MUNGU ni MWANAUME au MWANAMKE?

Kwanza kabisa kabla ya kuingia kwenye mada nzima iliyo beba kichwa cha habari hapo juu, inatubidi tufahamu nini maana ya Mungu au Mwenyezi Mungu.

Neno Mwenyezi Mungu kwa lugha ya Kiswahili linatumika kwa Muumba wa kila kitu, Mwenye kuabudiwa kwa haki, kinyume na neno 'miungu' ambalo lina maana chochote au yeyote anayeabudiwa si kwa haki. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu ni Muumba wa mbingu na ardhi na kila kilichomo baina yake, naye ni Mlezi wa viumbe vyote na Mpaji riziki kwa kila chenye uhai ulimwenguni.

Mwenyezi Mungu, katika dini na mila nyingi duniani, ni yule anayestahiki kuabudiwa kwa haki ikiwa peke yake bila kushirikishwa na chochote, au kwa kushirikishwa na viumbe vyengine, kwa nia ya kuwa hawa viumbe vyengine vinamkurubisha naye. Hii ni kwa sababu, kila dini au mila ina namna yake ya kumsawiri Mwenyezi Mungu, na njia gani sahihi ya kumuabudu, na kwa kuwa hakuna itifaki baina ya hizi dini, mila na madhehebu kuhusu Mwenyezi Mungu na namna anavyotakikana kuabudiwa, hizi tofauti chungu nzima zimetokea.

Uislamu, kwa mfano, unaeleza kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu hana mshirika, hana mwanzo wala mwisho, hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hapana yeyote mwenye kufanana au kushabihiana naye, naye ni Mola wa ulimwengu huu wote, na Muumba wa kila kitu. Kwake Yeye inatoka riziki ya kila kiumbe, na Yeye ndiye Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha. Marejeo ya viumbe vyote wakishakufa na kufufuliwa ni kwake Yeye tu siku ya Kiyama. Yeye pekee ndiye Mwenye kuhukumu viumbe siku ya malipo, na ndiye atakayewapa waja wake ujira na thawabu na kuwatia Peponi kwa mema waliyoyafanya, au kuwatia adabu na kuwapa adhabu na mateso na kuwatia Motoni kwa maovu waliyotenda hapa duniani.

Imani ya Wakristo
Ukristo unakubaliana na Uislamu katika mengi ya sifa hizi za Mwenyezi Mungu za kuumba, kuhuisha na kufisha, kuruzuku, kufufua, kuhukumu na kulipa ya kheri kwa mwenye kufanya kheri na ya shari kwa mwenye kufanya shari, lakini aghlabu ya madhehebu za Kikristo, ijapokuwa si zote, zinampa Mwenyezi Mungu sifa ya utatu, na kumsifu kuwa ni Mungu Baba, na Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu, na kuwa wote hawa watatu wanashirikiana katika Uungu na kuwa ni kitu kimoja. Uislamu, kwa upande wake, unakataa katakata mas-ala ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na kwa hivyo ni Mmoja tu wala hana mshirika wa aina yoyote.

Dini nyinginezo
Dini nyenginezo, kadhalika, zina tasauri na fikra nyengine kuhusu Mwenyezi Mungu. Kuna wale wanaoabudu viumbe mbali mbali wakichukulia kuwa wanamwakilisha Mwenyezi Mungu, kama kuabudu masanamu, nyota, jua, ngo'mbe, wanyama mbali mbali, mizimu, miti, panya, nyani, moto, viumbe wenziwao, malaika na majini na kadhalika. Dini na mila hizi, pengine huchukulia kuwa vitu hivi vinatusaidia kutufikisha kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa bila ya vitu hivi, ibada zetu haziwezi kufika. Ama wengine huwa na imani kuwa vitu hivi ndio Mola mwenyewe wa kuabudiwa na kuombwa na kutakwa msaada.

Majina
Mwenyezi Mungu anamajina au anajulikana kwa majina mengi sana. Kila kabila au taifa linamjuwa kwa majina tofauti tofauti. Ukiangalia Iman ya dini kuu tatu duniani yaani Uislam, Uyahudi na Ukristo, hawapishani sana kwenye upande wa majina. Allah, Yahwe, Yehova ni katika majina yanayojulikana sana kwenye dini hizi tatu.

The word "Allah" is the perfect description of the "One God" of monotheism for *Jews, Christians and Muslims!

Jina "Allah" alitumiki tu kwa Waislam, bali utumiwa pia na dini tatu zinazojulikana kama Abrahamic Faiths. (*Angalia hapo juu)

Jina "Allah" utumiwa na Wakristo wa Kiarabu, au Waarabu walioko kwenye dini ya kiyahudi (Christian and Jewish Arabs). Na Jina hili linapatikana kwenye Biblia ya Kiarabu na pia kwenye maandiko ya Kiyahudi kwa maana ya Mungu.

Ukiangalia Biblia ya Kiarabu kwenye agano la kale ukurasa wa kwanza neno Allah limetajwa mara 17. Jina hili pia alikukosekana kwenye agano jipya pale kwenye neno ‘Mungu’ kwenye Biblia ya kiarabu limeandikwa ‘Allah’.

"Allah" limetokana na "Illah" but it brings more clarification and understanding.

In answering the question. "Mungu ni Mwanaume au Mwanmke" inatukubidi kwanza tuelewe kuwa Mungu did not appear in any physical form anywhere in the Qur’an or Bible.

Tunasoma kwenye Qur’an sura ya 112 (Al-'Ikhlas)
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja

In the Name of Allah, the Merciful, the Most Merciful
Say: 'He is Allah, the One, the called upon.
Who has not given birth,
and has not been born,
and there is none equal to Him'

1 Yohana 4:12 inasema,
Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu.

Kwenye " Kutoka (exodus)33:20 Allah says,
"And he said, Thou canst not see my face; for man shall not see me and live." God said, "I will make my Goodness pass right in front of you; I'll call out the name, God, right before you. I'll treat well whomever I want to treat well and I'll be kind to whomever I want to be kind." God continued, "But you may not see my face. No one can see me and live." KJV

And he said, I will make all my goodness pass before thee, and I will proclaim the name of the LORD before thee; and will be gracious to whom I will be gracious, and will shew mercy on whom I will shew mercy. And he said, Thou canst not see my face: for there shall no man see me, and live.
The massage

Katika kitabu cha Kutoka 20 Allah anasisitiza kuwa:
Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu [Elohim] ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa, BWANA, Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami huwarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.

Hii ina maana hataki kufananishwa na yeyote wala chochote...!

Kwa lugha ya Kiarabu neno Allah halina Jinsia (Has no gender not male and not female)

Kwenye lugha ya Kiswahili hatuna matatizo ya kutambulisha kike au kiume. Unaposoma Biblia ya lugha ya kiingereza neno "He" limetumika kwa heshima na wala halimaanishi kwamba Mungu ni Mume. (is used only out of respect and dignity - not for gender).

Neno Allah halina wingi (Always singular - Never plural).

Lakini mtu waweza kujiuliza mbona kwenye baadhi ya aya za Qur’an na Biblia kumetumika wingi, je hii haionyeshi kuwa kuna miungu zaidi ya mmoja yawezekana mmoja akawa mke?

Kwenye uislam hili si tatizo na wala si hoja kubwa ya kushangaza. Qur’an imeshajibu hilo tayari, kwenye kwenye surat Ikhlas. Yaani …hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna anacho fanana nacho…

Wingi au mfano wa neno hili "We" is used only as the "Royal WE" just as in English for royalty and respect.

Allah Means "The Only One to be Worshipped"

Kama nilivyozungumza hapo mbele kutumika kwa “He na Him” ni lugha ya kiheshima tu au ni kule kutokuwa na fonimu za kuahinisha ili kupata tafsiri iliyokuwa sawa na ya kiarabu...

Tunafundishwa kuwa Mungu ni roho yaani pure spirit kwa maana kuwa hana umbo wala hana physical reproductive parts of a man or a woman.

Yohana 4:24 inasema,
"Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa Roho na kweli."

"God is spirit, and his worshipers must worship in spirit and in truth."

Ukisoma Biblia za kiingereza mfano Yohana na sura nyinginezo wametumia masculine term "Him au His" Na hii imewapelekea watu wengi hususani wakristo kufikiria kuwa M’Mungu ni Mume au Mwanaume.Tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa upande wa wakristo kiasi ya kwamba wameamua kutoa Biblia mpya ambayo imeondoa tatizo hili la Jinsia au Gender (gender-neutral language), lakini kabla ya kukubaliana na hili swala la Jinsia, wasomi wa kikristo walijadili mambo mengi sana na jina gani watumie mfano walijadili waihite "inclusive language," "gender-inclusive language," "gender generic language," "non-sexist language," etc. kuna waliopendekeza kuwa hiitwe "gender accurate language".

Baadhi ya seminary za ulaya zimepiga marufuku utumiaji wa neno "He" kwa maana ya Mungu. Mfano badala ya kutumia neno "God himself" wanatakiwa watumie "God Godself".
Palipokuwa panaonyesha "He" wameweka neno GOD. Na kama linamuhusu binadamu kwa maana ya neno 'Man' wameweka neno Person.

Mfano Proverb 12:2
A good man shall obtain favor of Jehovah; But a man of wicked devices will he condemn.(ASV)

A good person basks in the delight of GOD, and he wants nothing to do with devious schemers.
(The Message)

Ndani ya Qur’an tunasoma maneno haya toka surat Luqman.31:13-15
And when Luqman said to his son, in warning: 'My son, associate none with Allah, to associate others with Allah is a tremendous wrong. ' And We charged the human concerning his parents, for his mother bore him in weakness upon weakness, and his weaning was in two years. Be thankful to Me and to your parents, to Me is the arrival. But if they strive with you to make you associate with Me that of which you have no knowledge, do not obey them. And accompany them in this life with kindness; and follow the Path of he who turned to Me. To Me you shall return and I will inform you of all that you have done.

Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa.Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.

Aya inajieleza wazi kuwa Mungu keshakataa kufananishwa na kinyago chochote…

Ukiendelea mbele ndani ya sura hii hii tunasoma…31.20-21
Do you not see how Allah has subjected to you all that is in the heavens and the earth, and lavished on you His visible and unseen favors? Yet some people would argue about Allah without knowledge, or guidance, or an Illuminating Book. 'When it is said to them: 'Follow what Allah has sent down, ' they reply: 'No, rather we will follow that which we found our fathers upon. 'What! Even though satan is inviting them to the punishment of the Fire?
Qur'an 31:20-21

Kwani hamwoni ya kwamba Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni viliomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za dhaahiri na za siri? Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu pasipo ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru.Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, husema: Bali tunafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je! Ijapo kuwa Shet'ani anawaita kwenye adhabu ya Moto uwakao?

Ukisoma Kutoka 1:26: kwenye Biblia ya kiingereza utakuta maneno haya…
"Then God said, 'Let us make man in our image, in our likeness...

Kwa lugha ya Kihibrania neno "man" ni ‘Adam’ which can be translated as "mankind or humanity":

Tafsiri ya kiingereza limelichukuwa hili neno "man" kwa maana ya the whole of humankind - both men and women.

Biblia inayopigania mambo ya jinsia neno 'Man' limeondolewa na kuwekwa Human au them au Person.

Japokuwa wataalamu wa biblia wanatufahamisha kuwa Men and women are only patterned after the image of God-not identical replicas. This fact does not require God to have a body like a man or a woman. Being made in the image of God has nothing to do with physical characteristics.

Pia haimaanishi kuwa Mungu ni Kuntha yaani female+male.

BABA
Ndani ya Biblia kuna maneno yanayofikia 170 kumwelezea Mungu kwa jina la baba. Na hii inatokana na asili ya ubinadamu kuwa Baba ndo mlinzi wa familia na ndo mwenye kutunza familia. Ndo maana hata kwenye baadhi ya vitabu vya dini utakuta maneno kama Protector, supplier or provider. nk.

Women in Ministry chapter argues that "the equal pairing of male and female in parallel with ha’adam [man] in this verse [shows that] there is no hint of Ontological or functional superiority-inferiority or headship-submission between male and female. . . . Both participate equally in the image of God.

"The Qur’an 2:255. tells us:
Allah! La ilaha illa Huwa (There is no god to worship except Him), the Ever Living, the Sustainer and Protector of all that exists. He doesn't get tired and He doesn't sleep. Everything in the universe belongs to Him. Who then, could intercede between Him and his creatures without His Permission? He Knows everything about them and they have no knowledge except as He wills. His kursi extends over the entire universe and He doesn't get tired of guarding and preserving it. He is Most High, the Most Great.

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani.Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.

0 comments/Maoni: