Nani Aliandika Biblia?


Mwanzo inatakiwa ifahamike kuwa Biblia si kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu. Vitabu vitukufu vilivyoteremshwa na Allaah Aliyetukuka ni Suhuf (nyaraka) za Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), Taurati ya Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam), Zaburi ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam), Injili ya Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) na Qur-aan ya Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Biblia ni neno lililotokana na neno la Kigiriki Biblios lenye maana ya mkusanyiko wa vitabu vingi. Biblia yenyewe inatuhakikishia kuwa kuna mikono ya waandishi iliyoingia katika kutunga walichotaka ndani yake. Hii ni kwa mujibu wa Yeremia 8: 8: “Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima, sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’ hali waandishi wa sheria wameipotosha sheria yangu?”

Kulingana na wanazuoni wa Biblia, hata utunzi wa vitabu vya Agano la Kale na Anaajiyl (wingi wa Injili) zenyewe zina shaka na utata.

Taurati
Vitabu vitano vya kwanza vya Biblia (Pentateuch - Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Sheria.) kiada zinanasibishwa na Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam), hata hivyo, zipo aya nyingi sana katika vitabu hivi ambazo zinaashiria kuwa haiwezekani kwa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) kuwa aliandika kila kitu ndani yake. Kwa mfano, Kumbukumbu la Sheria 34: 5 – 8 inayosema: Basi Mose (yaani Musa) mtumishi wa Mwenyezi Mungu akafariki huko nchini Moabu kulingana na neno la Mwenyezi Mungu alilosema. Mwenyezi Mungu akamzika katika bonde la Moabu, mkabala wa mji wa Beth-peori; lakini mpaka leo, hakuna mtu ajuaye mahali alipozikwa. Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; macho yake yalikuwa hayajafifia, na alikuwa timamu na mwenye nguvu. Waisraeli waliomboleza kifo chake kwa muda wa siku thelathini kwenye nchi tambarare ya Moabu. Kisha siku za matanga na maombolezo ya kifo chake zikaisha”. Ni dhahiri kuwa mtu mwengine ndiye aliyeandika aya hizi kuhusu kifo cha Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam).
Katika kiambatisho cha RSV kilichopatiwa anwani “Books of the Bible – Vitabu vya Biblia”, yafuatayo yameandikwa kuhusu utunzi wa zaidi ya thuluthi ya vitabu vilivyobakia katika Agano la Kale:
Vitabu
Mtunzi
Judges (Waamuzi)
Huenda akawa ni Samueli
Ruth (Ruthu)
Huenda akawa ni Samueli
First Samuel (1 Samueli)
Hajulikani
Second Samuel (2 Samuel)
Hajulikani
First Kings (1 Wafalme)
Hajulikani
Second Kings (2 Wafalme)
Hajulikani
First Chronicles (1 Mambo ya Nyakati)
Hajulikani
Esther (Esta)
Hajulikani
Job (Yobu)
Hajulikani
Ecclesiastes
Hajulikani
Jonah (Yona)
Hajulikani
Malachi (Malaki)
Hakuna chochote kinachojulikana
Hata Zaburi nayo ina matatizo kwani katika Sura ya 72: 20 inasema: “Mwisho wa sala za Daudi mwana wa Yese”. Lakini Zaburi inaendelea hadi Sura ya 150. Je, ni nani aliyeandika Zaburi 73 – 150? Sura ya 73 ina kichwa cha habari: Haki itatawala (Zaburi ya Asafu). Je, huyu Asafu ni nani?
Apocrypha
Zaidi ya nusu ya Wakristo duniani ni Wakatoliki. Nakala yao ya Biblia ilichapishwa mwaka wa 1582 kutoka kwa Jerome’s Latin Vulgate (Biblia ya Kikatoliki ya Jerome), na kunakiliwa tena hapo Douay mwaka wa 1609. Agano la Kale la Roman Catholic Version (RCV – Nakala ya Kikatoliki) ina vitabu saba zaidi kuliko KJV inayotambulika na Waprotestanti. Vitabu hivi vya ziada zinajulikana kama Apocrypha (yaani utunzi wenye shaka) na zilitolewa kutoka katika Biblia katika mwaka wa 1611 na wanazuoni wa Biblia wa Kiprotestanti.
Anaajiyl
Aramai ilikuwa ndio lugha iliyokuwa ikitumiwa na Mayahudi huko Palestina. Kwa hiyo, inaaminika kuwa Yesu na wanafunzi wake walizungumza na kufundisha kwa Kiaramai. “Simulizi za kwanza ya mdomo za matendo ya Yesu na kauli zake bila shaka zilisambaa kwa Kiaramai. Hata hivyo, Injili nne ziliandikwa kwa ukamilifu wake kwa maneno mengine, Kiyunani ya kawaida, lugha iliyokuwa ikitumika katika dunia ya Kistaarabu ya Mediterania, ili kutumikia wengi katika Kanisa, ambayo ilikuwa ni ya Kiyunani (wenye kuzungumza Kigriki) badala ya Kipalestina. Mabaki ya Kiaramai yalikuwepo katika Anaajiyl za Kiyunani. Kwa mfano, katika Marko 5: 41, “Kisha akamshika mkono, akamwambia, ‘Tal’itha cu’mi’, maana yake, ‘Msichana mdogo, nakuambia amka’”. Pia Marko 15: 34: “Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, ‘Eloi, Eloi, lama sabachthani?’ maana yake, ‘Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?’” (Encyclopedia Americana, Mj. 3, uk. 654).
Injili ya Marko katika Agano Jipya, japokuwa inachukuliwa na wanazuoni wa Kanisa kuwa ndio kongwe kabisa kati ya Anaajiyl, haikuandikwa na mwanafunzi wa Yesu. Wamehitimisha wanazuoni wa Biblia, kutegemea na dalili zinazopatikana katika Injili, kuwa Marko mwenyewe hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Zaidi ya hayo, kulingana na wao, haijulikani kamwe huyu Marko alikuwa nani kwa uhakika. Mwandishi wa kale wa Kikristo, Eusebius (325 BI), alipokea kuwa mtunzi mwengine wa zamani, Papias (130 BI), alikuwa wa kwanza kuinasibisha Injili kwa John Mark (Yohana Marko), mwandani na mfuasi wa Paul (Paulo). Wengine wametoa rai kuwa huenda alikuwa mwandishi wa Petro na ilhali wengine wanaona kuwa huenda alikuwa mtu mwengine kabisa.
Hiyo ndiyo hali ya Injili nyingine. Japokuwa Mathayo, Luka na Yohana yalikuwa majina ya wanafunzi wa Yesu, waandishi wa Injili hizo waliokuwa na majina ya wanafunzi hao mashuhuri, lakini ni watu wengine ndio waliotumia majina yao ili maelezo yao yapate kusadikika. Kwa hakika, Injili zote zilisambaa hapo awali bila majina. Baadaye majina yenye kuaminika yalipatiwa kama watunzi wa Injili hizo na watu wasiojulikana katika kanisa za awali.


Vitabu
Watunzi
Gospel of Matthew (Injili ya Mathayo)
Hajulikani (“Japokuwa yupo Mathayo aliyetajwa katika orodha tofauti za wanafunzi wa Yesu… mwandishi Mathayo kwa kiasi kikubwa hana jina” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 824).
Gospel of Mark (Injili ya Marko)
Hajulikani (“Japokuwa mtunzi wa Marko huenda akawa hajulikani…” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 826).
Gospel of Luke (Injili ya Luka)
Hajulikani (“Sheria ya Muratori inamtaja Luka, tabibu, mwandani na mfuasi wa Paulo; Irenaeus anamuonyesha Luka kuwa ni mfuasi wa Injili ya Paulo. Eusebius anamuweka Luka kuwa ni tabibu wa Antiocha, ambaye alikuwa na Paulo ili kuipatia Injili mamlaka ya kiutume” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 827).
Gospel of John (Injili ya Yohana)
Hajulikani (“Kutokana na dalili za ndani, Injili hii iliandikwa na mwanafunzi mpenzi ambaye jina lake halijulikani” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 828).
Acts (Matendo)
Mtuzi wa Luka (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830.)
I, II, III John (1, 2, 3 Yohana)
Mtunzi wa Yohana (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830).

Na Allaah Anajua zaidi

0 comments/Maoni: