Jibu la James John


Ndugu Waislamu Nisaidieni

1) Aya hi 4:101 inawaelekeza waislamu wafanye nini katika vita (Anae kupiga vita ni adui yako, au sio?aya hii haipingani na aya ya 2:109) aya hiyo inasema hivi,

Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi (Quran 4:101).

Na unapo kuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na wachukue silaha zao. Na watakapo maliza sijida zao, basi nawende nyuma yenu, na lije kundi jingine ambalo halijasali, lisali pamoja nawe. Nao wachukue hadhari yao na silaha zao. Walio kufuru wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkawa wagonjwa, mkaziweka silaha zenu. Na chukueni hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha(Quran 102).

Pia aya ya 8:39 ilishuka wakati wa vita (makafiri walikuwa wanawatesa waislamu, Waislamu wanaambiwa wapingane nao (self defence) lakini wakiacha kupigana na nyie na kuwatesa waacheni),

Aya hiyo inasema hivi,

Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda. (Quran 8:39).
Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema (Quran 40).

2) Kuhusu aya ya 47:7

Hiyo ni lugha ya mifano (kama unaijua Biblia vizuri, bila shaka unajua maana ya lugha ya mifano)
Nikisema hivi,

"Mimi sihitaji shilingi elfu kumi zako lakini ukitoa hizo shilingi elfu kumi kwa ajili ya dini yangu (kama vile kusaidia masikini..) nitahakikisha kuwa kweli unanipenda".

Hapa kuna contradiction gani ?

au rafiki yangu mpendwa hajui lugha ya mifano ?

3)  Jiulize kwa nini inchi zote duniani zimeamua kuweka jela ?

Nadhani jawabu unalijua, au sio ?

Kuwaadhibu wahalifu au sio ?

Aya tukufu ya 42:40 inasema hivi,

Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.
4) Jibu la swali lako hili lipo hapo juu (katika jawabu namba moja)

5) Jawabu lako lipo katika aya hii ya Quran Tukufu 2:142,

Quran Tukufu inasema hivi,

WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka (Quran 2:142).

6) Aya hiyo tukufu 4:129,

Inaelezea ukweli wa mwanamme anapo owa wake zaidi ya mmoja (lazima atampenda mmoja zaidi lakini hata hivyo asimili moja kwa moja akamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa, ajaribu kadiri ya uwezo wako kufanya uadilifu).

Aya hiyo inasema hivi,

Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu (Quran 4:129).

7) Haha Haiiii, rafiki mbona unaanza kudanganya sasa, aya ya 16:28 inasema hivi,

Ambao Malaika waliwafisha nao wamejidhulumu nafsi zao! Basi watasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya uovu wowote. (Wataambiwa): Kwani! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyo kuwa mkiyatenda (Quran 16:28).

Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao kiburi! (Quran 16:129)

 Nimekujibu maswali yako yote (Alhamdulillah), na mimi nakuomba unijibu yangu.

1) Nani msemaji katika Biblia ? 
2) Je Biblia yote ni maneno ya Mungu ?
3) Kama Biblia ni maneno ya Mungu kwa nini yanapingana yenyewe kwa yenyewe ? 

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Nasubiri jibu.

Kisha nakuomba unijibu maswali haya,

UTATU
Kwa mujibu wa Wakristo wengi, Yesu amekuwa ni Mungu-mtu, mtu kamili na Mungu kamili. Je, kitu chenye mwisho na kile kisicho na mwisho vinaweza kuwa ni kimoja? Kuwa “Mungu kamili” maana yake ni kutokuwa na mwisho na kutohitajia msaada, na kuwa “mtu kamili” maana yake ni kutokuwa na uungu. 

1. Kuwa mtoto ni kuwa chini ya daraja ya uungu na kuwa na uungu ni kutokuwa mtoto wa yoyote. Vipi Yesu atakuwa na sifa ya utoto na uungu kwa wakati mmoja?

2. Wakristo wanadai kwamba Yesu alidai kuwa yeye ni Mungu wakati walipomnukuu katika Yohana 14:9: “…Aliyeniona mimi amemwona Baba…” Je, Yesu hakusema wazi wazi kwamba: kamwe watu hawakumuuona Mungu, kama inavyosema Yohana 5:37: “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona”?

3. Wakristo wanasema kwamba Yesu alikuwa ni Mungu kwa sababu alikuwa anaitwa mtoto wa Mungu, Mtoto wa mwanadamu, Masiha, na “mwokozi.” Ezekiel aliandikwa katika Biblia kama ni mtoto wa Mungu. Yesu alinena kuhusu “waletao amani” kuwa ni Watoto wa Mungu. Mtu yoyote aliyefuata matakwa na Mipango ya Mungu alikuwa akiitwa MTOTO WA MUNGU katika utamaduni wa Kiyahudi na katika lugha yao (Mwanzo 6:2,4; Kutoka 4:22; Zaburi 2:7, Warumi 8:14) neno “Messiah” ambalo kwa Kiebrania linamaanisha “Mpakwa Mafuta wa Mungu” sio “Kristo”, wala “Cyrus” na mtu huitwa “Messiah” au “mpakwa mafuta”. Ama kuhusu neno “mwokozi” liliopo katika Wafalme wa pili 13:5, watu wengine walipewa jina hilo vile vile bila ya kuwa miuungu. Kwa hivyo, katika maneno hayo uko wapi uthibitisho unaoonesha kuwa Yesu ni Mungu wakati neno mtoto halikutumiwa kwake peke yake?

4. Wakristo wanadai kwamba Yesu alikiri kwamba yeye na Mungu walikuwa ni kitu kimoja kwa maana ya Kimaumbile pale anaposema katika Yohana 10:30; “Mimi na Baba tu umoja.”, Baadae katika Yohana 17:21-23, Yesu alinena kwamba wafuasi wake, yeye mwenyewe na Mungu ni kitu kimoja katika sehemu tano. Sasa kwa nini walipe neno “Kitu kimoja” la kwanza maana nyingine tofauti na yale maneno “kitu kimoja” katika sehemu tano nyinginezo?

5. Je, Mungu ni watatu-katika-mmoja na ni mmoja katika watatu kwa wakati mmoja au ni mmoja kwa wakati huo huo?

6. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, kwa hiyo hakuna hata mmoja kati ya hao watatu ambae ni Mungu kamili. Tukikubali kwamba huo ndio ukweli, sasa je, wakati Yesu alipokuwa duniani, hakuwa Mungu kamili, wala “Baba aliyembinguni” hakuwa Mungu kamili. Je, hilo halileti mkanganyiko kwa kile alichokuwa akikisema Yesu kila siku kuhusu Mungu wake na Mungu wetu aliyembinguni, Bwana wake na Bwana wetu? Je, hilo vile vile halimaanishi kwamba hakukuwa na Mungu kamili, katika kipindi cha kati ya dai la kusulubiwa na dai la kufufuka?

7. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, sasa nani aliyekuwa Mungu huko mbinguni wakati Yesu alipokuwa aridhini? Je, hili halileti mkanganyiko na yale aliyokuwa akiyasema mara nyingi juu ya kuwa Mungu aliyembinguni ndiye aliyemtuma?

8. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, je, nani aliyekuwa Mungu huko mbinguni katika zile siku tatu zilizo kati ya dai la kusulubiwa na dai la kufufuka? 

9. Wakristo husema kwamba: “Baba (B) ni Mungu, Mwana (M) ni Mungu na Roho Mtakatifu (R) ni Mungu, lakini Baba si mwana, na Mwana si Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu si Baba”. Kwa hesabu rahisi na kwa kanuni inakuwa hivi, ikiwa B = G, M = G na R = G; kwa kufuatanisha inakuwa B = M = R, wakati sehemu ya pili ya maelezo hayo inaonesha kuwa B№ M№ R (inamaanisha haziko sawa). “Sasa je, huo si mkanganyiko na imani ya Wakristo juu ya utatu wenyewe?

10. Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, kwa nini alimwambia yule mtu aliemwita Yesu “Bwana Mwema” alimwambia asimwite “mwema” kwa sababu hakuna mwema ila Mungu wake aliyembinguni peke yake? 

11. Kwanini Wakristo wanasema kwamba Mungu ni watatu katika mmoja na mmoja katika watatu, wakati Yesu alisema katika Marko 12:29. “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” kama ilivyo katika sehemu nyingi ndani ya Biblia.

12. Ikiwa kuamini utatu lilikuwa ni jambo la lazima ili uwe Mkristo, kwa nini Yesu hakulifundisha na wala hakulisisitiza jambo hilo kwa Wakristo katika zama zake? Je, vipi hao wafuasi wa Yesu wachukuliwe kuwa ni Wakristo bila ya kulisikia neno utatu? Kama ingekuwa utatu ndio uti wa mgongo wa Ukristo, Yesu angeliufundisha na angeliusisitizia na angeliufafanua kwa watu wake kikamilifu.

13. Wakristo wanadai kwamba Yesu alikuwa Mungu kama walivyomnukuu katika Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”. Hayo ni maneno ya Yohana na si maneno ya Yesu, vile vile, neno la kwanza la Kigiriki kwa ajili ya Mungu ni “HOTHEOS” ambalo linamaanisha “Mungu” likiwa na M kubwa, wakati neno la pili la Kigiriki kwa ajili ya Mungu ni “TONTHEOS” ambalo linamaanisha “mungu” likiwa na “m” ndogo. Je, huko si kukosa uaminifu kwa wale waliotafsiri Biblia ya Kigiriki? Je, nukuu hiyo ya Yohana 1:1 iliyotambuliwa na kila mwanazuoni wa Kikristo aliyeisoma Biblia kwamba imeandikwa na Myahudi aitwae Philo Alexandria kabla ya Yesu na Yohana?

14. Je, neno “god” au “TONTHEOS” pia halikutumika kuashiria wengine kama ilivyo katika Wakorinto 2 4:4 (Na Shetani ndie) mungu wa ulimwengu huu na katika Kutoka 7:1 “Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; ?

WOKOVU:

Wakristo wanasema kwamba “MUNGU AEMTOA” mwanawe wa pekee ili kutuokoa sisi”. Je, Mungu alimtoa Yesu kumpa nani wakati yeye Mungu ndiye mmiliki wa ulimwengu wote?

15. Ikiwa ilikubalika kwa utukufu wa Mungu kuwa awe na watoto, basi angeumba mamilioni ya watoto kama Yesu. Sasa kuna jambo gani kubwa kumhusu huyu mtoto wa pekee?

16. Kwa nini Biblia inasema kwamba Yesu alitaka kufa msalabani, huku yule mtu aliyesulubiwa pale msalabani alikuwa anapiga kelele “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” kwa mujibu wa Matayo 27:45 na Marko 15:33?

17. Ikiwa Mungu alitaka kutuokoa, Je, angeshindwa kutuokoa bila kumtoa muhanga Yesu?

18. Mungu yeye mwenyewe ni haki, na haki inataka kusiwepo na mtu anayepaswa kuadhibiwa kwa madhambi ya wengine, vile vile haipaswi kuadhibiwa watu wengine kwa kuwaokoa wengine: Je! Dai la kwamba Mungu amemtoa muhanga Yesu ili kutuokoa haliteti mkanganyiko kama kweli Mungu ni mpenda haki? Je, Dai hilo halitofautiani na maana halisi ya haki?

19. Watu wanatoa muhanga vitu vyao ili kupata vitu vingine wasivyokuwa navyo ikiwa haiwezekani kuwa navyo vyote viwili kwa wakati mmoja. Wakristo wanasema kwamba “Mungu alimtoa muhanga mtoto wake wa pekee ili kutuokoa; Tunajua kwamba Mungu ni Mwenye nguvu; Mungu alimtoa Muhanga Yesu kwa nani?

20. Kutoa muhanga kitu maana yake ni kwamba huwezi kukipata tena kile ulichokitoa; sasa kuna siri gani katika kutolewa Muhanga Yesu wakati Mungu aliweza kumrudisha Yesu baada ya kusulubiwa (kwa mujibu wa maneno ya Wakristo)?

21. Ikiwa Wakristo wote wameokoka kwa kupitia Yesu na wanakwenda Peponi (kwenye uzima wa milele) bila kujali matendo yao, kwa hiyo mafundisho ya Yesu hayana umuhimu wowote na maana ya maneno “uovu” au “wema” hayana umuhimu wowote. Ikiwa hali sivyo hivyo, kwa hiyo wale Wakristo ambao wanamwamini Yesu lakini hawafuati mafundisho yake wala hawajatubu watakwenda motoni?

22. Vipi Wakristo wanayachukulia matendo kama kitu kisicho na umuhimu baada ya kuwa kitu kimoja wakati Yesu aliposema katika Matayo 12:36; “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.”?

23. Wakristo wanasema kwamba watu wanakwenda Peponi kwa kupitia Yesu tu! Wakati Paulo anasema katika 1 Wakorintho 7:8-16 kwamba Mume asieamini anakubalika kwa Mungu kwa sababu anaunganishwa na mke wake na kinyume chake, na watoto wao wasio na dini vile vile wanakubalika kwa Mungu. Kwa hivyo kumbe watu wanaweza kwenda Peponi bila ya kumwamini Yesu; kutokana na maneno hayo.

24. Vipi Biblia inasema kwamba Waisraeli wote wameokoka ingawa hawamwamini Yesu? Je, Hili halipingani na dai la Biblia ya kuwa njia ya pekee ya kwenda Peponi ni kwa kupitia Yesu tu?

25. Kwa mujibu wa Wakristo, wale wote ambao hawakubatizwa watakwenda motoni. Kwa hivyo hata watoto wachanga nao watakwenda motoni kwa vile walikufa kabla ya kubatizwa; kwa vile walizaliwa na dhambi la asili la kurithi? Je, hili halipingani na maana ya neno haki; kwanini Mungu awaadhibu watu kwa madhambi wasiyoyatenda?

ROHO MTAKATIFU

Sehemu pekee katika Biblia alipotajwa Roho Mtakatifu ni katika Yohana 14:26; “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia. “Ni kipi kile ambacho Roho Mtakatifu ameleta au kufundisha kwa miaka 2000 iliyopita?

26. Wakristo wanasema kwamba Msaidizi maana yake ni Roho Mtakatifu (Yohana 14:26) Yesu alisema katika Yohana 16:7-8. “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu;” Hii haiwezi kumaanisha Roho Mtakatifu; kwa vile Roho Mtakatifu inasemekana kwamba alikuwepo hata kabla ya Yesu hajazaliwa kama ilivyo katika Luka 1:41 “Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu”. Hapa, Roho Mtakatifu vile vile alikuwepo wakati wa Yesu: sasa vipi hii imaanishe kwamba ni sharti aondoke Yesu ndipo Roho Mtakatifu aweze kuja?

27. Katika Yohana 16:7-8, inasema; “Bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” Je, hii “Yeye” hapa inamaanisha nini? Je, viwakilishi hivyo havimaanishi mtu mwanamume? 

28. Je, Roho Mtakatifu anazungumza na Wakristo wema na waovu vile vile? Je, Roho Mtakatifu yu pamoja nao wakati wote au wakati fulani tu? Je, ni wakati gani anaanza kumtembelea mtu atakaye kuwa Mkristo?

29. Utasemaje kuwa wewe ni Mkristo ikiwa Roho Mtakatifu yu ndani ya Mkristo mwingine? Inakuwaje Wakristo wengi wanawapumbaza watu kwa kudai kwamba Roho Mtakatifu yu ndani yao tu! Na baadaye wanabadilisha dini?

30. Je, Roho Mtakatifu anaamuru kile ambacho Wakristo wanapaswa kukifanya bila ya uhuru wa kuchagua hata kidogo au anawaongoza tu na wao wana uhuru wa kufuata au kuto fuata?
31. Ikiwa Roho Mtakatifu anaamuru kile Wakristo wanachopaswa kukifanya, kwa nini Wakristo wanafanya maovu na madhambi? Vipi unaweza kuuelezea ubadilishaji wa dini na kuingia dini na imani mbali mbali kunakofanywa na Wakristo wengi? Je, Wanaambiwa kufanya hayo na Roho Mtakatifu? 

32. Ikiwa Roho Mtakatifu anawaongoza Wakristo tu, na wako huru kufanya wanavyotaka, sasa ni vipi tutajua kwamba waandishi wa Biblia hawakufanya makosa wakati walipoziandika?
33. Ikiwa Wakristo wanaamini kwamba Roho Mtakatifu huwajia na kuzungumza nao kila siku, kwanini hawamuulizi Roho Mtakatifu kuhusu chapisho lipi la Biblia wanalopaswa kulifuata kwa vile kuna machapisho mengi?

KAZI YA UJUMBE WA YESU Hivi bila ya kuazima kutoka katika dini na mifumo mingine, Ukristo unaweza kuwapa wanadamu mfumo kamili wa maisha? Huku Ukristo ukiwa umefungika kwa maisha ya kiroho tu na hautoi sheria, sasa vipi jamii itaweza kuamua sheria zipi ni sahihi na zipi ni makosa?

34. Kwa nini Wakristo wanasema kwamba Yesu alikuja kwa ajili ya ulimwengu mzima wakati yeye alisema kuwa alitumwa kwa Mayahudi tu? Alimwambia yule mwanamke Mkananayo aliyemuomba amtibie bintiye aliyekuwa anasumbuliwa na mapepo: “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” na pia alisema; Si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” (Matayo 15:21-28).

KUFUFUKA KWA YESU Ikiwa utasoma Matayo (28: 1-10), Marko (16:1-20), Luka (24:1-12), na Yohana (20:1-18) utakuta habari zenye kutatanisha: Maandika yote hayo yanakubali kwamba kaburi lilikuwa linalindwa kwa muda wa siku tatu. Hata hivyo, maandiko hayo yanaonesha kugunduliwa kwa kaburi kuwa ni tupu katika hali tofauti. 

1 Matayo (28) na Yohana (20) zinaeleza kwamba Maria Magdalena na Maria wengine walikuwa ndio watu wa kwanza kuliona lile kaburi.

2 Marko (16) inaeleza kwamba Maria Magdalena, Maria mama, James na Salome walikuwa wa kwanza kuliona kaburi likiwa tupu.

3 Marko (28) inaeleza kwamba kulikuwa na tetemeko la ardhi ambalo lililoondosha jiwe lililokuwa juu ya kaburi. Anasema kwamba Malaika ndie aliesababisha hivyo: Maandiko mengine hayataji kuwepo kwa tetemeko la ardhi. 

4 Matayo na Marko wanasema kwamba mwanamume mmoja tu aliyevaa mavazi meupe ndiye alikuwa malaika.

5 Luka inasema wanamume wawili waliovalia mavazi meupe, ambao walikuwa malaika, ndio waliokuwa wamekaa juu ya kaburi. Yohana inasema kwamba wale wanawake wawili hawakumkuta mtu yoyote kwa mara ya kwanza walivyokwenda kwenye kaburi, lakini waliporudi tena, waliwaona watu wawili, mmoja alikuwa Malaika na mwingine alikuwa Yesu.

6 Matayo inasema kwamba, wakati walinzi walipotoa taarifa hizi kwa Kuhani mkuu, yule Kuhani mkuu aliwalipa kiasi kikubwa cha pesa, na kuwaambia “Mnapaswa kusema kwamba wafuasi wake walikuja nyakati za usiku na kuiba mwili wake”. Alidai kwamba askari walichukua pesa na kusambaza habari hiyo na toka hapo, hadithi ilikuwa ni yenye kuzunguka kati ya Wayahudi; mpaka leo (kwa mujibu wa Matayo). Maandiko mengine hayasemi chochote kuhusu jambo hilo. 

35. Ni maelezo yapi ambayo ni ya kweli?

36. Kwa nini Yesu alipojitokeza baada ya tendo la kusulubiwa inachukuliwa kama ndio kigezo (uthibitisho) wa kufufuka kwake wakati kuna maelezo yasemayo kwamba si yeye aliyesulubiwa wala aliyekufa kwani aliyesulubiwa ni mtu mwingine wakati Mungu akimwokoa Yesu?
37. Vipi Matayo alijua dai au hoja ya makubaliano kati ya wale askari na yule kiongozi? Hivi mtu hawezi kusema kwamba kuna mtu aliyewalipa wale wanawake kiasi kikubwa cha pesa na akawaambia waeneze maneno yale ya kwamba Yesu alifufuka, pamoja na uthabiti huo huo kama ule wa habari ya Matayo.

38. Kwanini walimwamini yule mtu aliekuwa na mavazi meupe? Kwa nini walimuamini kwamba alikuwa ni malaika? Maelezo ya Yohana ni ya kustaajabisha sana, kwa vile yeye alisema kuwa Maria hakumtambua Yesu (ni yupi kati ya wale watu wawili) wakati alipokuwa akizungumza nae, hali alimtambua tu wakati yule mtu alipomwita Maria kwa jina lake?

39. Vipi lile kaburi lililokuwa tupu lina thibitisha kwamba Yesu alisulubiwa? Je, Mungu hawezi kumtoa mtu mwingine kutoka kaburini na kumfufua?

40. Injili inaaminiwa kuwa ni maneno asilia ya Mungu, yanasadikiwa kwamba yalisemwa na Roho Mtakatifu kwa wafuasi wake ambao waliyaandika. Ikiwa chanzo chake ni kimoja, kwanini yasilingane katika kulizungumzia tukio lile muhimu? (la kufufu Yesu).

41. Vipi Matayo, Marko, Luka na Yohana waliweza kuchukuliwa kama mashahidi walioona Yesu akifufuka wakati Biblia inatuambia kwamba hakuna mtu aliyemuona Yesu akitoka ndani ya kaburi?
BIBLIA Ikiwa Wakristo wanachukulia Agano la Kale kwamba ni maneno ya Mungu, kwa nini walibatilisha baadhi ya maandiko katika Agano la Kale ambayo yalikuwa yakizungumzia adhabu (kwa mfano adhabu ya uzinzi)?

42. Kwanini Marko 16:9-20 haipo kwenye machapisho mengi ya Biblia wakati katika baadhi ya machapisho imejitokeza kama tanbihi ya chini ya ukurasa tu au imewekwa katika mabano? Je, tanbihi ya chini ya ukurasa katika Biblia nayo inachukuliwa kuwa ni maneno ya Mungu, hasa hasa wakati inapozungumzia jambo muhimu kama la kupaa kwa Yesu?

43. Kwa nini Biblia ya Kikatoliki ina vitabu 73 ndani yake wakati Biblia ya Kiprotestanti ina vitabu 66 tu ndani yake? Wakati zote mbili ya Kikatoliki na Kiprotestanti zinadai kuwa na maneno kamili ya Mungu, ipi inatakiwa iaminiwe na kwa nini; kwa kigezo gani?

44. Ni wapi zinakotoka hizo tafsiri mpya za Biblia wakati ile Biblia ya asili haipo au haipatikani popote? Maandiko ya kizamani ya Kigiriki ambayo yenyewe ni tafsiri hayafanani na yanatofautiana yenyewe kwa yenyewe.

45. Unawezaje kuyachukua maandiko ya waandishi ambao kamwe hawakumuona Yesu kwamba ni sahihi, kama vile Marko na Luka?

46. Kwa nini nusu ya Agano Jipya imeandikwa na mtu ambae kamwe hakuonana na Yesu katika maisha yake? Paulo anadai alionana na Yesu alipokuwa njiani toka Jerusalemu kuelekea Damaskasi bila kutoa ushahidi wowote wa kuonana naye? Paulo alikuwa ndie adui mkubwa wa Ukristo; Je, hilo halitoshi kutilia shaka juu ya usahihi wa kile alichokiandika? Kwa nini Wakristo wanayaita maandiko ya vitabu hivyo vya Agano la Kale kwamba ni “MANENO YA MUNGU” wakati wale waliyoyapitia Biblia ya RSV wanasema kwamba mwandishi wa SAMWELI hajulikani na yule alieandika (na kuyakusanya) maandishi ya kale (KUMBU KUMBU) “HAJULIKANI HUENDA YALIKUSANYWA NA KUHARIRIWA NA EZRA”.!!!
UTATA

47. Kulingana na mambo yanayotatanisha katika Biblia, ni vipi Wakristo wanaweza kuamua kwa wingi wa theluthi mbili yapi ni maneno ya Mungu na yapi si maneno ya Mungu kama tangulizi ya baadhi ya Biblia zinavyosema kama ilivyosema ile ya RSV?

48. Kwanini Luka katika maandiko yake anazungumzia kupaa kwa Yesu kuwa ilikuwa ni siku ya Pasaka, na katika Matendo ya Mitume, maandiko ambayo yanajulikana kama yeye ndiye mwandishi, anasema alipaa siku arobaini baadae?

49. Ukoo wa Yesu umetajwa katika Matayo na Luka tu. Matayo iliorodhesha vizazi 26 kutoka Joseph hadi Daudi wakati Luka yeye iliorodhesha vizazi 41. ni Joseph tu anayeungana na Daudi katika orodha zote mbili. Hakuna jina jingine hata moja lingana! Ikiwa hayo yalitolewa na Mungu neno kwa neno, vipi yatofautiane? Baadhi wanadai kwamba moja ni kwa ajili ya Maria na moja ni kwa ya Joseph, lakini ni wapi alipotajwa Maria katika maandiko yote mawili?

50. Ikiwa Musa aliandika vitabu vya kwanza kabisa vya Agano la Kale, Musa aliwezaje kuandika taarifa ya kifo chake mwenyewe? Musa alikufa katika kitabu cha tano akiwa na miaka 120 kama ilivyotajwa katika Kumbukumbu la Torati; 34:5-10

51. Katika chapisho la King James, kwa nini linaeleza miaka 7 (saba) ya ukame katika Samweli 2 24:13 huku likieleza miaka 3 (mitatu) tu ya ukame katika Mambo ya Nyakati 1- 21:12? Kwa nini yote yalibadilika katika chapisho jipya la kimataifa na machapisho mengine?

52. Vile vile Katika chapisho la King James, kwa nini inasema kwamba JEHOIACHINI alikuwa na miaka minane wakati alipoanza kuongoza katika Mambo ya Nyakati 2 (21:12) huku ikisema alikuwa na miaka kumi na nane katika Wafalme 2 24:8? Kwa nini baadae zote zilibadilika na kuwa 18 katika chapisho jipya?

53. Katika machapisho yote, kwa nini yanasema kwamba Daudi aliwauwa waendesha magari ya Farasi MIA SABA wa Kisyria na wapanda farasi arobaini elfu kama ilivyooneshwa katika Samweli 2 10:18 huku ikisema watu elfu saba ambao walipigana kupitia magari ya farasi na wapiganaji wa miguu 40 elfu katika Mambo ya Nyakati 1 19:18?

54. Katika machapisho yote, kwa nini yanasema kuwa majosho elfu mbili katika Wafalme 1 7:26 huku katika Mambo ya Nyakati 2 4:5 linasema ni majosho elfu tatu?

55. Katika chapisho la King James, kwa nini linasema kwamba Solomoni alikuwa na vikalio vya farasi elfu nne katika Mambo ya Nyakati 2 9:25, huku likisema kwamba Solomoni alikuwa na vikalio vya farasi arobaini elfu katika Wafalme 1 4:26? Kwa nini yalibadilika yote mawili na kuwa arobaini elfu Katika chapisho jipya?

56. Mwanzo 1, uumbaji wa Mungu umeanzia majani kisha miti, ndege, nyangumi, ng`ombe na vitambaavyo na mwisho mwanamume na mwanamke. Mwanzo 2, hata hivyo, inauweka uumbwaji wa mwanamume kabla ya ng`ombe na ndege na mwanamke. Baadaye na wanyama. Vipi itawezekana kufafanua haya?

QURAN NA WAKRISTO
Ketengo hiki hakihitaji wala hakihoji, lakini sana sana kunampatia msomaji baadhi ya aya za Quran ambazo zinauelekeza Ukristo kwa upekee, na watu wa kitabu kwa ujumla. Sehemu kubwa ya Quran inahusika na au inafungamana na Wakristo na Wayahudi na nimeamua kuchagua aya zinazofungamana na maudhui ya makala hii. 

1 “Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; Alimuumba kwa udongo kisha Akamwambia: “Kuwa”; basi akawa.” (Quran 3:59)

2 “Sema: “Enyi watu mliopewa Kitabu (cha Mwenyezi Mungu. Mayahudi na Manasara)! Njooni katika neno lilio sawa baina yetu na baina yenu: ya kwamba tusimwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe (Mwenyezi Mungu) na chochote; wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu (au pamoja na Mwenyezi Mungu). Wakikengeuka, semeni: “Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu, (tumenyenyekea amri za Mwenyezi Mungu).”

3 “Enyi watu mliopewa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahimu, na hali Taurati na Injili havikuteremshwa ila baada yake? Basi je, hamfahamu?” 

4 “Ibrahimu hakuwa Myahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu, mtii; wala hakuwa katika washirikina.” 

5 “Watu wanaomkurubia zaidi Ibrahimu ni wale waliomfuata yeye (katika zama zake) na Mtume huyu 
(Muhammad) na waliomwamini (Mtume huyu). Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa wenye kuamini.” 

6 “Baadhi ya watu waliopewa Kitabu wanapenda wakupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao; na (hali wenyewe) hawatambui.” 

7 Enyi mliopewa Kitabu! Mbona mnazikataa Aya za Mwenyezi Mungu, hali mnajua (kuwa ndiyo ndizo)?

8 Enyi mliopewa Kitabu! Mbona mnachanganya haki na batili, na mnaficha haki, hali mnajua?” (Quran 3:64-71)

9 “Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).” (Quran 3:85)

10 “Na kwa (ajili ya) kusema kwao: “Sisi tumemuua Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mungu,” hali hawakumwua wala hawakumsulubu, bali walibabaishiwa (mtu mwengine wakamdhani Nabii Isa). Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika) hiyo (ya kumwua nabii Isa)wamo katika shaka nalo (jambo hilo la kusema kauawa). Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa kweli wamemwua Nabii isa), ispokuwa wanafuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumwua. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua Kwake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima.” (Quran 4:157-158).

11 “Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na (ni kiumbe aliyeumbwa kwa) tamko Lake (tu Mwenyezi Mungu) alipompelekea Maryamu. Na ni roho iliyotoka Kwake (Mwenyezi Mungu kama roho nyengine). Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mitume Yake; wala msiseme “watatu …” Jizuieni (na itikadi hiyo); itakuwa bora kwenu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mungu Mmoja tu. Ni mbali na Utakatifu Wake kuwa ana mwana. Ni vyake (vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini; na Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa kutosha. Masihi (Nabii Isa) hataona unyonge kuwa mja wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika waliokurubishwa (na Mwenyezi Mungu hawataona unyonge kuwa waja wa Mwenyezi Mungu). Na watakaoona unyonge uja wa Mungu na kutakabari, basi Atawakusanya wote Kwake (Awatie Motoni). Na ama wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, basi Atawapa ujira wao (sawa sawa), na kuwazidishia fadhila zake. Lakini wale walioona unyonge na kufanya kiburi, basi Atawaadhibu kwa adhabu iumizayo, wala hawatapata rafiki wala msaidizi (yoyote) mbele ya Mwenyezi Mungu. (Quran 4:171-173) 

12 “Na kwa wale waliosema: “Sisi ni Wakristo,” Tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa, kwa hivyo Tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na bughudha mpaka Siku ya Kiama. Na Mwenyezi Mungu atawaambia walivyokuwa wakiyafanya. Enyi watu wa Kitabu! Amekwisha kufikieni Mtume wetu, anayekudhihirishieni mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na husamehe mengi. Bila shaka imekwisha kufikieni nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Kitabu kinachobainisha (kila jambo). Kwa (Kitabu) hicho Mwenyezi Mungu huwaongoza wenye kufuata radhi Yake katika njia za salama, na huwatoa katika kiza kuwapeleka katika nuru kwa amri Yake, na Huwaongoza katika njia iliyonyooka. Kwa yakini wamekwisha kufuru wale waliosema: “Mwenyezi Mungu ni Masihi bin Maryamu.” Sema: “Ni nani atakayemiliki (kuzuilia) chochote mbele ya Mwenyezi Mungu kama Yeye angetaka kumwangamiza Masihi mtoto wa Maryamu, na mama yake na vyote vilivyomo katika ardhi?” Na ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake ni wa Mwenyezi Mungu (tu peke yake). Huumba Apendavyo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.” (Quran 5:14-17) 

13 “Bila shaka wamekufuru wale waliosema, “Mwenyezi Mungu ni Masihi (isa) bin Maryamu.” Na (hali ya kuwa) Masihi alisema: “Enyi wana wa Israili! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia Siku ya Kiama).”

14 Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Mwenyezi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu; (Yeye ndiye wa tatu wao).” Hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja (tu peke yake). Na kama hawataacha hayo wayasemayo, kwa yakini itawakamata – wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao – adhabu iumizayo.

15 Je! Hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba msamaha? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.

16 Masihi bin Maryamu si chochote ila ni Mtume (tu). (Na) bila shaka Mitume wengi wamepita kabla yake. (Hawajaona)? Na mamake ni mwanamke mkweli. (Na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na wakenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo)? Tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).

17 Sema: “Je! Mnawaabudu – badala ya Mwenyezi Mungu (peke yake) – wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukunufaisheni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Asikiaye (na) ndiye Ajuaye.”
18 Sema: “Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu bila haki, wala msifuate matamanio ya watu waliokwisha potea toka zamani; (nao ndio hao wanavyuoni wenu) na wakawapoteza wengi, na (sasa) wanapotea njia iliyo sawa, (hawataki kumfuata Nabii Muhammad).” (Quran 5:72-77) 

19 Na (kumbukeni) Mwenyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryamu! Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu?” aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika. Hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uwongo). Kama ningalisema bila shaka Ungalijua; Unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyo nafsini Mwako; hakika Wewe ndiye Ujuaye mambo ya ghaibu.

20 “Sikuwaambia lolote ila yale Uliyoniamrisha: ya kwamba, ‘Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu.’ Na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao; na Uliponikamilishia muda wangu, Wewe ukawa Mchungaji juu yao, na Wewe ni Shahidi juu ya kila kitu.

21 Ikiwa Utawaadhibu, basi bila shaka hao ni waja wako; na Ukiwasamehe basi kwa hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima; (Hutaambiwa kuwa wamekushinda kuwatia adabu).”

22 Mwenyezi Mungu atasema: “Hii ndiyo Siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele. Mwenyezi Mungu amewawia (amewapa) radhi; nao wawe radhi Naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa.” (Quran 5:116-119) 

23 Na Mayahudi wanasema: “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;” na Wakristo wanasema: “Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu”; haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale walio kufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

24 Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na (wamemfanya) Masihi mwana wa Maryamu (pia mungu), hali hawakuamrishwa ispokuwa kumuabudu Mungu Mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Yeye. Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo.

25 Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa ispokuwa kuitimiza nuru Yake, ijapokuwa makafiri wanachukia.
26 Yeye ndiye Aliyemleta Mtume Wake kwa uongofu na Dini ya haki ili Aijaalie kushinda (Dini hii) dini zote; ijapokuwa watachukia hao washirikina.

27 Enyi mlioamini! Wengi katika makasisi (wanavyuoni wa Mayahudi na Manasara) na watawa (wao) wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inayoumiza (inayowangoja)

28 Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika Moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambiwa): “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya.” (Quran 9:30-35)

MUHAMMAD AU YESU? Wakristo wanadai kwamba utabiri wa Kumbukumbu la Torati 18:18 unamuhusu Yesu na sio Muhammad. Hiyo aya inasema: "Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.” Kumbukumbu la Torati 18-18 Hoja ya pekee wanayoikimbilia katika tafsiri hiyo ni kuwa wote wawili Musa na Yesu walikuwa Mitume. Ingawa hoja hiyo inapingana na madai yao ya kuwa Yesu alikuwa ni Mungu na si Mtume. Mitume wengi wa Kiyahudi walifanana na Musa. Hata hivyo, kama tutamlinganisha Muhammad na Musa, tupata kuwa: 

Muhammad alikuwa ni Mwarabu, na Waarabu wanatokana na Ismaili, mtoto wa Ibrahimu, huku Musa alikuwa ni Myahudi, na Wayahudi wanatokana na Isaka, mtoto wa Ibrahimu, kwa kuwa neno NDUGU ZAO linaashiria watoto wa mtoto wa kwanza kuwa ndugu wa mwingine. Hili halikubaliki kwa Yesu, kwa kuwa alikuwa ni Myahudi.

Kwa mujibu wa Wakristo, Yesu alienda Motoni kwa siku tatu huku Musa akiwa hajaenda. Kwa hiyo, Yesu si kama Musa. (Katika Uislamu, hakuna yoyote katika hao Manabii watatu aliyeingia Motoni)
Musa na Muhammad walizaliwa na baba na mama huku Yesu alizaliwa na mama tu.

Musa na Muhammad walioa na kuwa na watoto, huku Yesu akiwa hajaoa kabisa.
Musa na Muhammad walipata matatizo na mambo magumu kutoka kwa watu wao mara ya kwanza, lakini mwishoni walikubaliwa na watu wao. Huku Yesu alikuwa amekataliwa na watu wake mwanzoni na anaendelea kukataliwa na Wayahudi hadi leo hii. “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” Yohana 1:11

Musa na Muhammad walikuwa na nguvu, kando na kuwa Mitume. Wote wawili walitekeleza adhabu kubwa, hilo likiwa ni mfano, huku Yesu hakuwa na madaraka kwa watu wake. “Yesu akajibu, ufalme wangu sio wa ulimwengu huu”, Yesu amesema katika 18:36.

Musa na Muhammad walileta sheria mpya huku Yesu hakuleta.

Musa alilazimishwa kuhama alipokuwa mkubwa aende Median huku Muhammad pia, alilazimishwa ahame alipokuwa katika hatua moja ya maisha yake, kuelekea Madina. Huku Yesu hajalazimishwa kuhama katika utuuzima wake.

Musa na Muhammad wote wawili walikufa vifo vya kawaida na kisha wote walizikwa, huku jambo hilo haliwezi kuongelewa kwa Yesu. Yesu hakuuliwa wala hakusulubiwa kabisa kabisa, kwa mujibu wa Quran na hakufa kwa kifo cha kawaida kama ilivyothibitishwa na Wakristo ambao wanaamini kasulubiwa.

MASWALI YA MWISHO

57. Kwa nini, ewe kiongozi wa Kikristo, huji kusikiliza na kujifunza dini ya kweli ya Yesu?
58. Ukiwa kama Mkristo, uliyeusoma Uislamu na ikiwa ni hivyo, je, uliusoma kutoka kwa Waislamu wa kweli?

59. Kama Mkristo, je, unakubali kwa uadilifu na wema kuwa ni lazima uchunguze kile kinachosemwa na Uislamu juu ya Mungu, Yesu, pamoja na maisha haya na ya baadae?

60. Kwa kuwa ni Mkristo, je, pia, waamini kile tunacholazimika kuhesabiwa kwa Muumba wetu na kwamba Muumba ni mkamilifu na Muadilifu? Kama muumini mwaminifu kwa Mungu. Je, hulazimiki kutafuta ukweli usiobadilishwa bilia kujali matokeo yake?


___


Kwa msaada mkubwa kutoka kwa BrotherSekenke Blog


0 comments/Maoni: