UUNGU WA BIKIRA MARIA

Wakristo haswa wa Roman Catholic church na Orthodox church hufanya maandamano na Ibada maalumu kila mwaka tarehe 15 Agosti [Assumption of the Virgin] (Latin assumere, “to take up”) soma ‘article of faith by Pope Pius XII in 1950’ Wakristo humsifu na kumuomba Mariamu huku wakiamini kwamba Mariamu baada ya kifo chake alipazwa mbinguni na kuungana na roho yake tarehe 15 Agosti, ibada hii ilihasisiwa mnamo karne ya 6 BC.

Pia huamini kwamba Mariamu ni mama wa Mungu tena ni Malkia wa Mbinguni bila Mariamu kutoa msaada maombi ya Mkristo hayawezi kupokelewa na Mungu? Je, fundisho hilo ni mpango wa Mungu au ni mapokeo ya wanadamu katika kumshirikisha Mungu na viumbe vyake?

Tangu wakati wa Yesu hajaondoka Duniani wanafunzi wa Yesu walikuwa wanamheshimu Mariamu kama Mama yao sababu Yesu alikuwa amewachagua kuwa rafiki zake soma YOHANA 15:14: "Ninyi mmekuwa rafiki zangu mkitenda niwaamruyo… Maneno hayo waliyashika na kuyaelewa vizuri waliendelea kumheshimu Mariamu Mama wa rafiki yao na walishirikiana naye katika Ibada mbalimbali za kumuomba Mungu wakitumia jina la Yesu kama walivyoelekezwa na rafiki yao, utaratibu huo uliendelea kwa zaidi ya miaka mia moja.

Mnamo mwaka 107 AD. Alikuwa ni Askofu Inyasyo wa Antiokia mtu huyo kanisa linamheshimu kwamba ni nabii mwenye uwezo mkubwa wa kufundisha, huyo ndiye aliyewahimiza Waefeso wazidishe heshima kwa Mariamu, fundisho hilo halikuwa na upinzani mkubwa, watu walilipokea kwa bidii hadi mwaka 165 AD. Ambapo Askofu Justin Martyr mzaliwa Flavia Neapolis 100-165 BC (sasa ni Nabulus, West Bank), mtu huyu alikuwa ni mwenye sifa katika juhudi kushawishi na kuhamasisha aliweza kuwavuta watu wengi zaidi kuongeza heshima kwa Mariamu. Askofu huyu ndiye aliyependekeza Uungu wa Yesu.

Kadri miaka ilivyoendelea ndivyo fundisho lilizidi kuhimizwa, Askofu Origen 185-254 AD. Pia ujulikana kama Origenes. (bone in Alexandria, Egypt. According to standard church histories, he was a student of Clement of Alexandria). Naye anasifiwa na Kanisa kwa juhudi zake katika kuhimiza upendo, huyu alichanganya ukristo na dini ya kigiriki na heshima kwa Mariamu na heshima nyingi zilizidi kumiminwa kwa Mariamu na kwa yesu na yeye ndiye aliyependekeza kwa yesu kuitwa Logos yaani neno.
Askofu mwingine aliye fuata mawazo haya ni Ambrose mzaliwa Trier (Germany) na kusoma Rome Italia 240-397 AD. Askofu huyu mnamo mwaka 370 alichaguliwa kuwa governor wa Aemilia na Liguria makao makuu yake yalikuwa mjini Milan. Na baadaye alichaguliwa kuwa bishop of Milan in 374. ijapokuwa wakristo walikuwa na imani naye lakini cha ajabu mpaka anachaguliwa kuwa Askofu hakuwa amebatizwa. Ambrose alikuwa amevutiwa sana na maandiko ya Origen na Mt Basil. Askofu huyu akishirikia na mkuu wanchi walifanya juhudi kubwa sana kupinga imani ya Mungu mmoja. Imani ambayo wakristo wa mashariki ya kati walikuwa nayo (Arianism). Vile vile waliwanyima hata kusali makanisani wale wote walio kuwa wanaamini Mungu mmoja. Huyu naye Aliongeza sifa nyingine kwamba Mariamu ni mama wa fadhila zote lazima mtu apitishie maombi kwa Mariamu ndipo atapata jibu toka kwa Mungu. Ikatungwa sala maalumu ya kumuomba Mariamu inayosema: "Tunakukimbilia Wewe Mlinzi Wetu Mama Mtakatifu wa Mungu".

Kuanzia hapa, na ukichanganya na mkutano mkuu ulofanyika Nicaea 325 AD, (Nicaea Council of 325 A.D) Kanisa likaanza kupingana na maelezo ya Yesu ya kuabudu M’Mungu mmoja. Kanisa likawafundisha Wakristo wamuombe Mungu kwa jina la Mariamu, upotezaji haukuishia hapo, viongozi walizidisha upendo wao zaidi kwa Mariamu ilipofika mwaka 350 AD. Kanisa likamtangaza rasmi Mariamu ni (Theotokos) yaani Mama wa Mungu jambo lililotokea baada ya Yesu kupandishwa cheo na Mababa wa Kanisa kwenye (Kredo ya Nicea) mwaka 325 AD. Mkutano unajulikana kama mtaguso wa Nicea.

Viongozi waliendelea na juhudi za kumtukuza Mariamu kwa bidii zaidi na ilipofika 381 A.D. Askofu Epfamia wa Jimbo la Cryprus aliwashangaza hata Maaskofu wenzake kwenye Mtaguso wa Konstantinopol alipotamka bila wasiwasi kwamba yeye anaamini kwamba Mariamu hakufa bali alipalizwa akiwa hai mbinguni na Kanisa linamheshimu sana kwa vile alivyokuwa mzungumzaji mwenye mvuto wa pekee kwa hiyo aliweza kuitetea hoja vizuri na kuungwa mkono na viongozi wenzake likawa fundisho kamili hadi sasa Wakristo wanaamini hivyo kwamba Mariamu alipalizwa hai. Msisitizo wa mapokeo yote niliyoyasema ulitolewa kwenye Mtaguso wa Efeso mwaka 431 A.D. (Theostokos) yaani Mama wa Mungu imani ilizidi kupanda, viongozi nao waliyavalia njuga na fundisho yao, hali hiyo ilipopata nguvu zaidi wakati mfalme Moris wa Konstantinopol 582-603 A.D. ambaye alikuwa mshauri wa Papa na Kanisa la Ugiriki alipochagua siku ya tarehe 15 Agosti kila mwaka iwe ndiyo siku ya kusherehekea kupalizwa Mariamu mbinguni ambayo inaadhimishwa hadi sasa na Wakristo. Mradi kila kiongozi alijitahidi kuonyesha upendo na heshima zake kwa Mariamu.

Askofu Germanus wa Antiokia 634-733 A.D. naye alichangia na kumuongezea cheo Mariamu kwamba mtu hawezi kuokoka bila kumwamini Mariamu, hadi sasa Wakristo wanaamini hivyo. Padri Yohana Damascene wa Damascus Syria (Father of the Church, and Doctor of the Church) mtu anayeheshimiwa sana kwa kutunga nyimbo nzuri sana za kumsifu Mariamu ambazo hutumiwa katika liturjia hadi sasa zinaongoza.

Naye Papa Sergio 687 - 701 A.D. aliamua kupanga vizuri kalenda ya sikukuu ya Kanisa kuhusu kupalizwa Mariamu mama wa Mungu, alifuata tarehe iliyokuwa imepangwa na Mfalme Moris 582-603 A.D. Alichofanya Papa ni kuweka katika taratibu nzuri zaidi hadi karne ya 11-13 Wakristo wengi sana Duniani walikuwa wamemkubali Mariamu kwamba ni Mama wa Mungu pia ni Malkia wa mbinguni. Maandamano ma mihadhara mikubwa ilikuwa inaongezeka kila mwaka, msisimko na kuhamasika kuliongezeka sana.

Tarehe 1/11/1950 Papa Pius wa XIII alitunga (Munificentissimus Deus (Most Bountiful God) Bulla Municentess yaani kupalizwa mbinguni tamko rasmi la Kanisa. Tarehe 8/2/1954 Papa Pius wa XIII alitangaza rasmi (Bulla inetabilis Deus) yaani Mariamu mkingiwa dhambi za asili. Pia hilo ni tamko la Kanisa hadi sasa Wakristo wanamsimamo huo na tarehe 21 Novemba 1964 Kanisa lilitangaza kwamba Mariamu ni Mama wa Mungu na Mama wa Kanisa pia hivyo ndivyo Kanisa linavyowapoteza watu wa Mungu badala ya kumwabudu Mungu mmoja, wao wameongeza mapokeo ambayo hata Yesu aliwaonya wanafunzi wake; soma Mark7:6-7:

Akawaambia Isaya alitabiri vema juu yenu enyi wanafiki kama ilivyoandikwa watu hawa huniheshimu kwa midomo yao ila mioyo yao iko mbali nami nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu".

0 comments/Maoni: