JE UNAJUA (DO YOU KNOW)

1. Kuwa Qur'an ndio kitabu pekee ulimwenguni kinachotumiwa na watu wengi na hakijabadilika wala kubadilishwa tangu kilipo teremshwa duniani?

3. Kuwa sura 54:1 aya hii ya kwanza sura 54 ukihesabu aya zilizokuwa mbele yake unapata aya 1389. na 1389 huu ndio mwaka wa Hijiria ambao Neil Armstrong alitua mwezini. Neil Armstrong alituwa mwezini mwaka 1969. Na kuna aya 4845 toka sura 1:1 mpaka aya ya kwanza ya sura 54.

4. Je unajua kuwa muda aliondoka mwezini ni 17: 54: 1 (Universal Time) or 1: 54: 1 (EDT) na hinashabiihana na sura 54:1

5. Je unajua kuwa sura 111:1-5 inamzungumzia Abu Lahab ambaye alikuwa anampinga sana Mtume (saw) kwa kila jambo mfano Mtume akisema hii ni nyeupe yeye husema hii nyeusi, lakini cha ajabu iliposhuka aya hii na yeye anajua kuwa kuna aya imemtabiria kuingia Jahanam yeye na Mkewe, na amekaa miaka kumi mbele na aya ipo na yeye hata siku moja hakuipinga mpaka anakufa. Na laiti angepinga basi Qur'an ingetiliwa shaka kubwa na makafiri.

  1. Unajua kuwa neno Bahr yaani (Sea or Water) limetajwa mara 32 ndani ya Qur'an na neno barr, (yabas), yaani nchi kavu (Landmass), limetajwa mara 13. Na ukitafuta uwiano kwa asilimia kati ya landmass na sea inakuwa kama ifuatavyo:

32+13 = 45 [32/45x100% = 71.1111111% Sea]

na ukichukuwa

[13/45x100% = 28.888888889% Landmass]

na kwa mahesabu ya karibu tunakisia kuwa

71.111111~ 71%

na hii ndio uwingi wa maji katika Dunia yetu. Na

28.88888889% ~ 29%

na hii ndio ukubwa wa ardhi tulio kuwa nayo.

71+29=100

7. Je unajua kuwa MwenyeziMungu ametufunulia idadi ya miezi kwenye Qur'an kuwa ni 12 Qur'an 9:32

8. Je unajua kuwa kila unapo paa angani hewa ya oksijen (Oxygen) inapunguwa, na uvutaji wa hewa unakuwa wa shida sana, kiasi ya kwamba kifua kinabana kwa kukosa hewa? Na hii imeandikwa kwenye Qur'an 6:125

9. Je unajua kuwa hata miti ina msujudia Mwenyezi Mungu tena imeelekea kibla?

Angalia picha hapa chini.

10. Je unajua kuwa ukiugeuza mkono wako wa kulia linajiandika neno ALLAH

kwa kiarabu

11. Je unajua kuwa Qur'an 10:92 inatufahamisha kuwa MwenyeziMungu ameahidi kuuifadhi mwili wa *firauni wa enzi ya Nabii Musa (as). Mwili ambao ulikaa zaidi ya miaka 30,000 baharini. Na leo hii hupo huko Misri katika jumba la makumbusho?

*Kadhaalika tujue kuwa kutoka Wana wa Israili katika nchi ya Misri kulikuwa mwishoni mwa karne ya kumi na tatu kabla ya kuzaliwa Nabii Isa a.s., katika enzi ya mmoja wa Mafirauni wa Ukoo wa kumi na tisa, naye ni Minfitah mwana wa Ramsis wa Pili, ambaye ndiye aliye wakandamiza Wana wa Israili akawalazimisha wamjengee Jiji la ufalme wake.

0 comments/Maoni: