi wao.

MSM: Mashahidi hao ni:
Shahidi wa kwanza: bwana Matthayo,
Shahidi wa pili bwana Marko,
Shahidi wa tatu bwana Luka,
Shahidi wa nne bwana Yohana.

Baada ya mashahidi wote kuapishwa na kujazwa roho mtakatifu hakimu alianza kwa kuwauliza maswali mashahidi wale wanne…

HKM: Je mashahidi mmeshuhudia nini ktk kadhia nzito iliyowagawa watu ulimwenguni, kadhia hii ya Bwana huyu Yeheshua? Na mnamjua vipi mtu huyu aliyependa kujiita mwana Adam?

Matthayo: Bwana hakimu (Matthayo akaanza) kwanza kabisa mie namfahamu Bw. Yesu vizuri sana, yeye ni kizazi cha 28 toka Daudi mpaka Joseph. (Matt 1:6-16).
1. David, 2.Solomon, 3.Rehobo'am, 4.Abi'jah 5.Asa, 6.Jehosh’aphat, 7.Joram, 8.Uzzi’ah, 9.Jotham, 10.Ahaz, 11. Hezeki'ah, 12.Manas'seh, 13.Amos, 14.Josi'ah, 15.Jechoni'ah, 16.She-AI’ti-el, 17.Zerub’babel, 18.Abi’ud, 19. Eli’akim, 20.Azor, 21.Zadok, 22.Achim, 23.Eli'ud, 24.Elea’zar, 25.Matthan, 26.Jacob, 27.Joseph, 28.Jesus (From RSV English 1952)
1. David, 2.Solomon, 3.Roboam, 4.Abia 5.Asa, 6.Josephat, 7.Joram, 8.Uzias, 9.Joatham, 10.Achaz, 11. Ezekias, 12.Manasses, 13.Amon, 14.Josias, 15.Jechonias, 16.SaIathiel, 17.Zorobabel, 18.Abiud, 19. Eliakim, 20.Azor, 21.Zadoc, 22.Achim, 23.Eliud, 24.Eleazar, 25.Matthan, 26.Jacob, 27.Joseph, 28.Jesus. (From KJV, English 1611)

1. Daudi, 2.Suleman, 3.Rehoboam, 4.Abiya 5.Asa, 6.Yehoshophati, 7.Yoramu, 8.Uzia, 9.Yotham, 10.Ahazi, 11. Hezekia, 12.Manase, 13.Amoni, 14.Yosia, 15.Yekonia, 16.SheaItieli, 17.Zerubabeli, 18.Abihudi, 19. Eliakimu, 20.Azori, 21.Sadoki, 22.Akimu, 23.Eliudi, 24.Eleazari, 25.Matani, 26.Yakobo, 27.Yusufu, 28.Yesu
(From holy bible in Kiswahili Union Version. 1952)
Na ninakumbuka ilikuwa pale kwenye mlima wa Gethsemane (Matt 26:36), alikuja Yuda na watu wenye mapanga na marungu, na Yuda akaja kumbusu bwana Yeheshua ikiwa ni ishara ya kuwa ni yeye anayetafutwa. (Matt 26:49) na tulitaka kujitetea kwa mapanga yetu mawili tuliokuwa nayo. Mmoja wetu simkumbuki kwa jina alimkata askari mmoja sikio, lakini bwana wetu akaogopa kwa sababu askari walikuwa wengi. Akalirudisha sikio lililo katwa sehemu yake. (Matt 26:51).

HKM: Bwana wenu aliwaagiza muwe na mapanga au sio?

Matthayo: Hapana sikumbuki kuagizwa hilo mheshimiwa hakimu.

HKM: Luka wewe unamfahamu vipi binadam huyu aitwaye Yeheshua?

Luka: yeye ni kizazi cha 43 toka Daudi mpaka Joseph

HKM: kizazi cha 43…?!!

Luka: ndio Muheshimiwa Hakimu ni kizazi cha 43 na si cha 28 kama alivyo eleza Matthayo.
Luke. 3:23-31
1. David, 2. Nathan, 3. Mat’tatha, 4. Menna, 5. Me’Ie-a, 6. Eli’akim, 7. Jonam, 8. Joseph, 9. Juda, 10. Simeon, 11. Levi, 12. Matthat, 13. Jorim, 14. Eliezer, 15. Joshua, 16. Er, 17. Elma’dam, 18. Cosam, 19. Addi, 20. Melchi, 21. Neri, 22. Sheal’ti-eI, 23. Zerub'babel, 24. Rhesa, 25. Jo-an’an, 26. Joda, 27. Josech, 28. Sem’e-in, 29. Matathi’as, 30. Ma'ath 31. Nag’ga-I, 32. Esli, 33. Nahurn, 34. Amos, 35. Mattathi'as, 36. Joseph, 37. Jan'na-I, 38. Melchi, 39. Levi, 40. Matthat, 41. Heli, 42. Joseph, 43. Jesus. (From RSV English 1952)
1. David, 2. Nathan, 3. Mattatha, 4. Menan, 5. MeIea, 6. Eliakim7. Jonam, 8. Joseph, 9. Juda, 10. Simeon, 11. Levi, 12. Matthat, 13. Jorim, 14. Eliezer, 15. Jose, 16. Er, 17. Elmodam, 18. Cosam, 19. Addi, 20. Melchi, 21. Neri, 22. SalathieI, 23. Zorobabel, 24. Rhesa, 25. Joanna, 26. Juda, 27. Joseph, 28. Semei, 29. Matathias, 30. Maath 31. Nagge, 32. Esli, 33. Naurn, 34. Amos, 35. Mattathias, 36. Joseph, 37. Janna. I, 38. Melchi, 39. Levi, 40. Matthat, 41. Heli, 42. Joseph, 43. Jesus. (From KJV, English 1611)
1. Daudi, 2. Nathani, 3. Matatha, 4. Mena, 5. MeIea, 6. Eliakimu, 7. Yonamu, 8. Yusufu, 9. Yuda, 10. Simeoni, 11. Lawi, 12. Mathati, 13. Yorimu, 14. Eliezeri, 16. Er, 15. Yoshua, 16. Er I, 17. Elmadamu, 18. Kosamu, 19. Adi, 20. Melki, 21. Neri, 22. ShealtieIi, 23. Zerubabeli, 24. Resa, 25. Yoana, 26. Yuda, 27. Yusufu, 28. Semei, 29. Matathia, 30. Maathi 31. Nagai. I, 32. Esli, 33. Nahurnu, 34. Amosi, 35. Matathia, 36. Yusufu, 37. Yana. I, 38. Melki, 39. Lawi, 40. Mathati, 41. Eli, 42. Yusufu, 43. Yesu. (From holy bible in Kiswahili Union Version. 1952)
(Angalia mgongano wa majina)
Bwana hakimu, mie nakumbuka tulikuwa pale kwenye mlima wa mizeituni na wala thi mlimani Gethsemane kwani bwana wetu alituagiza tuwe nayo mapanga, hata kwa kuuza nguo zetu (Luk 22:36). Ila sikumbuki ni nani aliyemkata askari thikio.

Yohana: Bwana hakimu mie sitaki kusema uongo, sina uhakika kabisa na mambo ya ukoo wake. Ninacho kumbuka mie tulikuwa kwenye bustani, kando ya kijito Kedroni na wala si mlima wa mizeituni na wala si mlimani Gethsemane. Na ni Simon Petro ndio aliye kuwa na upanga na ndiye aliyemkata mtu sikio. Ila sikumbuki kuagizwa tuwe na mapanga, Na wala sikumbuki kwa Yuda kumbusu Bwana wetu, ila Yesu ndio aliye wauliza kama wanamtafuta yeye. Wakarudi nyuma na kudondoka (Yoh 18:4-6)

Marko: Mie pia nakumbuka hatukuwa mlimani bali kwenye bustani ya Gethsemane (Mark 14:32) na Yuda alimbusu bwana (Mark 14:45).

HKM: Ina maana wewe Matthayo, Luka, na Marko hamkumbuki chochote kudondoka kwa askari kabla ya kumkamata bwana Yeheshua?

Kwa pamoja isipokuwa Yohana: hapana bwana hakimu tendo hilo halikutokea.

HKM: Sasa nambieni jambo moja, bwana Yeheshuwa alikuwa kwenye bustani ya Gethsemane au mlima wa Gethsemane au alikuwa kwenye bustani ya Mizeituni au kando ya kijito Kedroni kwenye bustani isiyo julikana?

Wote: Kimyaaa!!

HKM: Haya endeleeni kutoa ushahidi wenu!

Matthayo: Mie kusema kweli saa na muda sikumbuki ila nakumbuka baada ya kumsurubisha askari waliweka anuani ya mashtaka yalioandikwa juu ya kichwa chake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI’ (Matt 27:37). Na kiza kilianza saa sita mpaka saa tisa. Na alipiga kelele na kusema : Eloi Eloi lama sabakhtani? Yaani; Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha? (Matt 27:46). Na pazia la hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini. (Matt 27:51). Na isitoshe makaburi ya watukufu yalifunguka na watakatifu wakatoka makaburini wakaingia mjini na wakawatokea watu (Matt 27:52-53).

HKM: Munguuu wanguuuu… basi ilikuwa kasheshe siku hiyo, bwana Matthayo. Ilikuwa *Halloween siku hiyo. Una uhakika na unayosema na watu kweli walifufuka toka makaburini mwao?!!
*
It is a religious holiday among some Christians.
Halloween had its origins in the festival of Samhain among the Celts of ancient Britain and Ireland. November 1 was considered the end of the summer period, the date on which the herds were returned from pasture and land tenures were renewed. It was also a time when the souls of those who had died were believed to return to visit their homes. People set bonfires on hilltops for relighting their hearth fires for the winter and to frighten away evil spirits, and they sometimes wore masks and other disguises to avoid being recognized by the ghosts thought to be present. It was in these ways that beings such as witches, hobgoblins, fairies, and demons came to be associated with the day. The period was also thought to be favourable for divination on matters such as marriage, health, and death. When the Romans conquered the Celts in the 1st century AD, they added their own festivals of Feralia, commemorating the passing of the dead, and of Pomona, the goddess of the harvest.

Matthayo: Ni kweli bwana hakimu, tena si watu wadogo, ni watu watakatifu na watu wengi waliwatokea siku hiyo, mie niliwaona kwa macho yangu.

HKM: Mmmmh… hayaaa… Bwana Marko wewe ushuhuda wako unasemaje?

Marko: Bwana hakimu nakumbuka mida ya saa tatu ndio walimsurubisha, na juu ya kichwa chake waliandika anuani hii: ‘MFALME WA WAYAHUDI’. (Mark 15:25-26). Ila sikumbuki ni nani aliye andika. Na kiza kilianza saa sita mpaka tisa. (Mark 15:33). Na maneno hayo ya kumwita Eloi kweli aliyasema. (Mark 15:34). Na pazia likapasuka baada ya kutoa sauti kuu (Mark15:38). Ila kuhusu kufufuka kwa watakatifuuuu…. Mmmmh… Bwana hakimu siwezi sema owongo ilo sikulishuhudia kwa kweli. Sijui bwana Matthayo labda atueleze mbona sie wote atukuliona?

Matthayo: Tatizo nyie hamkuwa na roho mtakatifu kipindi kile.

Wote kwa pamoja isipokuwa Matthayo: Tafadhali tuheshimiane roho mtakatifu hukuwa naye peke yako banaa sote tulikuwa nayee, banaa alaaa…
Matthayo: Hamkuwa nayee banaaaa mbona hamkuona kufufuka kwa watakatifuuu…Kwanza wewe Luka hata Yesu hukumuona umehadithiwa tu, alafu unajitia kujuwa hapa, mwone vileee…

Luka: Oooh.. Oooh… pole pole kaka mdomo utaponza kichwa huoo, Oooh!! Shauri yako, kwanza kwani hata kama nilihadithiwa lakini thi nilikuwa namuandikia Theofilo Mtukufu ili apate juwa mambo yaliotokea henzi ya Herode tena bathi… bathi… naliandika thi baada ya kuwa na roho mtakatifuuu. (Luk 1:1-4).
Na alafu uthitake tutoe thiri hapa. Kwanza wewe thi mwanafunzi wake na wala thi mtodha ushuru wa pale forothani. Mwenyewe alikuwa anitwa Lawi. (Luk 5:27).

Matthayo: nilikuwa mie banaa Mathayo mtoza ushuru (Matt 9:9)

HKM: Ooorder… order… Ooooooorderrrr… Heshimuni mahakama yangu tukufu na takatifu tafadhaliiii… (huku akipiga rungu lake lipatalo kilo ishirini hivii kwenye meza), buu… bu bu… bu bu…. Tunaendereaaa… shahidi nambarii tatu bwana Luka tafadhaliii...
Marko: (Huku akijisemea moyoni Yaani Mathayo hana hata haya jamaa alikuwa anitwa Lawi wa Alfayo, Mark 2:14)
Pilato anatabasamu kwa chaati huku akishika mdomo wake kuzuiya kicheko…

Luka: Mie ninacho kumbuka bwana hakimu, maandishi yaliyo andikwa juu ya kichwa chake ni kama ifuatavyo… ‘HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI’ (Luk 23:38). Ila thikumbuki nani aliye andika. Na Kidha kilianza thaa thita mpaka thaa kenda, yaani baada ya kuthurubiwa. (Luk 23:44). Na pazia la hekalu likapathuka kabla ya Yethu kulia. Baada ya pazia kupathuka ndio Yethu akalia kwa thauti kuu akithema: Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu ndipo alipo kufa. Na wala thi Eloi Eloi… (Luk 23:46). Na hakuna haliye shuhudia hilo la kufufuka kwa watakatifu kwa kweli…!!! Bwana hakimu kenda thi unajuwa kuwa ni tithaa…!

HKM: Sawa tunaelewa kuwa KENDA ni TISA . Yohanaaa...!!! na wewe unasemaje kuhusu hili…

Yohana: Eeeh bwana hakimu mie nakumbuka mpaka mida ya saa sita bwana Yeheshua alikuwa kwa Pilato ajasurubiwa bado (Yoh 19:14), na kuhusu maandishi ninayo yakumbuka mimi ni: YESU MNAZARETI MFALME WA WAYAHUDI mwandishi ni Pilato (Yoh 19:19). Na walimpa siki baada ya kuona kiu na alipokwisha kuinywa neno lake la mwisho lilikuwa ili: ‘IMEKWISHA’ sikusikia neno lolote zaidi ya hili bwana hakimu.

HKM: Okey Yohana Asante, (Huku akiandika maelezo Fulani kwenye kitabu chake), na je kuna mtu yeyote aliyemsaidia kubeba msalaba?

Matthayo: Ndio kuna mtu mkirene anaitwa Simoni walimshurutisha kubeba msalaba wa bwana na walipo fika Golgotha walimpa divai ila hii divai mmmh nahisi alipewa mkirene, na ilichanganywa na nyongo na alipo iyonja hakuinywa (Matt 27:32).

HKM: Marko wewe unasemaje?

Marko: Ndio bwana Hakimu… walimshurutisha mtu mmoja alikuwa akitoka mashamba, Simoni Mkirene baba yao Iskanda na Rufo. Ili auchukuwe msalaba wake, walipo fika Golgotha walimpa mvinyo na wala si divai (Mark 15:21)

HKM: Mvinyo ndio divai kijana… endeleaa…

Marko: Sawa bwana hakimu ila mie nakumbuka ni mvinyo na si divai

HKM: Luka wewe unasemaje?

Luka: Aliyebeba mthalaba ni mkirene aitwae Thimoni (Luk 23:26). Ila thikumbuki kupewa divai wala togwa lolote lile. Mmmh yaah… nishakumbuka bwana hakimu alipewa thiki na si divai wala mvinyo (Luk 23:36).

HKM: Yohana unasema naona unatingisha kichwa…!

Yohana: Bwana hakimu kusema kweli bwana Yesu alibeba msalaba wake mwenye, hakuna mtu alimsaidia. Si Simoni wala mkirene yeyote aliye beba msalaba wa Yesu. (Yoh 19:17). Nakumbuka Yesu alisikia kiu ndo wakampa siki na akainywa (Yoh 19:29-30).

Petro huku akimnong’oneza Mgalatia mmoja ktk watu walio kuja kuhudhuria kesi hii.

Petro: Unajuwa kuwa Yesu walimtundika kwenye mti. (1petr 2:24)

Mgalatia: Niii-nnni-ni-ni… uuwa-aachaa uuoongo, mmimi kkwa kwa k-k-kkweli naa-na-kumbuk-aaaa sss-sana si ka-ka-aa-laniwa (Gal 3:13) na aaah-lafu mmmi- mi nakuumbuka kkkama hhhhhaaa-hakusurubiwa vile (Gal 3:1).

HKM: Shhhiii..!!! kimyaaa pale. Matthayooo tuambie ilikuwaje kwa Yuda Eskariote…

Matthayo: Kusema ukweli Yuda alijinyonga baadae (27:5).

Therofilo: (Akijisemea moyoni)… Mmmh mi najuwa kuwa Yuda alianguka kwa kasi akapasuka matumbo yote yakatoka. Na watu wote wakaao Yerusalemu wanajuwa hilo na wala hakujinyonga. (Mdo 1:18-19).

HKM: Na nyie wengine mnasemaje…?

Kwa pamoja: Hatuna huhakika na hilo bwana hakimu.

HKM: Sawaa... mmh kuna lingine la ziada. Matthayo!

Matthayo: Bwana hakimu Mariamu Magnalene na Mariamu yule wa pili walikwenda kaburini kwa bwana, na malaika toka mbinguni alikuja kuliviringisha lile jiwe la kaburi, huku wakishuhudi na tetemeko kubwa lililotokea… (28:1-5). Wanawake walikuwa wawili tu na malaika alikuwa mmoja baaasi…!

HKM: Marko unasemaje ushahidi wako kuhusu hili…?

Marko: Bwana hakimu, wanawake walikuwa watatu tu. Yaani Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo na Salome, lakini hawakushuhudia kuviringishwa kwa jiwe lile, walilikuta kaburi li wazi. Na kulikuwa hakuna tetemeko lolote la nchi. Ila walimkuta kijana mmoja kaka kwenye jiwe (Mark 16:3-4).

Luka: Bwana hakimu waliokwenda makaburini ni zaidi ya watu watatu na thi wawili.

HKM: Eeeh.. nani na nani bwana Luka…?!

Luka: Ni Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, Yohana na wale wanawake wengine waliokuja nao, ila thiwakumbuki majina yao (luk 24:10). Kusema ukweli waliwakuta watu wawili wamesimama mbele yao na thi malaika mmoja, ni watu wawili bwana hakimu (Luk 24:4)

HKM: Yohana unasemaje kuhusu hili…

Yohane: Bwana hakimu aliye kwenda makaburini ni mmoja tu naye ni Mariamu Magdalene na hakukuta mtu pale makaburini (Yoh 20:1). Ila baada ya kuja Petro pamoja na yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu ndipo malaika wawili wakamtokea Mariamu Magdalene (Yoh 20:12) na baadae Yesu mwenyewe akamtokea Mariamu Magdalene hakiwa amevaa mavazi ya mtunza bustani naye asimjue. (Yoh 20:14)

Hakimu: Je kuna la ziada kabla sijasoma hukumu inayomkabiri bwana Pilatoo…?

MSM: Hakuna la ziada bwana Hakimu.

Hukumu.
Bwana hakimu huku akirekebisha miwani yake vizuri na kukohowa kidogo hili kurekebisha koho
lake, anawaangalia, wale mashahidi vizuri na kuanza kusoma maelezo ya kesi nzima kama ifuatavyo.

HKM: Ndugu mleta mashtaka pamoja na mashahidi ulowaleta hapa, wasikilizaji wa kesi hii mabibi na mbwana, kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka kuleta ushahidi wao mbele ya mahakama hii tukufu na takatifu. Baada ya kupitia vipengele vyote vilivyoletwa hapa, kwa kweli kuna kujichanganya kwa ushahidi wote. Nikianza na ushahidi huu wa mwisho tumeona kuwa …

*Mwanamke mmoja kaona malaika wawili kaburini (Yoh20: 12), au…
*Wanawake wawili wameona malaika wawili (Matt 28:2), au…
*Zaidi ya wanawake watatu wameona mtu mmoja? (Luk24: 4), au…
*Wnawake watatu wamemuona kijana mmoja kaburini? (Mark16:5)
Ushahidi wenu hauna ushirikiano hata kidogo. Napata wasi wasi kama kweli wote nyie mlicho vieleza ni vitu amabavyo mmevishuhudia kwa macho yenu, au hata kuhadithiwa na watu walioshuhudia kwa macho. Na hii inanipa wasi wasi kama kweli huyu mtu alisurubiwa kweli. What a paradoxical piece of no-logic!!?

Matthayo na Marko mnadai kuwa Yesu aliachwa na Mungu wake ili asurubiwe, na alilia kwa kusema, Eloi eloi lama sabakhtani. (Matt 27:46 na Mark 15:34), ila Luka na Yohana nyinyi hamkubaliani na hili. Pia hata ile anuani iliyokuwa juu ya kichwa hamkubaliani nayo mfano…

Matthayo anasema… HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI,
Marko anasema… MFALME WA WAYAHUDI,
Luka anasema… HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI,
Yohana anasema … YESU MNAZARETI MFALME WA WAYAHUDI.
Matthayo ushahidi wako unaonyesha kuwa kulitokea tetemeko la ardhi wakati wa kusurubiwa kwa Yesu, na makaburi ya watakatifu yakafunguka na watakatifu wakatoka makaburini mwao, kwa maana ya kufufuka na wakaingia mjini Yerusalemu, na kila mtu aliwaona. Cha ajabu hapa wenzio wote hawakuliona hili ni wewe peke yako umeliona hili. Kusema kweli Tetemeko la ardhi ni jambo kubwa sana si rahisi kwa mtu kulisahahu kilahisi hasa ukizingatia kuwa wenzako pia wana roho mtakatifu kama wewe, sasa sijui roho huyo alikupendelea wewe peke yako na akawasahaulisha wengine. Sielewi kwa kweli. This Is Another Gospel Disagreement In The Crucifixion Story.

Yohana ktk maelezo yako uloandika Polisi unasema kuwa Yesu alichomwa mkuki alipokuwa pale msalabani na ikatoka damu na maji, jambo hili wenzio wote hawalisemi (Yoh 19:34). Hata wewe Yohana nakutilia shaka ni vipi maiti ikatoa maji na damu. Kama kweli Yesu alikufa msalabani?
Pia natilia shaka kuhusu bwana Yeheshua kusikia kiu kwake kama kweli alipewa Divai au Mvinyo ulochanganywa na nyongo au alipewa Siki kwa maana ya vinegar?
Hakuna injili hata moja inayomzungumzia kuwa mama yake na Yeheshua yaani Mariam, kuwa alikuwepo kwenye tukio lile kubwa, hata kule kwenye makaburi hakuonekana. Matthayo wewe unawataja watu wawili tu, Mariam Magnalene na Mariamu yule wa pili (Matt. 28:1) Marko wewe pia unamtaja Mariamu Magdalene mama yake na Yakobo na Salome, watu watatu hao sasa (Mark 16:1). Luka unawataja wanawake kutoka Galilya bila kutaja idadi na majina yao (Luk 23:55). Baadae ndo ukatuelezea idadi ya watu si chini ya wane (Luk 24:10). Wakati wewe Yohana unataja kuwa aliye kwenda makaburini ni Mariam Magdalene tu peke yake. Hivi nyinyi nyote hamkuweza kumtaja mama yake na Yeheshua katika kadhia ile kweli, hakuwepo au ndo ktk wale Mariamu mamaye na Yakobo…??!!

Kutokana na maelezo yako pale polisi inaonyesha Matthayo yule mwanafunzi wa Yesu sio Matthayo wewe uliye simama hapa mbele yangu [yesu …aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Matthayo akamwambia nifuate…akaondoka akamfuata]. (Matt9:9) kwa nini isiwe “…akaniona mimi Matthayo…”??!!!
Au nikubaliane na maneno ya Luka na Marko, kuwa wewe si mwanafunzi yule aliyeitwa pale forodhani. Alikuwa ni Lawi aliyeitwa na bwana Yesu. (Luk 5:27, Mark 2:14).
Sasa sijui ni nani mkweli kati yenu…

Marko wewe hukuwahi kumuona yesu wala hukuwahi kusikia sauti yake. Wewe ni mwanafunzi wa Petro ambaye inasemekana ndio alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Kijana Luka wewe ulikuwa mwanfunzi wa Paulo, Paulo ambaye hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Yohana inavyo onekana hukuandika haya, ila wamekubambikia haya ili kuyapa uzito maandishi haya kwa kuyaita Injili. Na ndio maana maneno yenu ya pale polisi yameandikwa “INJILI KAMA ALIVYOIANDIKA …”

Yesu alizungumza lugha ya Aramaic, lugha ambayo ndio tulitarajia injili moja iwepo na si injili hizi ambazo zinapingana, na hii inanipa wasi wasi kuwa mambo yalibadilishwa pale mjini Nacaea mwaka 325 A.D. na kwa uhakika zile injili zinazo karibiana na ukweli(?) ndipo zilipo potezwa. With a lost of original, the road to corruption and distortion becomes wide open. Yohana unanikumbusha Maneno yako, “…Mtanitafuta wala hamta niona…” (Yoh 7:34). Hii inaonyesha kuwa hadith zima ya kusurubiwa kwa Yesu kuwa ni dhana tu yaani ni Drama au mchezo wa kuigiza.
Hii inaonyesha kwamba bwana Yeheshua He was safety from arrest and crucifixion. Kama vile maneno yako Yohana ulivyosema (Yoh 8:29)
“...aliye nipeleka yu pamoja nami; hakuniacha peke yangu…

He Was Not Crucifixion But He Was Crucifiction…

HUKUMU HII NAKUWACHIA NDUGU MSOMAJI. SOMA, ZINGATIA NA KISHA TOA HUKUMU YA HAKI KWA BWANA PILATO.

Cooooooooooooooooourt……………………..!!!

0 comments/Maoni: