Ukifungua "Al-Kitaab Al-Muqadis(الكتاب المقدس)' (yaani Kitabu Kitakatifu), bibilia hitumiwayo na wakristo wanaozungumza lugha ya Kiarabu neno Allah limetumiwa kila penye neno Mungu au Yehova.
Kwa wale ambao hawafahamu herufi za Kiarabu nimeweka hapa aya kutoka katika Qur'an ili wapate kulinganisha. Katika aya hizi za kiarabu zilizopo hapa chini, neno la Kiarabu "Allah" nimelikoza ili liweze kutambulika kirahisi. Baada ya kulinganisha aya hizi inategemewa kila mmoja ataweza kuona kwamba neno 'Allah' linaonekana katika Qur'an na pia katika Biblia, kwani ni neno la Kiarabu lenye maana ya Mwenyezi Mungu.
Insha'Allah, mifano hii itaondoa mashaka kwa wale walioingizwa kwenye mkumbo wa kuamini kwamba "Waislamu na wakristo wanaamini Mungu tofauti"
Hakuna njia nyingine ya kuthibitisha ukweli huu isipokuwa kumshauri kila mmoja mwenye mashaka kufanya utafiti wake mwenyewe bila ya upendeleo, chuki na jazba.
[Qur'an 1:1 * tafsiri ya Kiswahili]
"Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu"
"Bismi Allahi ar-Rahmani, ar-Raheem"
بسم الله الرحمن الرحيم
[Mwanzo 1:1 * Biblia ya Kiswahili]
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na na nchi"
[Mwanzo 1:1 *Biblia ya Kiarabu]
"Fiy-al-badi' khalaqa Allahu as-Samawawwat wal Ardh"
فِي الْبَدْءِ خَلَقَ اللهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ،
source: BibleGateway.com - Passage*Lookup: Genesis 1:1;
[Yohanna Mt. 3:16 * Biblia ya Kiswahili]
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa..."
[Yohanna 3:16 * Biblia ya Kiarabu]
"Li-annhu haakadha ahabba Allahu ul 'Aalama hataa badhala"
لأَنَّهُ هكَذَا أَحَبَّ اللهُ الْعَالَمَ حَتَّى بَذَلَ ابْنَهُ الْوَحِيدَ، لِكَيْ لاَ يَهْلِكَ كُلُّ مَنْ يُؤْمِنُ بِهِ، بَلْ تَكُونُ لَهُ الْحَيَاةُ الأَبَدِيَّةُ.
source: BibleGateway.com - Passage*Lookup: John 3:16;
[Luka 1:30 * Biblia ya Kiswahili]
"Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu"
[Luka 1:30 * Biblia ya Kiarabu]
"Laa takhaafiy, yaa Maryam, li-annaki qad wajadt ni'mat(an) 'inda Allahi"
لاَ تَخَافِي يَامَرْيَمُ، فَإِنَّكِ قَدْ نِلْتِ نِعْمَةً عِنْدَ اللهِ
source: BibleGateway.com - Passage*Lookup: Luke 1:30;
[Luka 3:38 * Biblia ya Kiswahili]
"wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu"
[Luka 3:38 * Biblia ya Kiarabu]
"bni anuusha, bni shiyti, bni Aadama, abni Allahi."
بْنِ أَنُوشَ بْنِ شِيثِ، بْنِ آدَمَ ابْنِ اللهِ
source: http://www.biblegateway.com/passage/?search=luke 3:38;&version=28;
[Mathayo 19:17 * Biblia ya Kiingereza * New King James Version]
Yaani "aliye mwema ni mmoja, naye ni Mungu
"there is none good but one, that is, God"
[Mathayo Mt. 19:17 * Biblia ya Kiarabu]
"laysa ahadun saalihaan illa waahdun wa huwa Allahu"
BINADAMU NA UPATIKANAJI WA MVI KATIKA QUR'AN
-
*Msongo wa mawazo katika maisha yetu ya kila siku.*
Sayansi Inathibitisha Kutoka Mvi kwa Haraka kama Ilivyoelezwa Ndani ya
Qur’an
*'MSONGO WA MAWAZO na...
8 years ago
0 comments/Maoni:
Post a Comment