Majini Na Imani Zetu


Leo nimeonelea kulileta moja kati ya maswali ambayo nimekutana nayo kwenye mitandao yenye kuuisha majadiliano ya kiimani. Na hapa ni moja kati ya maswali ambayo yameulizwa na dada yetu (Jina naliifadhi). Yeye ni mkristo na si yeye tu, wakristo wengi wanapenda sana kunasibisha mambo haya ya majini na Uislam. Na hii ni kutokana na kuto kuuelewa Uislam.

Swali lake liliaza hivi:
Naomba nieleweshwe tafadhali. Hili jambo limekuwa likinisumbua kwa muda mrefu sasa. Majini ni nini? Majini na waislam wana uhusiano gani katika ulimwengu wa roho? Nashangaa kwa sababu majini yana majina ya kiislam kama vile maimuna,nk. Pia yeyote aliye nayo hulazimishwa kuswali msikitini hata kama alikuwa mkiristo hulazimishwa nayo aache aslim. kuna housegirl tiliwahi kuwa naye akawa anaenda nasi kanisani, siku moja akaamka kakasirika tangu asubuhi yakampiga sana na yakagoma kuongea na sisi eti makafiri na alipokuja mama mmoja muislam ndo yakasema eti kiti wao huyo kawakosea kwa kwenda kanisani mara nyingi, so yanataka kumuua, alipoyabembeleza sana yakatoa masharti lazima aswali sala tano kila siku. mama yule akaendelea kuwa msikiti upo mbali na ni mtoto mdogo, yakasema kama hivyo asikose kila ijumaa kuswali. Sasa nimekuwa nikishindwa kuelewa iweje majini, ambayo ni mapepo au roho chafu zijihusishe na dini ya uislam kwa karibu hivyo? After all hayana nafasi kwenye ufalme wa Mungu. Kwa nini yauchukie ukristo namana hiyo? Tafadhali nisaidieni hii puzzle...


Majibu: 
Assalamu Alaiykum wa rRahmatullah wa Barakatuh

Ama kwa hakika nimevutiwa kidogo na maswali ya dada yetu hapa na nikaona nijaribu kumjibu baadhi ya vipengere ambavyo ameviuliza. Kwa uelewa wangu maswali yalioulizwa nimeyagawa mafungu matano kama ifuatavyo:

1. Majini ni nini?
2. Majini na waislam wana uhusiano gani katika ulimwengu wa roho?
3. Nashangaa kwa sababu majini yana majina ya kiislam kama vile maimuna, nk.
4. Pia yeyote aliye nayo hulazimishwa kuswali msikitini hata kama alikuwa mkiristo hulazimishwa nayo aache aslim.
5 ...yakatoa masharti lazima aswali sala tano... asikose kila ijumaa kuswali.



Insha'Allah nitajitahdi kuyajibu kadri ya M'Mungu atakavyo nijaalia.


Swali la 1. majini ni nini?
Kwanza kabisa yatupasa kuelewa nini maana ya neno jini, Neno jini linatokana na neno la kiarabu Jinn (djinn au Jinnee). Na lina maana ya kitu kisichoonekana au kilichofichika. (Mapepo).


Tafsiri kutoka kamusi za kiingereza zinaeleza hivi maana ya neno jini: 
A: a spirit, often appearing in human form, that when summoned by a person carries out the wishes of the summoner.


B: any spirit; demon or ghost.

C: any of a class of spirits, lower than the angels, capable of appearing in human and animal forms and influencing humankind for either good or evil.

D: A supernatural creature who does one's bidding when summoned.

kwa hali hiyo basi, Majini ni miongoni mwa viumbe alivyo viumba M'Mungu kama tulivyoumbwa Binadam, Malaika, Wanyama na viumbe vingine tusivyo vijuwa, wakiwemo wadudu wa aina mbali mbali.

Matumaini kuwa mpaka hapo dada yetu pamoja na wasomaji wengine wa makala haya watakuwa wamelewa nini maana ya neno jini.

Swali la 2. Majini na waislam wana uhusiano gani katika ulimwengu wa roho?

Jibu:
Kwenye ulimwengu wa kiroho si kwa waislamu tu ambao wanahusishwa na kuwepo kwa majini,
Tukiangalia vitabu vya ulimwengu wa Dini, kama vile Uhindu (Vedas, Puranas), Ukristo (Bible),
Uyahudi (Tamud) nk. Tukichungulia Biblia ya wakristo tunakuta bwana yesu akiyakemea mapepo yaliyokuwa yakikaa ndani ya vichwa vya watu. Haya ni majini ambayo yanasumbuwa watu na kufanya ukorofi kama walivyo baadhi ya binadamu wenye tabia chafu za kukaa vichochoroni na kukaba watu nyakati za usiku na wakati mwingine mchana kweupe. Kwenye Biblia Majoni au Mapepo asili yao ni Malaika. Baada ya kuhasi amri ya M'Mungu wakafukuzwa wao pamoja nakiongozi wao Lucifer (Ibilisi). Kwa Jinsi hiyo Malaika wabaya uitwa kwa jina la Pepo.

Angalia baadhi ya aya kutoka kwenye Biblia:
Genesis 6 :2&4
...that the sons of God saw the daughters of men that they were fair; and they took them wives of all that they chose...The Nephilim were in the earth in those days, and also after that, when the sons of God came unto the daughters of men, and they bare children to them: the same were the mighty men that were of old, the men of renown.American Standard Version that the sons of God, looking at the women, saw how beautiful they were and married as many of them as they chose....The Nephilim were on earth in those days (and even afterwards), when the sons of God resorted to the women, and had children by them. These were the heroes of the days gone by, men of renown
From Jerusalem Bible (catholic).

some of supernatural beings* saw that these girls were beauutiful, so they took the ones they liked... In those days and even later, there were giants on the earth who were descendants of human women and the supernatural beings. They were the great heroes and famous men of long ago.*supernatural beings; or son of gods; or sons of God
From the Good News Bible

the sons of God saw that the doughters of men were beautiful, and they married any of them they chose....The Nephilim were on earth in those days -and also afterward- when the sons of God went to the doughters of men, and had children by them. These were the heroes of the old, men of renown
From King James Version



Pia waweza kupitia kwenye kitabu cha… Isaiah 14:12-15, Job 1: 6 and 2:1 kumb 18:10-11


Kuna majina mengi tu yanayo tumika kumaanisha neno jini, mfano mapepo (pepo), demons, Lucifer, Ghost na jamaa zangu wa kule Commoro visiwa vya ngazija wao wanawajuwa kwa jina la Kibuki. Wamasai wao wanwajuwa kwa jina tofauti. Wapo baadhi ya watu wanawaita kimakosa kwa jina la shetani. Wanashindwa kuelewa kuwa neno shetani ni sifa mbaya, sifa ambayo hata binadamu anapoonekana kuwa ni mwenye kufanya vitendo viovu uhitwa kwa jina la shetani.
Angalia pia Mark 16:9 Pia rejea Genesis 6:2&4, Job 1: 6 na Job 2:1 kumb 18:10-11
Kwa mujibu wa biblia bwana yesu anawaagiza wanafunzi wake watawanyike ulimwenguni wakahubiri Injili kwa viumbe wote. Kwa matumaini kwamba na mapepo wamo, maana nao ni viumbe. Mark16:15-16

Kwenye ulimwengu wa imani ya kuamini dini, majini nayo yana imani tofauti tofauti kama vile tulivyo sisi binadamu. Kuna majini yenye kuamini Uislam, Ukristo, Uhindu, Upagani, na hata dini ambazo tuanziita za jadi. Na kuna yale majini yasioamini kuwepo kwa M'Mungu.
Rejea Qur'an  SURAT AL-JINN[72]:1-11

Ni vipi anatakiwa mwislam kuamini kuhusiana na majini?
(a) Wao (Majini) ni viumbe wa M'Mungu, kama ambavyo M'Mungu alivyoumba malaika vile vile aliumba majini na watu.

(b) Qur-an Tukufu haikuelezea namna ya sifa ya ndani ya maisha ya majini isipokua tu vile
walivyoumbwa kwa moto, na namna ya kuongea kwao na sisi kuongea nao na kuwasiliana nao.

(c) Lakini la kuzingatia mno ni kwamba Qur'an kwa nguvu zote inakataza watu kutaka msaada
kutoka kwa majini au kuwategema, kuwaogopa n.k kwani atakaye wafanya kuwa ni wapenzi
wasaidizi, na kuomba kinga kutoka kwao kinyume na M'Mungu, M'Mungu atamdhalilisha huyo
atakayefanya hivyo. Kwani majini hawana uhusiano wowote na mwanadamu katika maisha yao.
Hawawashi wala hawazimi, wala hawatufanyii lolote gumu kuwa jepesi wala jepesi kuwa gumu, wala hawafanyi lililopo mbali kuwa karibu. Wala hawana uwezo wa kumdhuru yeyote mwenye kumuani M'Mungu.

Huenda watu wakaomba roho hao yaani majini au mapepo wawalinde, wawadhuru wengine, watabiri wakati ujao, au wafanye miujiza. Hakika huu ni ushetani na ni uovu mkubwa.
Mwisho wa yote wao (majini) ni viumbe waliopo chini ya mamlaka ya M'Mungu hawatoki kwenye himaya yake, wala hawawezi kutoka nje ya hukumu zake, kama vile walivyo viumbe wengine.

Ndugu mwislam na wale ambao si waislam watambue kuwa Uislam ni DINI iliyokuwa mbali mno na ushirikina, kwa kutabiri mambo yatakayotokea kwa uongo. Na tutambue kuwa majini watalipwa kwa vitendo vyao vizuri au vibaya kwa ushahidi wa Qur'an, M'Mungu anasema:

"Na wote wana daraja (malipo) sawa kwa yale waliyoyatenda. Na Mola wako si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda."
Qur'an Al-An'am 132.

And the great dragon was cast out, that old serpent, called the Devil, and Satan, which deceiveth the whole world: he was cast out into the earth, and his angels were cast out with him.
Revelation 12:9 From KJV

Swali la 3. Nashangaa kwa sababu majini yana majina ya kiislam kama vile maimuna, nk. Je majini wana majina mengine?

Jawabu ni ndio, majini wana majina mbali mbali mfano:
Lucifer, *Gagoyle, Supernatural beings, Seraphs, Cherubs, Thrones, Dominions, Virtues, Powers, Principalities, vibwengo, mzuka, nk

*ligious History: Based in Catholic believes.
From website:

During the 1200's when gargoyles first appeared (and at many other times), the Roman Catholic Church was actively involved in converting people of other faiths to the Catholic, often very keenly indeed (as the Christian but non-Catholic Cathars could testify). The argument for decorated gargoyles runs as follows. Since literacy was generally not an option for most people, images were very important. Since the religious images (if any) that non-Christians were accustomed to were of animals or mixtures of animals and humans (e.g. the horned god, the Green Man), then putting similar images on churches and cathedrals would encourage non-Catholics to join the religion and go to church, or at least make them feel more comfortable about it, or at least ease the transition. This argument has reasonable grounds if you think about some of the other accomodations the Christian (not just Catholic) church has made, such as fixing the birth of Christ at around the winter solstice to fit in with existing pagan celebrations. Even the Romans made similar adaptations, e.g. in Britain the Celtic goddess Suli worshipped at modern day Bath bore a remarkable resemblance to the Roman goddess Minerva. Rather than replace Suli and upset the locals, both were incorporated into and revered in the Roman baths there. It's amazing how flexible an established church can be if it needs to be - pagan images? no problem if it puts bums on seats.


The Gargoyle Myth and how gargoyles drive off evil:I've put comments in brackets(). 

They can stand guard and ward off unwanted spirits and other creatures. If they're hideous and frightening they can scare off all sorts of things. They come alive at night when everyone's asleep (and you can't see them to prove that they don't) so 
they can protect you when you're vulnerable. Better still, the ones with wings can fly round the whole area and cover the village or town as well as the church. (And if someone does see something, who's to say whether it was just a bat or one of the 
gargoyles on the wing?) They return to their places when the sun comes up (and no-one can prove that they weren't out and about, and no-one respectable who rises and sets with the sun is going to be mistaken by them for an enemy and be dealt with). If you want to see an example of the kind of gargoyle that fits the myth, look at the ones on Woburn church. 

Katika lugha ya kiarabu tutataja baadhi yake:
a) Jinni : Anapokusudiwa jinni tu. Na maana ya neno jinni ni kitu kisichoonekana au
kilichofichika.
b) Aamir : Anapokusudiwa yule anaishi katika majumba ya watu.
c) Shetani : Anapokuwa na shari) Rauhaan : Yule anaewatokezea watotoe) Afriit : Anapokuwa na nguvu za kupindukia.

Haya ni baadhi ya majina ya sifa za majini kwa ujumla. Ama kutokana na swali letu hapo juu kuwa majina yana majina ya kiislam (!?), ni upeo tu wa kufikiri wa muulizaji wa swali. Kwanza napenda kukufahamisha kuwa HAKUNA majina ya kiislam wala ya Kikristo kwenye ulimwengu wa Imani.
Haya tunayo yaita majina ya Kiislam au kikristo kwa asili ni majina ya Kiarabu, kiyahudi au kutoka uropa kwa maana ya majina ya kizungu. Swala hili la majina nakumbuka tulisha wahi kulizungumzia kabla, kwa mtu kuitwa Aziz, Mpambalioto, Judith, Mkejina, Mariam, John haina maana yoyote zaidi ya kumtofautisha kati ya huyu na yule. Yaaani ni katika kuturahisishia tufahamiane tu, hakuna la zaidi. Unaweza kuitwa Fungameza na ukawa ni muumini mzuri wa dini au imani yako. M'Mungu aangalii unaitwa nani, anacho angalia ni kile unacho kiamini ndani ya nafsi yako. Yaani uchaji wako Kwake.

Swali la 4 na la 5. Pia yeyote aliye nayo hulazimishwa kuswali msikitini hata kama alikuwa mkiristo hulazimishwa nayo aache aslim....yakatoa masharti lazima aswali sala tano... asikose kila ijumaa kuswali.

Swali lako lilishajibiwa na Qur'an kabla ujaliuliza...
Sura ya 2 Aya ya 256
Hakuna kulazimishwa kuingia katika dini. Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anayemkataa Taghuut na akamwamini Allah, bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika. Na Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Inasadikiwa kuwa kabla ya kuja Uislamu Madina na baadae kufuatiwa na Mtume (s.a.w.), palikuwepo wenyeji Waarabu wa Madina ambao ama walikuwa waumini wa dini za kishirikiana na hivyo kuabudu masanamu au waliamini dini ya Kiyahudi. Wale wote ambao walikuwa washirikina na baadhi ya makafiri waliukubali Uislamu kirahisi na bila ya taabu kubwa. Kwa upande wa wale Mayahudi wao walisita kidogo licha ya kuwa jamaa zao wote walisilimu. Wazee au ndugu wa Mayahudi hao wa Kiarabu walijaribu kutumia nguvu ili kuhakikisha kuwa watoto au ndugu zao hao wanaukubali Uislamu kwa nguvu au hiari. Kwa kuwa imani si suala la kulazimishwa bali kujengeka yenyewe baada ya hoja na kuyakinisha ndipo Allah (swt)aliteremsha aya hii ili kuzuia mpango huo ambao uliletwa zaidi na msukumo na siyo hoja.

Msimamo huu wa Kiislamu haukuwa wa muda ule na baadae kufutwa; la hasha! Msimamo huu ni wa kudumu kuanzia wakati ule hadi mwisho wa dunia.

Kwa kweli haikubaliwi na hairuhusiwi kwa Mwislamu au mtu yoyote kumlazimisha asiye Mwislamu kuingia katika Uislamu. Kilichopo na kilichoamriwa na Uislamu ni kulingania Uislamu kwa hoja kulingana na yule anayelinganiwa na mazingira kwa ujumla kama tusomavyo:

"Walinganie watu katika njia ya Mola wako (Uislamu) kwa hekima na mawaidha mema na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako ndiye amjuae aliyepotea katika njia Yake, Naye ndiye anayewajua walioongoka."
Qur'an 16:125.


Kulingania wasio, Waislamu ili wawe Waislamu kwa kutumia hoja kama za Qur’an yenyewe, vitabu vyengine vya dini (kama Biblia, Talmud, Veda n.k.), sayansi na nyingine huko siyo kumlazimisha mtu kuwa Muislamu.

Wala kutoa dosari zilizomo katika vitabu hivyo haijakatazwa na Uislamu licha ya jitihada za wale
wanaojipendekeza kwa Wakristo kudai kuwa Uislamu hauruhusu jambo hilo. Kilicho bayana katika mafundisho ya Uislamu ni kukatazwa kuwatukana wale wanaolinganiwa au miungu yao:

Wala msiwatukane wale ambao wanawaabudu kinyume cha Allah wasije wakamtukana Allah kwa jeuri zao bila kujua. Namna hivyo tumewapambia kila watu vitendo vyao. Kisha marejeo yatakuwa kwa Mola wao. Naye atawaambia waliyokuwa wakiyatenda.
Qur'an 6:108

Aya hizi pamoja na nyingine nyingi zinatufahamisha kuwa kutokulazimishwa katika masuala ya dini ni kule kutowashurutisha wasio-Waislamu kuingia au kuukubali Uislamu. Kwa wale walioukubali Uislamu ama kwa kuzaliwa au baada ya kusilimu kwenye kipindi chochote cha umri wao baada ya upambanuzi hapa siyo kulazimishwa lakini ni kuwajibishwa kufanya wajibu wao.

Dola ya Kiislamu au wazee hapa wanawajibika kuona wale walio chini yao wanafuata maelekezo ya Uislamu kama ilivyo elezwa ndani ya Qur’an.
Qur'an inatufundisha kuwa yule ambaye amemkanusha Twaghuut na akamuamini Allah basi huyu ameshikilia mashiko madhubuti. Abul-A’la Maududi katika uchambuzi wake wa Twaghuut anaelezea: Neno la Kiarabu Twaghuut katika lugha linamuhusu kila mtu anayechupa mipaka.

Qur’an inalitumia neno hili kwa kila mtu anayemuasi Allah na akajidai yeye mwenyewe ubwana na mamlaka yasiyo na mipaka juu ya waja wa Allah na kisha akatumia nguvu kuwalazimisha kuwa watumwa wake.

Uasi dhidi ya Allah una daraja tatu za uovu:
(1) Yule ajulikanaye kama Fasiq iwapo anakubali kuwa ni mja wa Allah lakini matendo yake ya kila siku yanakwenda kinyume na amri zake (Allah).

(2) Yule ajulikanaye kuwa ni Kafri iwapo yeye hujitenga moja kwa moja na utegemezi wa Allah au anayemtumikia kwa utii mwingine kinyume na Allah.

(3) Twaghuut n i yule ambaye anafanya uasi dhidi ya Allah na kisha akajitahidi kuwafanya waja wa Allah kuwa ni waja wake yeye badala ya Allah.Twaghuut anaweza kuwa ni shetani au kiongozi wa dini au kiongozi wa kisiasa kama mfalme au serikali. Kwa sababu hiyo mtu hawezi kuwa muumini wa kweli bila ya kumkanusha au kupingana na Twaghuut.

Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini - huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru. Lakini wale walikufuru; walinzi wao ni Matwaghuut - huwatoa katika nuru na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.
Qur'an 2:257

Mbali na jinni, Twaghuut mwingine aliyefichika kwa wengi na nafsi yake mwenyewe binadamu. Nafsi ya binadamu humfanya kuwa mtumwa na matamanio na matashi na kumuongoza kwenye kila aina ya upotofu na njia zilizokwenda upogo. Matwaghuut wengvine ni mke au mume, watoto, jamaa zake, kabila au familia, marafiki au taifa. Aidha Matwaghuu wengine ni viongozi wa kisiasa au kidini na hata serikali yake.

Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.
Qur'an 6:116

5 comments/Maoni:

Anonymous said...

nimependa sana hii makala ya ufafanuzi wa majini na uhusiano na dini ya uislamu ni nzuri inaeleweka,na pia nimefurahishwa sana na ufafanuzi wa majina kwamba hakuna majina ya kikristo na usilamu bali majina mengi yana asili ya uyahudi na uarabu ni kweli kabisa ila watu wengi hawafahamu nimependa sana umejibu vyema

gracekiondo75@yahoo.co.uk

Anonymous said...

Nimekuellewa

Anonymous said...

Ok

Unknown said...

Butrus

Quote
Unajua unachanganya fundisha watu uzima wa milele shekh, ulitakiwa kujibu directly kwanini majini yanalazimasha wasilimu na kwenda msikitini?
End Quote

Somo la hapo juu ni kuhusu majini/mapepo na iyman zetu, somo la uzima wa milele ni kitu kingine kabisa.
Unasema kuwa Majini yanalazimisha watu wawe waislamu na kwenda Misikitini, nadhani labda uelewi nature ya majini na mazingira yao.

unapaswa ufanye utafiti wa kina kuhusiana na viumbe hivi na tabia zao. Tafuta kujuwa majini yanayoishi nchi za Mexico, Brazil na nchi zingine za kikatoliki au kikristo utajuwa majini yao yanalazimisha watu wawe dini gani.

Tafiti uko Comoro utaelewa zaidi.

Katika Uislamu hakuna kulazimishana... Jini kupanda au kukaa kwenye kichwa cha binadamu ni makosa na wataadhibiwa kwa makosa yao hayo.

Quote
Nilitegemea kusoma kwamba kuruani ALLAH wenu aliwasamehe majini baada ya kukosea kwa kiongoz wao shetani ila Uislamu ndio uliochukua jukumu la kuelezea kwamba Allah amewasamehe na majini JIBU VIZURI BRO.Uislamu ni dini iliyotokana na BABILONIA yakishetani na imeudwa na VATIKAN OVER mashetani wenzake.
End Quote

Kuhusu majini kusamehewa ni wale ambao wamekubali kurejea kwenye Twaa yake MwenyeziMungu, kwa sababu MwenyeziMungu anasamehe makosa ya viumbe vyake.

Majini ni viumbe vyake MwenyeziMungu na baba yao Ibilisi alifanya makosa kama vile Baba yetu Adam (as) alivyofanya makosa na kusamehewa.

Majini waliishi Ulimwenguni kabla ya Binadamu kwa mamilioni ya miaka na ni viumbe vilivyopewa hiyari ya kutii au kuhasi kama vile wanadamu.

Quote
Ona kuhusu Sahihi Buhari muandishi alikua Mroma,bi khadija,binamu wake,muandishi wote walitumwa na Roma kuandaauislamu ili kushindana na Wayahudi,
End Quote

Uhujui Uislam na hujui unacho kiandika zaidi ya kukariri kile ulichoandikiwa bila ya ushahidi.

Neno Sahihi Buhari ni Maneno mawili tofauti, ikimaanisha kuwa Buhari amekusanya maelezo yalio Sahihi ndio kwa Kiarabu "Sahii Buhari"

Huyu alikuwa Muislamu msomi jina lake Muhammad al-Bukhari, mwenye asili ya Kiajemi Iran hana uhusiano wowote na Uroma.

Quote
SOMA HOW VATICAN CREATED ISLAM utajua mengi
Mtume taharifa zake zinaenea Afrika ua kaskazini anaongozwa na makasisi kwamba atakua mtu mkubwa wote waliokua wakimuongoza ni wakristo wa siria zamani
NO THING THE DEMON FAITH.
End Quote

Hizo zote ni katika propaganda ambazo hazina ukweli wala ushahidi, kabla ya kuandika tafuta kwanza ukweli kisha ukishamaliza kufanya utafiti yakinifu ndio utoe taarifa kuhusiana na jambo lolote, si kupita kuokoteza vitu ambavyo havina kichwa wala miguu.

Unknown said...

https://teteauislam.blogspot.com/2017/04/majibu-ya-hoja-shetani-na-majinipepo.html