Biblia Na Mwenyezi Mungu

Maelezo yafuatayo ni kuhusu waandishi wa Biblia jinsi walivyokuwa na mawazo ya kipagani kuhusu Mwenyezi Mungu. Kiasi gani Biblia imetopewa kwa maovu na uwongo kuhusu Mwenyezi Mungu aliyeumba Ulimwengu!!?

Biblia inasema vitu ambavyo haviingii hakilini hata kidogo juu ya Utukufu wa Mwenyezi Mungu. Na kuhusu M’Mungu kuitwa baba kwenye bibilia haya ni mambo ya dini za kale za kipagani. Dini zilizokuwepo kabla ya ukristo. Na inajulikana kuwa ukristo umerithi mambo mengi toka dini hizi za kipagani hususani dini iliyokuwa ikiaminiwa Iran (Mithraism). Dini hii imeathiri mambo mengi sana ktk ukristo. Mfano mmoja wapo ni huku kumwita M’Mungu baba pamoja na kumpa mwana. Kitu ambacho M’Mungu ameepukana nacho.

Hata hizo version za bible ambazo zipo zaidi ya 100, zinapingana zenyewe kwa zenyewe. Zipo zinazomwita Jesus as only son na zipo zinazomwita as only begotten son John 3:16. Only son or only begotten son?
Nukuu kutokaKJV na RS).


Na hata huku kuwaitwa mapadri na makasisi kuwa ni mababa ni mila za kipagani. Mithraic bishops walikuwa wakiitwa Pater yaani Father. Na hata huko kuvaa kwao mitre (a liturgical headdress worn by bishops and abbots. neno ambalo limetokana na mithra) na kubeba shephrd’s staff na hiki cheo cha kuitwa Ponifex maximus, ambacho ndo cheo cha papa hata leo ni mila za kipagani.

Hawa Wamithra walikuwa na tambiko (sakramenti) saba; muhimu kabisa katika hizo ni ubatizo, na Ekaristi (Misa), ambapo hao washirika hula mkate na hunywa mvinyo, kwa kuwa ndio wanakula nyama ya Mithra, na kunywa damu yake.

Bwana Paulo alifundisha ibada hiyo (ya kuua wana) akiunga mkono dhana ya kuuliwa mwana wa Mariamu kama kafara ya dhambi za Wakristo wote.

Sambamba na mafundisho hayo ya Bwana Paulo juu ya ibada hiyo (kuua wana) waandishi wa agano jipya kwa kuwa nao walidhamiria kuuandikia Ukristo wa Paulo, kama ilivyo kazi yao (kusherehesha mafundisho ya Paulo) katika kusherehesha ibada hiyo kama ilivyofundishwa na "mwalimu wao" Bwana Paulo, katika Injili zao na nyaraka zao wamediriki hata kupenyeza maneno kinywani mwa Bwana Yesu (a.s.) wakisimulia kuwa Yesu mwenyewe (a.s.) ati aliwahi kutabiri kuuliwa kwake msalabani (Tazama Mathayo 12:40, 20:17-19; Marko 10:32-34; Luka 18:31-33 na kadhalika)!

Nasema waandishi hao wamepenyeza ibada hiyo (ya kuua wana) kinywani mwa Yesu (a.s.) kwa sababu siyo wao tu, bali hata 'mwalimu wao' Bwana Paulo anajua wazi kuwa Bwana Yesu (a.s.) kamwe hawezi akathubutu kufundisha ibada potofu za watu wa mataifa, yaani wapagani, zilizokemewa vikali na M’Mungu.

Kwa upande mwingine, kutokana na mafundisho hayo ya Paulo yanayounga mkono ibada hiyo ya wapagani (ya kuuwa wana), katika kuunga kwao mkono na kutilia mkazo mafundisho hayo (ya Paulo), Wakristo pia wameibua kitu kiitwacho "Ekaristi takatifu", "Chakula cha Bwana", "Meza ya Bwana" na kadhalika. Hapo ula mikate na kunywa divai wakiashiria kuula mwili wa Yesu (a.s.) na kuinywa damu yake wakijifariji kwa dhana ya kuuliwa mwana wa Mariamu! Sambamba na hilo, pia wamezua "sikukuu ya Pasaka ya Yesu" kama kumbukumbu ya kutukuza dhana ya kuuliwa mwana huyo wa Mariamu kama kafara ya dhambi zao! Kwa ujumla, ibada hiyo ya kipagani inaungwa mkono mia kwa mia na dini ya Kikristo.

Upagani wao pia hudhirika pale dini hiyo (ya Kikristo) inapowafundisha waumini wake kutumia sehemu ya sala zao kuwaomba watakatifu wao waliokufa! Kwa mfano, Wakristo wanayo sala maalum ya kumwomba Bikira Mariamu ambaye inafahamika wazi kuwa mtu huyo kishakufa tokea zamani. Mfano wa sala yao hiyo ni kama ile wasemayo:

"Kumbuka, ee Bikira Maria mpole sana, haijasikika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, aliyeomba msaada na maombezi yako. Kwa matumaini hayo, nakukimbilia, ee Mama, Mkuu wa mabikira, Ninakuja kwako, nasimama mbele yako nikilalamika mimi mkosefu, ewe mama wa Neno wa Mungu. Naomba usikatae maneno yangu, bali uyasikilize. Amina. Tunakimbilia ulinzi wako, mzazi mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukikuomba katika shida zetu; utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, ewe Bikira mtukufu mwenye baraka. Amina".

(Tazama Chuo kidogo cha sala na nyimbo uk. 34).
Kumbuka na ile sala ya salam Maria umejaa neema…

Wakristo pia wanayo sala maalum ya kumwomba mtakatifu Yosefu (Saint Joseph) ambaye naye pia ni mfu. Kupitia sala hiyo, wanamwomba Yosefu kama ifuatavyo:

"Ee Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya mchumba wako mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako...". (Toka Chuo kidogo cha sala na nyimbo uk. 37).

Yapo maombi mengi ambayo Wakristo huyatumia kuwaomba watakatifu wao wengi waliokufa, kama vile Petro (Saint Peter), Bernard (Saint Bernard) na kadhalika. Ibada hii vile vile kama nyingine nilizozibainisha hapo juu, M'Mungu amewakemea vikali wanadamu kuzitenda kwa kuwa hazitokani na Yeye bali zinatokana na watu wa mataifa yaani wapagani.

Wakristo kuzitenda ibada hizi ni uthibitisho wa wazi kwamba hawamwabudu M'Mungu, Mungu wa Nabii Ibrahimu, Ismaili, Isaka, Yakobo, Yesu, Muhammad na Mitume na Manabii wake wengine wote aliowatuma duniani. Kinyume chake wanatenda ibada za dini ya mungu-mtu ya Kikristo.

Kuabudu Sanamu:
Hii pia ni ibada ya msingi katika dini ya Kikristo ambapo sala za waumini wake (Wakristo) huwa hazitimii bila ya kuomba na kuabudu sanamu. Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la mungu-mtu Yesu wa Kikristo akiwa amebebwa na mama yake (Madona) na kumpa cheo cha umama wa mungu. Yaani Theotokos (“Mother of God”), na kwenye sanamu lingine akiwa amekufa msalabani, sanamu la "Bikira Maria", sanamu la malaika na masanamu mengine mengi ya watakatifu wa Kikristo waliokufa!

Kama maandiko ya Biblia tukufu yafundishavyo, ibada hii (ya sanamu) ifanywayo na Wakristo, kiasili imetokana na watu wa mataifa (wapagani). Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandiko yafuatayo:
"Bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao.Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao".
(Zaburi 106:35-36).

Lakini kwa kuwa Lucifer amewapoteza wakasahau hata haya maonyo halali ya M'Mungu:

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini ya dunia; Usivisujudie; wala kuvitumikia; kwa kuwa Mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu, mwenye wivu...
Kutoka 20:4 kjv

Kwa uchache, maandiko hayo juu yanathibitisha wazi kuwa waasisi na wahusika wakuu wa ibada hiyo (ya sanamu) ni watu wa mataifa, yaani wapagani.

Sambamba na ukweli huo, Biblia haikuacha pia kubainisha jinsi M'Mungu alivyowakemea wanadamu tangu mapema kujaribu kuchonga (kufanya) na kuabudu sanamu, kama ifuatavyo:

"Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao".
(Kumbukumbu la Torati 5:8-9).

Ubatizo:
Hii pia ni ibada kuu na ya msingi katika dini ya Kikristo ambayo hata watoto wachanga nao huusishwa nayo pia! Kwa ujumla wake, ibada hii (ya ubatizo) imeshamiri sana katika Ukristo.

Hata hivyo, pamoja na kuwemo katika orodha ya ibada za Kikristo, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Biblia tukufu, asili ya ibada hiyo (ya ubatizo) imetokana na dini ya kipagani (Mithraism). Uthibitisho wa hayo tunaupata katika maelezo ya Biblia yafuatayo:

"Ibada ya (ubatizo) kutosa mwili majini ni mfano wa utakaso au wakujitengeneza upya. Ibada kama hiyo ilijulikana na kutendeka katika dini za kale za kipagani na dini ya Kiyahudi pia...
(kama ubatizo wa waongofu Mdo 2:10; Waesseni)'.
(Tazama Biblia ya Wakatoliki, Imprimatur M. Mihayo Archbishop of Tabora, February, 1967, kwenye maelezo ya Mathayo 3:6 uk. 879).

Maelezo hayo ya Biblia hapo juu yanathibitisha wazi kwamba ibada hiyo ya ubatizo inatokana na dini za kale za kipagani na kamwe haitokani na dini ya M'Mungu.

Nasema ibada hiyo (ya ubatizo ya kipagani) katu haitokani na M'Mungu, kwa sababu tangu mapema M'Mungu alikwishawakataza na kuwaonya wanadamu kutenda ibada yoyote (kama hiyo ya ubatizo) ya watu wa mataifa (yaani wapagani) kama asemavyo (M'Mungu) katika maandiko yafuatayo:
"Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale".
(Kumbukumbu la Torati 18:19)

Mkristo anaweza kutaka kuutetea ubatizo kuwa ndio ondoleo la dhambi. Lakini wakrito wote wanakiri kuwa Bw. Yesu hakuwa mwenye dhambi, je iweje asiye na dhambi kama bw. Yesu abatizwe? Huu kama si uzushi ni kitu gani?

Hitimisho
Pamoja na ukweli wa shuhuda hizo juu, jambo la kuzingatia hapa ni kwamba, ibada zote ambazo zimefundishwa na Ukristo, Biblia imetuonyesha kuwa ni ibada za kipagani.

Pia Biblia imetuonyesha kuwa mungu-mtu wa Kikristo ni mungu wa kipagani. Kwa kuwa sifa zake zitofauti kabisa na za M'Mungu.

Na bila shaka wenzetu wameona na wameelewa kwa nini Waislamu wanasema kwamba Wakristo hawamwabudu M'Mungu, Mungu wa Nabii Ibrahimu, Ismaili, Isaka, Yakobo, Musa, Yesu, Muhammad na Mitume na Manabii wengine wote.

Ni kwa sababu imani yao (ya mungu-mtu) na ibada zao kamwe hazitokani na Yeye (M'Mungu).
Na kwa ujumla, mradi ibada kuu zinazotekelezwa na Wakristo ni hizo za watu wa mataifa au wapagani, ni dhahiri kuwa mbali ya kutomtambua kwa kutojua sifa zake tukufu na takatifu, M'Mungu daima siye Mungu anayeabudiwa na Wakristo.


Kabla hujasali jiulize swali hili: Je hivyo unavyo sali ndivyo Bw.Yesu (as) ndivyo alivyo fundisha?

Hebu na tutazame baadhi ya mistari inavyomuelezea M’Mungu.
Katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, Sura 1:26-27, Imeandikwa hivi:


Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, Kwa sura yetu… Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Kwa mfano wa Mungu akamwumba, Mwanamume na Mwanamke aliwaumba.”


Swali: Ni kweli Mwenyezi Mungu ana sura kama binadamu?

Mwenyezi Mungu hajui wapi Adam alipo jificha? Mungu wa biblia naye hutembelea bustani kupunga hewa?


Mwanzo, sura ya 3:9, imeandikwa hivi:

Kisha wakasikia (Adamu na mkewe) sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga: Adam na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. Bwana Mungu akamwita Adam, akamwambia hupo wapi? "

Mwanzo 3:14 inaelezea kuwa nyoka amelaaniwa na Mungu, na atakula mafumbi daima.
Je ni kweli nyoka chakula chake ni mavumbi, basi hata alicho kiumba hajui kinakula nini?


Je Mwenyezi Mungu husikitika na kuwa na majonzi kwa kitendo alichofanya?
Mwanzo 6 :6-7, imeandikwa hivi:


Bwana akaghairi kwa kuwa amefanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Bwana akasema, Nitamfuatilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi.”

Mwenyezi Mungu husema uwongo hali nyoka husema kweli?
Mwanzo 3:3-6 Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema , msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na baya.”

Mwenyezi Mungu hushinda mweleka na kiumbe wake?
Mwanzo 32:24-28, imeandikwa hivi:


Yakobo akakaa peke: na mtu mmoja akaashindana naye mweleka hata alfajiri... Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, Ila Israeli, Maana unashindana na Mungu, na watu nawe umeshinda”

Je hii inaingia akilini kweli?

Mwenyezi Mungu hajui anacho kisema?
Mwanzo 6:3, inasemaa hivi:


Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na wanadamu milele kwa kuwa yeye naye ni nyama: basi siku zake zitakuwa miakaa mia na ishirini.”


Kipindi hicho binadamu walikuwa na maumbo makubwa sana. Na walikuwa wanaitwa Wanefili.
Hebu tutazame, Mungu alifuata ahadi yake kwa binadam kuishi miaka 120 tu?


Si kweli watu wengi waliishi juu ya umri alioahidi Mungu. Imeandikwa katika Mwanzo 9:28, kwamba,


Na Nuhu akaishi baada ya ile ghaarika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafaa.”

Huyu ndo mungu wa kwenye Bibilia. Mzee mwenye mvi. Huu ni utani usofaa hata kidogo.
Ni katazama hata viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye mzee wa siku (Mwenyezi Mungu) ameketi, Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi. Danieli 7 :9

Ufunuo wa Yohana 4:2, Imeandikwa hivi:

"Na mara nalikuwa katika Roho: na tazama, Kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kiti: na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.”

Mungu kweli hawezi kupambanua kati ya milango ya wenye kuamini na makafiri ila kwa alama?
Kutoka, sura ya 12:12-13, meandikwa hivi:

Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wamwanadamu na wanyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.”

Mwenyezi Mungu anavunja ahadi zake! Je hajui kuwa Kuvunja ahadi ni aibu kubwa!?
1 Samweli 2:30-31,

"Kwa sababu hiyo,Bwana, Mungu wa Israel, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele:lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami…Angalia, Siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbali ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwa mzee.”


Mungu pia aliwahidi Eli kwamba ukuhani wake ulikuwa wa maisha juu yake na wanawe, lakini baadaye hayo hayakutekelezwa.

Na vilevile katika 1 Samweli 13:13-14 imeandikwa hivi:

“… Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu.”

Mungu yu mbali na uzushi huu, Ati alimwahidi Sauli Ufalme wake kuwa imara milele, na baadaye akavunja ahadi na akampa ufalme mtu mwingine:

Paulo naye kaja na mpya Ati upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu?
Hakika Mwenyezi Mungu si mpumbavu kamwe, vipi itakuwa upumbavu wake una hekima zaidi ya wanadamu ?

Lakini Biblia katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho1:25, imeandikwa hivi:

"Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu.”

Mwenyezi Mungu hujuta akisha tenda jambo?
1 Samweli, 15:10-11, Imeandikwa hivi,

Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, Kusema, najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe Mfalme.”

Je Mungu anaogopa umoja wa binadamu?
Biblia katika kitabu cha Mwanzo 11:1-9, imeandikwa hivi:

"Nchi yote ilikuwa na na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambalale katika nchi ya Shinari: waakakaa huko. Waliambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto.Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni tujifanye jinaa: ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha moja: na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya, Haya, na tushuke huko huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno yao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni paa nchi yote : wakaacha kujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Baabeli."


Je, wewe unaona huyu Mungu wa Biblia ni wa namna gani? Kama Mungu nao mwili, nywele na vazi, anaishi katika mahala , hajui kitu kilichofichika nyuma ya mti, anadanganya watu, huvunja ahadi yake, je binadamu yukoje?

Haya si mafunzo ya M’Mungu hata kidogo huu ni upagani.

2 comments/Maoni:

UWT RAIS VINA said...

Maraan-atha.

Besty said...

maran 'athâ' "Anathema Maranatha"
If any one has no love for the Lord, let him be accursed. Our Lord, come!
(1 Cor 16:22 RSV)