Tofauti za kimsingi kati ya Qur’an na Biblia

Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu visivyo pungua 73 kwa mujibu wa madhehebu ya Wakatoliki na kuna yenye vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya Waprotestanti na Kuna ile yenye vitabu 81 kwa madhehebu ya Kanisa la Kiethiopia.

Vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40. Tofauti na Qur’an, yenyewe ni kitabu kimoja kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu mmoja na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.

Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno ya Mwenyezi Mungu, ya Mitume na maoni ya wanahistoria.

Qur’an ni neno la Mwenyezi Mungu tu peke yake. Hata maneno ya Muhammad (s.a.w.) hayamo katika Qur’an.

Katika Agano la Kale na Jipya yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya Mitume mbalimbali. Kumbukumbu la Torati (na Si Torati yenyewe), siyo tu ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu bali pia historia ya maisha ya Nabii Mussa (a.s).

 Injili ya Mathayo, Luka, Marko na Yohana zinaelezea historia ya Yesu kama ilivyosimauliwa na wafuasi wake.

Qur’an si historia ya Muhammad (saw) kama ilivyosimuliwa na maswahaba zake. Qur’an inataja habari za Mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.

Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu Mitume hao. Ndio maana wanazuoni wa kikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika hayo lini

Kwa mfano katika biblia iliyotolewa na Collins iitwayo "Revised Standard Version" ya 1971 uk. 12-17 imeandikwa kuwa Mwandishi wa Samweli hajulikani, pia hajulikani mwandishi wa kitabu cha 2Samweli, 1Wafalme, 2Wafalme, 1Mambo ya Nyakati, Esta, Ayubu, Yona na Habakuki.

Halikadhalika mpaka leo kuna wasi wasi kama kitabu cha Waebrania kiliandikwa na Paulo au na mtu mwingine. Encyclopaedia Britanica inakiri kuwa mpaka hivi sasa hakuna uhakika jinsi gani au ni wapi vitabu vinne vya Injili vilipatikana.

Kinyume chake Qur’an yote iliandikwa wakati wa uhai wa Muhammad na kuhifadhiwa na mamia ya watu.

Injili nne zilizomo katika Agano Jipya siyo Injili zote zilizoandikwa. Zilikuwapo Injili nyingine nyingi. Ila kwa amri ya Mfalme Constantine ilifanyika Sinodi (mkutano wa wawakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua Injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe.

Injili kadhaa zilikataliwa kama vile injili ya Barnabas, Injili ya Marcion, Injili ya Basilides, Injili ya Maryam, Injili ya Yuda, Injili ya Philipo, Injili ya Wahebrania, Injili ya Nazareti, Injili ya Bartholomew na nyingine nyngi (Fungua hapa kuona zaidi).  Na katika historia ya Kanisa viko vitabu vilivyokubaliwa na baadaye kukataliwa na kinyume chake. Ni binadamu waliokuja baadaye ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la Mungu na lipi lisiwe.

Katika uislamu hakukuwa na Ijitimai yoyote iliyokaa kuamua sura ipi iwe Qur’an na ipi isiwe.

0 comments/Maoni: