Kwa Nini Waislam Wanasoma Biblia?

Yamekuwepo majaribio ya nguvu toka kwa viongozi wa Kanisa kuzuia Waislamu wasitumie Biblia katika mahubiri yao. Sababu wanayotoa ni kuwa, Biblia ni Kitabu cha Wakristo, hivyo wasikitumie. Kwa bahati mbaya sana shutuma hizo zinatolewa na Wanatheolojia waliosoma theolojia kwa kiwango cha juu. Hivyo wanajua kabisa wanachokifanya. Wakristo wengi siku hizi wakiongozwa na maaskofu, mapasta, mapadri na hata walei wa kanisa, haweheshi kujiuliza “hivi kwa nini siku hizi waislamu wanachambuwa sana biblia…!!?” Hii inanikumbusha methali moja ya Kiswahili isemayo ivi… “aliyekula usahau ila aliye zowa si rahisi kusahau…!”

Waislamu hawakuwa watu wa kusoma na kujadili au hata kuchambua biblia kabla. Waislam walikuwa na Qur’an yao na wakristo na biblia yao. Sasa mambo haya yalianzaje basi…?! Leo hii wakristo wameshasahau kuwa ni wao ndio walio wapelekea waislam biblia. Wakristo walikuwa wakionekana majiani, vituo vya mabasi, masokoni wakiubili kwa ghamu kubwa “…mfuate Yesu utaokoka…!” Wahubiri wengine walitufuata mashuleni na kutugawia zawadi za biblia na wengine wakadiriki kutufuata mpaka majumbani mwetu, wakipita mlango kwa mlango kutuhubilia injili. Waislamu tu watu wakarimu sana, tuliwakaribisha na kuwasikiliza. Huku tukiwapa kile kidogo Allah alichoturuzuku. Wengi wao walikuwa hawataki tuwaulize maswali. Tulivumila usumbufu wote huo na tukapokea zawadi za biblia, majarida na vitabu kadhaa wakadhaa vya kikristo. Wengi wetu tulivisoma vitabu vyao na wachache hawakuthubutu kuvisoma.

Wakristo walijuwa tu mradi wametuwachia vitabu ipo siku kama si sisi basi ni watoto zetu watakuja visoma vitabu hivyo. Na ni kweli wazazi na watoto walivisoma vitabu hivyo. Kuna walio viona kuwa havina faida kwao na kuna walioviona kuwa vinahitaji uchunguzi wa kina, kwa kile walichokuwa wanakisoma.

Mimi binafsi sikumbuki haswa nilianza kusoma biblia na baadhi ya vitabu na majarida ya kikristo. Ninacho kumbuka nikiwa bado na umri kati ya miaka tisa nilikuwa tayari ni msomaji wa biblia na vijarida vya kikristo.
Na sikuishia kuhudhuria vipindi vya kikristo pale shuleni kwetu bali nilikuwa nakwenda hata kule kanisani kuangalia sinema za kikristo na wakati mwingine tulipokea zawadi za peremende na biskuti. Na baadhi ya wenzetu walipewa mpaka nguo kutoka kwa ma’father na ma’sisters wa kanisani. Mimi binafsi nakumbuka zile sinema za Yesu (?!) na baadhi ya mitume wengine waliotajwa ndani ya biblia. Wakati mwingine tulioneshwa sinema za wale wachekeshaji wawili maarufu ambao tuliwapachika majina ya Chale mnene na Chale mwembamba… na wakati mwingine tulionyeshwa sinema za Charles Chaplin.
Hawa watu walikuwa na malengo yao… Nia ilikuwa kutuweka karibu na kanisa na ikiwezekana kutubatiza na kupata wafuwasi wapya.

Kampeni hizi hazikuishia hapo tu, ilitafutwa mikoa yenye shida na matatizo mbali mbali na kuutumia mwanya huo wa matatizo ya watu kwenda kuwahubiria injili ili kupata wafuwasi wapya. Tulishuhudia mahospitali ya serikali na magesti house mengi yakiwa na biblia za agano jipya.

Waislamu baada ya kusoma wakataka kujuwa zaidi kuhusu mambo mengi waliyasoma ndani ya biblia. Wakristo walipokuwa wakipita tena kwenye majumba yetu, tukawauliza tena maswali mengi na asilimia 99% ya maswali tuliyo wauliza hayakupata majibu muwafaka. Wengi wao walidai kuwa hatuna roho mtakatifu ndo maana tunauliza uliza maswali mengi.

Wengi wetu tukabakizwa na hamu kubwa ya kuujuwa ukristo... Baadhi tukabahatika kusoma vitabu mbali mbali vinavyo uhusiana na ukristo. Vikiwemo vitabu vinavyo elezea elimu ya Theology (elimu ya uungu). Na tukajifunza mambo mengi sana kuhusu elimu za Theosophy. Hii ni elimu ya Religious Philosophy (Falsafa ya Dini). Theosophy ni muunganiko wa maneno mawili, Theos yaani mungu na Sophia likiwa na maana ya Busara au Hikma. Kwa kiingereza tunaweza kusema kuwa ni Divine wisdom. Elimu hizi ukiziangalia asili yake zimeegemea sana kwenye falsafa za kigiriki. Hata somo linalo husu siku ya mwisho yaani Kiyama (Eschatology) yaani study of last time. Limeegemea sana kwenye kitabu kinacho aminiwa na wakristo kuwa kimeandikwa na Yohana wa Zebedayo, alipokuwa kifungoni kule Asia ya kati. Somo la Angelology* na somo la Demonology**

*Angelology: that treatise in systematic theology which studies the function, nature and hierarchies of angels, as well as their cult and iconography.
** Demonology: the study of demons, their nature as fallen Angels and their role in tempting and harming human being.


Vile vile kuna elimu ya mambo ya taswira na alama yaani Iconology (image and symbol). Kuna somo linalo husu uungu wa Yesu yaani Christology. Kwa ujumla somo la thologia ya kikristo imeegemea sana mawazo ya Kiyunani (Ancient Greek). Ukisoma ukristo hukosi kugunduwa kuwa kuna kushabihiyana na dini za kale, kama vile Mithraism. Dini iliyoanzia India ikafika mpaka Mesopotamia, Iraq ya kale.

Biblia ni kitu gani?
Biblia ni neno la Kigiriki lenye maana ya vitabu. Yaani ni mkusanyiko wa vitabu tofauti tofauti.
Kwa mujibu wa wakristo maana ya Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vya Agano la Kale, Na Agano jipya yaani, Injili na nyaraka za Mitume wa Yesu (as). Na barua za Paulo.

Kitheolojia na Kiebrania Agano la Kale linaitwa "Tanaki", yaani `Torati" (Torati au Sheria), "Tanaki" ni kitabu kinacho tumiwa na dini ya Kiyahudi (Judaism). "Tanaki" zipo za aina mbili, ipo ya Kiebrania (Hebrew text) iliyotumiwa na Wayahudi waliokuwepo ndani ya Jerusalem na ya tafsiri ya Kigiriki ambayo baadaye iliitwa "Septuaginta", yaani tafsiri ya watu sabini. Imeitwa hivyo kwa kuwa ilitafsiriwa ya watu sabini katika mji wa Alexandria (Misri) katika karne ya tatu kabla ya Kristo. "Septuaginta" ina vitabu vingi zaidi kuliko "Hebrew text". Aidha, baadhi ya vitabu vyake ni virefu na vina maneno yasiyo kuwemo katika kitabu cha Kiebrania (angalia vitabu vya Esta na Daniel).

Hii Biblia ya Kiswahili tuliyoizoea (Union Vision) imefasiriwa toka Biblia ya King James amabayo imetokana na "Septuaginta" Tafsir ya kigiriki, ambayo haikutumiwa na Nabii Yesu (as), wanafunzi wake wala Wakristo wa mwanzo kabisa.
Maandiko Matakatifu ya Wakatoliki yanajumuisha vitabu vya "Apocrypha" (vitabu vilivyofichikana). Waprotestanti hawakubali kitabu chochote katika vitabu hivi.

Matoleo mbali mbali ya biblia
Wakubwa wa makanisa baada ya kugunduwa kuwa ukweli wote unaanikwa adharani. Nao wakawa na mbinu zao za kujirinda na kile kinacho gundulika siku hadi siku. Mbinu mojawapo ni hii ya kubadilisha baadhi ya vipengele vya biblia. Na hii ikapelekea kupatikana version mbali mbali za biblia. Hali hii si kama ilikubalika na makanisa mengine. Wako baadhi ya wakubwa wa makanisa waliogunduwa tatizo hili la tafsiri ya biblia wakaamua kujitenga na kuanzisha madhebu yao, wapo walioamua kuiandika tena bibli kabla ya vuguvugu la waislam na waandishi wa kimagharibi kuanza kuwauliza maswali kuhusu imani hii ya ukristo. Mfano mmoja wapo mdogo tu ni biblia ya King James Version. Biblia hii peke yake ina version zisizo pungua sita kuna King James Version 1611, King James Version. (KJV) 2000, King New Testament, Defined King James Bible, New King James Version (1979, 1982) (NKJV), 21st century King James Version.
Version hizi pekee si kwamba zina fanana, kila version inatofautiana na nyingine aidha kwa kuongeza baadhi ya mambo au kupunguza kile ambacho wanakiona kuwa kitawasumbuwa baadae. Biblia hii si kwamba kwa kuierekebisha kwake kwingi imekuwa bora, lah hasha... Bado hata wale waliokuja kuandika Revised Standard Version of Bible (RSV) baada ya ile ya king James wanatufahamisha kuwa toleo la King James si kamirifu na lina makosa mengi sana. Angalia Dibaji ya kwenye Revised Standard Version.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuudia mabadiriko makubwa sana kwenye tafsir za biblia. Hususani kwenye matoleo ya biblia za kiingereza. Kwenye pekua pekua yangu, siku moja nilibahatika kununua tafsiri ya Revised Standard version (Biblia Sanifu Iliyo Sahihishwa). Biblia hii ni tofauti sana na zile tulizo zizoea. KJV na RCV.

Katika dibaji ya Biblia ya RSV waandishi wameandika kwenye Dibaji maneno yafuatayo:
"The Revised Standard Version of the Bible is an authorized revision of American Standard Version, which published in 1901, which was a revision of the King James Version, published in 1611... KJV had to compete with the Geneva Bible in popular use; but in the end it prevailed, and for more than two and a half centuries no other authorized translation of Bible into English was made... Yet the King James Version has grave defects. By the middle of the nineteenth century, the development of Biblical studies and the discovery of many manuscripts more ancient than those upon which the King James Version was based, made it manifest that these defects are so many and so serious as to call for a revision of the English translation... "....decision was reached that there is need for a thorough revision of the version of 1901..."
(Tafsiri hisiyo rasmi) “Biblia ya RSV ni masahihisho yaliyoruhusiwa kufanywa kwa nakala ya American Standard Version (ASV) (Nakala Sanifu ya Marekani) iliyochapishwa mwaka 1901, ambayo nayo ilikuwa ni masahihisho ya King James Version (KJV) (Nakala ya Mfalme James), iliyochapishwa 1611... KJV ilikuwa ni lazima ishindane na Geneva Bible (Biblia ya Geneva – 1560) kwa umaarufu wake; lakini mwishowe ikashinda, na kwa zaidi ya karne mbili na nusu (zaidi ya miaka 250) hakuna tafsiri nyengine yoyote iliyoidhinishwa ya Biblia kwa Kiingereza ilifanywa. KJV ndiyo iliyokuwa “Nakala Iliyo Ruhusiwa” kwa watu wanaozungumza Kiingereza… Japokuwa KJV ina dosari na upungufu mkubwa sana(grave defects). Katikati ya karne ya 19, muendelezo wa somo la Biblia na kupatikana kwa miswada mingi ya kale zaidi kuliko yale yaliyotegemewa na KJV, ilidhihirika kuwa dosari hizi ni nyingi, nzito na kubwa, hivyo kuitisha masahihisho ya tafsiri ya Kiingereza. Kazi hiyo ilifanywa, na wenye mamlaka wa Kanisa la Uingereza, katika mwaka wa 1870. English Revised Version (Nakala ya Kiingereza Iliyosahihishwa) ya Biblia ilichapishwa katika kipindi 1881 – 1885; na ASV, kibadala chake kilichounganisha uteule na upendeleo wa wanazuoni wa Marekani walioshirikishwa katika shughuli hiyo, ilichapishwa mwaka wa 1901”. (The Holy Bible: Revised Standard Version, uk. iii.)

“ASV iliwekewa haki ya kunakili, kuilinda matini yake kutokana na mabadiliko yasiyoidhinishwa. Katika mwaka wa 1928, haki hii ya kunakili ilipatiwa International Council of Religious Education (Baraza la Kilimwengu la Elimu ya Kidini), hivyo kuingia katika umiliki wa Makanisa ya Marekani na Canada, ambayo yalishirikishwa katika Baraza hiyo kupitia kwa kamati na halmashauri za elimu na uchapishaji. Baraza ilichagua kamati ya wanazuoni ili wamiliki matini na andiko la ASV na kufanya uchunguzi kama nakala hiyo itahitaji masahihisho ya ziada… [Baada ya miaka miwili] uamuzi ulifikiwa kuwa ipo haja ya kufanya masahihisho kamili kwa nakala ya 1901, ambayo itabaki kuwa karibu iwezekanavyo na ada ile ya Tyndale-King James… Katika mwaka wa 1937 masahihisho yaliruhusiwa kura ya Baraza” (The Holy Bible: Revised Standard Version, uk. iii - iv).

“Wanazuoni thelathini na mbili (32) walishiriki kama memba wa Kamati iliyopatiwa jukumu la kusahihisha na walikuwa tayari wamepewa ruhusa ya kuchambua, kuhakiki na ushauri wa Kamati ya Ushauri ya wakilishi hamsini (50) kutoka katika madhehebu yanayoshirikiana… RSV ya Agano Jipya ilichapishwa 1946”(The Holy Bible: Revised Standard Version, uk. iv). “RSV ya Biblia, iliyokuwa na Agano la Kale na Jipya, ilichapoishwa Septemba 30, 1952, ambayo imekubaliwa sana” (The Holy Bible: Revised Standard Version, uk. iv).
''KJV ya Agano Jipya ilitegemea matini ya Kiyunani iliyoumbuwa na kuharibiwa na makosa, ikiwa na makosa yaliyokusanyika kwa karne kumi na nne (14) ya kunakili miswada. Kimsingi hii ilikuwa ni matini ya Kiyunani ya Agano Jipya kama ilivyohaririwa na Beza, 1589, ambaye alifuata kwa karibu ile iliyochapishwa na Erasmus, 1516 – 1535, ambayo ilitegemea miswada michache ya kale. Ya kale na miswada mizuri zaidi ambayo Erasmus aliitumia ni yale ya karne ya kumi, naye aliyatumia kwa uchache sana kwa sababu yalitofautiana sana na maandiko yaliyopokewa; Beza alifanikiwa kupata miswada miwili yenye thamani kubwa, yaliyoandikwa baina ya karne ya tano na sita, lakini aliyatumia kwa uchache sana kwa sababu yalitofautiana na andiko lililochapishwa na Erasmus'' (The Holy Bible: Revised Standard Version, uk. v)

Katika Biblia ya RSV, idadi kubwa ya vifungu muhimu kutoka kwa Agano la Kale na Jipya ya KJV, ambazo wanazuoni wa Biblia walihitimisha kuwa ziliongezwa katika karne za baadaye, ziliondolewa kutoka kwa matini na kuwekwa kuwa tanbihi chini ya kurasa. Kwa mfano, kifungu maarufu katika Injili ya Yohana 8: 7 kuhusu mzinzi mwanamke ambaye alikaribiwa kuuawa kwa kupigwa mawe. Ilisemekana kuwa Yesu alisema:

Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe”.
Yohana 8:11

Tanbihi za chini ya kurasa katika RSV ya Biblia (ya 1952) inasema:
“Hati kongwe za kale hazina sehemu hii John 7: 53 hadi John 8: 11” (The Holy Bible: Revised Standard Version Uk 96). *("most ancient manuscripts omit this verse" or, "this verse is not found in earliest manuscripts.")

Kuanzia kwa mswada wa Vatican nambari 1209 na mswada wa kodeksi ya Sinai kuanzia karne ya nne hazina kifungu hiki cha aya kumi na mbili (12), wanazuoni wa Biblia wameamua kuwa maneno haya hayawezi kunasibishwa kwa Yesu. Mfano mwengine ni kifungu kinacho nasibishwa na Yesu na kutumiwa kama dalili ya Utatu katika Maandiko Matakatifu. Katika 1 Yohana 5: 7, Yesu alinukuliwa kuwa amesema:

Basi wapo mashahidi watatu wanaoshuhudia mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtkatifu: na hivi vitatu ni mmoja
KJV.

Mwanachuoni maarufu wa Biblia, Benjamin Wilson, anaandika kuwa kifungu kinachohusu “mashahidi wa mbinguni” hakipo kabisa katika mswada wowote wa Kiyunani ulioandikwa kabla ya karne ya 15! Kwa hiyo, katika RSV, aya hii iliondolewa katika matini bila ya kuekewa tanbihi yoyote. Hata hivyo, ili kubakisha jumla idadi ya aya katika RSV sawa kama zile za KJV, wasahihishaji waliigawa aya ya 6 kuwa ni aya mbili.

Toleo la Pili kwa tafsir ya Agano Jipya (1971) ilifaidika kutokana na masomo ya kimatini na ya hisimu iliyo chapishwa kuanzia Agano Jipya la RSV ilipotolewa 1946 (Revised Standard Version, uk. vi.). Baadaye, baadhi ya vifungu vilivyofutwa vilirudishwa, na baadhi ya vifungu vyengine vilivyokubaliwa vilifutwa. “Vifungu viwili, mwisho mrefu wa Marko (16: 9 – 20) na kadhiya ya mwanamke aliyeshikwa katika uzinzi (7: 53 – 8: 11), zilirudishwa katika matini, ikiwa zimetengwa na nafasi tupu isiyo andikwa kitu na kufuatiliwa na maneno yenye kujuvya… Kwa kusaidiwa na mswada mpya, vifungu viwili, Luka 22: 19b – 20 na 24: 51b, zilirudishwa katika matini, na kifungu kimoja, Luka 22: 43 – 44, kiliwekwa katika tanbihi ya chini ya kurasa, kama vile ibara ya Luka 12: 39” (The Holy Bible: Revised Standard Version, uk. Vii).
Kulingana na wanazuoni wa Biblia, hata utunzi wa vitabu vya Agano la Kale na Injili zenyewe zina shaka na utata.
Vitabu vitano vya kwanza vya Biblia (Pentateuch, Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Taulati.)
kiada zinanasibishwa na Nabii Musa (‘as), (Mayahudi wa Kiothodoksi (wenye imani halisi) wanadai kuwa Torah (Taurati) jina la Kiyahudi kwa Vitabu vitano vya kwanza, ilianzishwa kwa kuumbwa vizazi 974 kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Kulingana na wao, Mwenyezi Mungu alitoa imla ya Taurati katika siku arobaini (40) za Musa kuwa katika Mlima Sinai, katika hali yake ya mwisho na mfumo usiobadilika na kuwa ni makosa na madhambi kwa mtu kudai kuwa Musa aliandika hata herufi moja kwa nafsi yake mwenyewe).
Hata hivyo, zipo aya nyingi sana katika vitabu hivi ambazo zinaashiria kuwa haiwezekani kwa Nabii Musa (as) kuwa aliandika kila kitu ndani yake. Kwa mfano, Kumbukumbu la Sheria 34: 5 – 8 inayosema:


''Basi Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu akafariki huko nchini Moabu kulingana na neno la Mwenyezi Mungu alilosema. Mwenyezi Mungu akamzika katika bonde la Moabu, mkabala wa mji wa Beth-peori; lakini mpaka leo, hakuna mtu ajuaye mahali alipozikwa. Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; macho yake yalikuwa hayajafifia, na alikuwa timamu na mwenye nguvu. Waisraeli waliomboleza kifo chake kwa muda wa siku thelathini kwenye nchi tambarare ya Moabu. Kisha siku za matanga na maombolezo ya kifo chake zikaisha”.

Ni dhahiri kuwa mtu mwengine ndiye aliyeandika aya hizi kuhusu kifo cha Nabii Musa (as).
Baadhi ya wanazuoni wa Kikristo wameelezea hitilafu hizi kwa kutoa maoni kuwa Musa aliandika vitabu vyake, lakini Manabii waliokuja baadaye, na vile vile waandishi wanaopata wahyi, waliongeza yaliyotajwa kabla. Kwa hiyo, kulingana na wao, matini yenyewe, kwa ukamilifu wake, ilibaki kuwa ni maandiko ya ufunuo ya Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, maelezo hayo hayakuweza kusimama mbele ya uchunguzi makini, kwa sababu ya mtindo na sifa bainifu ya fasaha wa aya zilizotomwa ni sawa na matini iliyobaki.

Katika karne ya 19, wanazuoni Wakristo wa Biblia walianza kujadili maana ya “nenokikoa” yanayopatikana katika Taurati. Hizi ni Hadithi zinazopatikana mara mbili, kila mara na ziada tofauti. Miongoni mwayo ni tafsiri mbili kwa uumbaji wa ulimwengu, ahadi baina ya Mwenyezi Mungu na Ibraahim, ya Mwenyezi Mungu kubadilisha jina la Yakobo kuwa Israili na Musa kupata maji katika jabali. (Who Wrote the Bible, uk. 54 – 70).

Watetezi wa utunzi wa Musa wanasema kuwa manenokikoa hayana upinzani wala migongano, lakini ya kuelimisha. Lengo hasa ni kutufundisha sisi kuhusu maana ya ndani na kina ya Taurati kwa ustadi. Hata hivyo, dai hili liliwekwa kando baada ya muda mchache na wanazuoni wenye akili ya wazi ambao walitoa maoni kuwa sio tu baadhi ya hadithi zina ukinzani wa dhahiri, lakini pia lau manenokikoa yatatenganishwa kuwa hadithi mbili tofauti, kila moja kwa uthabiti inatumia jina tofauti la mwenyezi Mungu. Moja inamtaja Mwenyezi Mungu kila mara kwa Yahweh/ Yehovah (Jehovah). Waraka huu unaitwa “J”. Nyengine wakati wote inamtaja Mwenyezi Mungu kwa jina Elohim, na hivyo kuitwa “E”
. (Mwanachuoni wa Kijerumani katika mwisho wa karne ya 19, Julius Wellhausen, alikuwa wa kwanza kutambua machimbuko mengi sana kwa vitabu vitano vya kwanza)
Zipo sifa bainifu za fasihi nyengine tofauti zinazopatikana sana kwa waraka mmoja au mwengine. Wataalamu wa kisasa wa lugha wamechambua, kulingana na Profesa Richard Friedman (Richard Elliot Friedman ni Profesa katika Chuo Kikuu cha California huko San Diego. Alipata shahada ya udaktari katika Biblia ya Kiebrania katika Chuo Kikuu cha Harvard, na ni mtunzi wa kitabu kilicholeta ubishani, Who Wrote the Bible).


Inaonyesha kuwa vitabu vitano vya Musa ni mchang’anyiko wa Kiebrania kuanzia karne ya tisa, nane, saba na sita kabla ya kuzaliwa kwa ‘Iisa (as). Hivyo, Musa, aliyekuwa hai katika karne ya 13 Kabla ya ‘Iisa (as), alikuwa mbali sana na Kiebrania cha Biblia kuliko Shakespeare kutoka kwa Kiingereza cha leo.
Utafiti zaidi wa Pentateuch ulileta uvumbuzi kuwa haikutengenezwa na machimbuko mawili makuu bali manne. Ilivumbuliwa na kuonekana kuwa baadhi ya hekaya hazikuwa tu ni manenokikoa bali ni pacha tatu (sei ya vitu vitatu). Nyongeza ya fasihi kwa sifa bainifu zilitambuliwa kwa nyaraka hizi. Chimbuko la tatu liliitwa “P” (kumaanisha kasisi/ priestly), na ya nne kuitwa “D” (kumaanisha Kumbukumbu la Taulati/Deutoronomy) (The Interpreter’s Dictionary of the Bible, Mj. 1, uk. 756, na Mj. 3, uk. 617. Pia tazama The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 773 – 774.)


Kiwango cha kujua nyongeza zisizo dhahiri zilizofanywa kwa matini ya asili ni vigumu kubainisha. Kwa hiyo, ipo shaka kubwa sana kwa utunzi wa vitabu vyote kwa ujumla.
(Kwa msaada mkubwa kutoka Kitabu cha Doctor. Abu Ameenah Bilaal Philips)

Toleo la RSV lilipo toka kulikuwa na kampeni kubwa kubwa na majisifu kutoka kwa waandishi na wachapishaji wa toleo hili la RSV.

''The Finest Version Which Has Been Produced In The Present Century."
– (Church of England Newspaper)

"A Completely Fresh Translation By Scholars Of The Highest Eminence."
- (Times Literary Supplement)

"The Well-Loved Characteristics Of The Authorised Version Combined With A New Accuracy Of Translation."
- (Life and Work)

"The Most Accurate And Close Rendering Of The Original"
- (The Times)

The publishers (Collins) themselves, in their notes on the Bible at the end of their production, say on page iv:

This bible (RSV) is the product of thirty-two scholars, assisted by an advisory committee representing fifty co-operating denominations.


0 comments/Maoni: