UTABIRI WA ISAYA

Isaya 7:14 …Tazama bikira atachukuwa mimba, atazaa mototo mwanamume naye ATAMWITA jina lake Imanueli. 

Wakristo upenda sana kutumia huu mstari kuonyesha kuwa Nabii Yesu alitabiriwa kwenye mstari huu, lakini ni kitu cha kushangaza sana kwa kushindwa kuangalia mstakabri mzima wa huo mstari ulipo anzia mpaka kufikia aya ya 14.

Ukisoma kuanzia Anza Isaya 7:10, utagunduwa kuwa utabiri ulikuwa unamuhusu Mfalme Ahazi au Isaya mwenyewe kuwa mkewe ndio atakaye zaa mtoto na ndio maana ukiendelea mbele mpaka kufikia Isaya 9:6, utakutana na maneno haya:

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Isaya 9:6

Mstari huu, umeandikwa kwa present past tense, yaani tukio ambalo limekwisha tokea, ila utokeaji wake si wa muda mrefu. Ndio maana ikaandikwa "...Tumepewa mtoto mwanamume..." Kuonyesha kuwa tendo limekwisha tendeka, si kuwa litatendeka kwa wakati ujao.

Hapa nanukuu kitabu kimojawapo ambacho ni mwongozo kwa walimu wa theologia (Teacher’s guides to religions education series) uliokubaliwa na Wanatheologia wote (Agreed Sylabases).

Kitabu hiki kinaitwa "The Rise of the Prophets" Senior lessons – Volume Six cha Norman J. Bull, M.A – Champlain and lecturer in Divinity Saint Luke’s College.

Mfululizo wa miongozo hii imetayarishwa na The Religious Education Press Ltd. Wallington Survey (1961) katika ukurasa wa 156 kikizungumzia "Imanuel"

Kinasema
"(b) Immanu-el. It was Isaiah’s Unwavering Conviction that Yahweh was with His people – Immanu-el (God with us) – If they would but put their whole trust in Him. The Prophet offered a sign of this to the weak and wavering Ahaz  (see above). A ‘Young woman’ – not ‘ a virgin’ – was with child, and would bear a son to be called Immanu-el. Before he was old enough to know good from evil, Israel and Syria will have been destroyed. This ‘sign’ is given in a concrete historical situation (7:14, 8:8,10 cf. Rom 8.31); it is not visionary future possibility. The ‘young woman’ may well have been Isaiah’s own wife (ef. 8:3) or even the wife Ahaz. From the point of view of Isaiah, there is no Prophecy here of a virgin birth".
Hicho ndicho wanachofundishwa Makadinali, Maaskofu, Mapadre n.k. kuwa huyo mwanamke hakuwa bikira (not a virgin) na tayari alikuwa na mtoto (was with child) na wala sio Maria bali mke wa Nabii Isaya au mfalme Ahazi. Na wanasisitiziwa kuwa hakuna utabiri wa uzazi wa mwanamke bikira hapo " there is no Prophecy here of a virgin birth".

Vilevile ukisoma Biblia ya Revised Standard Version (RSV) kuhusiana na Isaiah 7:14, wao wamelitafasiri neno la Kihebrania  (עַלְמָה) 'almāh{al-maw'}  kuwa ni "young woman" Mwanamke Kijana au kwa Kiswahili cha kawaida twaweza kusema Msichana (Kigori) na si kama wanavyotafasiri kwenye biblia zingine kuwa neno ilo lina maana ya "virgin" yaani Bikra au Bikira.

Neno Bikira au Bikra kwa Kihibrania ni  [בְּתוּלָה (bəṯūlāh)] limetumika mara 50 kwenye Septuagint.

Hapa chini kuna tafasiri mbalimbali kutoka baadhi ya Biblia

Revised Standard Version (American; RSV) 
Therefore the Lord himself will give you a sign. Behold, a young woman[a] shall conceive and bear a son, and shall call his name Imman'u-el
---

Tafasiri Nyingine:

The Jerusalem Bible (Koren Publishing; JBK). 
Therefore the Lord himself shall give you a sign: a maiden is with child and she will bear a son, and will call his name Immanuel.
---

New Jerusalem Bible (Catholic; NJB)
The Lord will give you a sign in any case:  It is this: the young woman is with child and will give birth to a son whom she will call Immanuel
---

New English Bible (NEB)
Therefore the Lord himself shall give you a sign: A young woman is with child, and she will bear a son, and will call him Immanuel.
---

New English Translation Bible (NET)
For this reason the sovereign master himself will give you a confirming sign. Look, this young woman is about to conceive and will give birth to a son. You, will name him Immanuel.

Waweza kupitia Rejea kwenye link hizi kujisomea zaidi




"Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana aendavyo" (Mithali 14:15).

0 comments/Maoni: