Ukristo
Mambo ya kuyaangalia ndani ya Biblia ni mengi mno. Insha’Allah tutajaribu kuyaangalia machache kwa kadri ya uwezo wetu utakapotupeleka.
Nazarayo [Nasara], (Nazarene) ni dini iliyo anzishwa dhidi ya jumuiya za Mafarisayo na Masadukayo zilizokuwepo kabla. (Taz. Matendo 23:6-8, Mathayo 2:23, na kitabu kungine cha Luka kiitwacho Matendo 24:1-5 na 28:16-22).
Jina “Wakristo" lilianza kutumika kule Antiokia baada ya kuondoka Bwana Yesu (as). (Matendo 11:26). Hilo ni jina la kupanga walilotumia Wapagani wa Antiokia katika kuwaita wafuasi wa Paulo. Wapagani hao walilifahamu neno "Kristo" kama jina la ukoo tu, si kama jina la cheo kwa asili yake yaani mtiwa mafuta au Masiya" (Taz. Biblia Takatifu Tabora).
Matatizo na Ukinzani ndani ya Biblia
Kama nilivyo eleza hapo juu si waislam tu walioamua kuchimba zaidi kuhusu asili ya ukristo. Hata waandishi wasio amini dini yoyote ile nao wakawa wamo ndani ya kutafuta ukweli wa dini hii. Tarekh (History) ikatufunza mambo mengi na kufukuwa siri nyingi mno zilizo fichwa kwa karne kadhaa. Yaliyo gundulikana ni mengi sana. Historia inatufahamisha kuwa Nabii Yesu (as), amezaliwa mnamo karne ya sita (6BCE). (Encyclopaedia Britannica 1978 Vol 10. p 145 under the word Jesus Christ).
Muhulize mtu yeyote yule nini maana ya BCE iliyo fuatiwa na namba kabla (mf: 8BCE). Kwa asilimia 99.99% atakwambia kuwa ni Before Christ, lakini ni kweli hii ndo maana yake haswa? Mbona haiendani na tarehe halisi ya bwana Yesu? Encyclopaedia ya Webster toleo la mwaka 1992 chini ya neno “BC” wamelitafsiri kama Christian Calendar. Ukiendelea mbele zaidi wanatufahamisha kuwa neno hili asili yake ni kifupisho cha maneno haya yafuatayo “Before Common Era” yaani BCE. Bwana Yesu kazaliwa karne ya sita na kuondoka karne ya sita. Na ndo maana hata madhebu na hata baadhi ya maskofu wamekiri kuwa sikukuu hii ya krisimas haina asili yoyote au mnasaba na siku aliyo zaliwa Bwana Yesu (as). Ukisoma Encyclopaedia Brittanica chini ya kichwa cha maneno Chrismas utakuta mamneno haya yafuatayo…
Christmas for example, has much more to do with pagan festivals and idol worship than the worship of the One true God.
The 25th of December is actually the time of the winter solstice when the pagans celebrated the 'return of the sun' when the days began lengthen and the sun began to climb higher in the sky
[Encyclopaedia Britannica Vol 3]. Fananisha maneno hayo na Aya kutoka Jeremiah 10:2-5
The "Christmas Tree" was originally an idol, and the presents underneath it offerings to the idol, in order to speed the return of the dying winter sun.
[Encyclopaedia Britannica Vol 3]
Sikukuu hii iliingizwa ndani ya ukristo mnamo mwaka 336AD, baada ya wapagani wengi kukubali ukristo wa Paulo na wanatheolojia wa kikristo kwa sababu walikuwa wanataka wafuasi wakakubali kuiingiza siku hii ndani ya dini yao ya kikristo, ili kuwafurahisha mapagani.
Injili kama ilinyo andikwa na…
Wanatheolojia wanatufahamisha kuwa Biblia imeandekwa kwa uwezo wa roho mtakatifu kwa maana kila kilichokuwemo ndani ya biblia ni kitakatifu na hakina shaka. Historia kama nilivyo eleza hapo juu, haitufahamishi chochote kile kuhusu asili ya biblia ya mwanzo imepotelea wapi. Kilicho patikana ni ile iliyokuwa imeandikwa kwa kigiriki na kisha ikatafsiriwa kwa Kiyahudi na lugha nyinginezo. Ikiwemo lugha maarufu ya kiingereza. Kosa mojawapo kubwa lililo fanyika katika kutafsiri biblia hizi, ni kunakili kutoka biblia zenye asili ya Kiyunani au kigiriki. (Greek). Watarajuni walio tafsiri kutoka asili yake na kupeleka kwa lugha ya kigiriki hawajulikani na wala hatuambiwi ni kina nani. Naogopa kusema kuwa asili ya biblia ilitokana na lugha aliyo zungumza Bwana Yesu kwa kuchelea kutopata ushahidi yakinifu. Kwa maana hiyo basi injili asili haipatikani kwenye biblia hizi tuzijuazo. Kinachopatikan ni kumbukumbu na mifano ya injili iliyochanganyika na maneno ya waandishi. Na ndio maana tukaona injili hizi za kwenye biblia zimebeba vichwa vya maneno yafuatayo… “Injili kama ilivyoandikwa na…” (The Gospel According to…), Kumbukumbu la... nk.
Na ukiangalia madhumuni ya injili ya Luka, hutashindwa kugunduwa kuwa mwandishi alikusudia kumfahamisha Theofilo mambo mambo yaliopitikana zamani. Mambo yaliyompata Bwana Yesu.
Thomas Ward mwandishi wa kikatoliki ameandika kwenye kitabu chake kuwa;
''…Wasomi wa zamani walikuwa na wasi wasi na sura ya mwisho ya injili ya Marko na wengine hawakukubali baadhi ya aya za sura ya 23 kwenye injili ya Luka na wengine hawakubali kabisa sura mbili za mwanzo katika injili hiyi hiyo ya Luka. Kwa sababu sura hizo hazi kuwemo kwenye injili za asili...''
Wataalamu wa mambo ya uandishi, fasihi na lugha wanasema kuwa mtindo wa uandishi wa kiyahudi hautofautiani sana ule wanao tumia waislam. Yaani kuunganisha mapokeo (Isnad). Lakini katika injili hizi nne hatuyakuti hayo. Tumeletewa tafsiri bila asili.
Kwenye Injili ya Yohana sentesi zilizo tumika au aya zinaonyesha kuwa zimeandikwa katika mtindo wa nafsi ya tatu kiambata. (third person). Yohana 1:6 na 1:15, Hii inaonyesha kuwa mwandishi si Yohana bali mtu mwingine kabisa, lakini lengo lake ni kutaka kuinasibisha injili hii na Yohana wa Zebedayo.
Injili hii imeandikwa mnamo mwaka wa 90-100AD. Japokuwa wanatheolojia wanatuambia kuwa mwandishi yawezekana ni Yohana wa Zebedayo au Yohana Mkubwa (John The Elder). Uandishi wa biblia na kukosa kwake kupata asili yake, ndo ulopelekea hata hao walio nakili kutoka kwenye lugha ya kigiriki kuwa na shaka na kuamua kuandika maneno haya yafuatayo… “Injili kama ilivyo andikwa na…”
Ukisoma Yohana 21:24 utagunduwa tu kuwa mwandishi alikuwa anataka kumsingizia Yohana ili injili yake ikubaliwe. Wayahudi ni kama Waarabu hawatumii jina moja katika kutaja majina yao. Hawa wana tabia ya kutaja jina lake na baba na hata babu wakati mwingine. Utamaduni ulotumika hapa ni wa kigiriki na si wa kiyahudi.
Askofu Irenaeus wa Lione wa karne ya pili, ambaye aliakuwa mwanafunzi wa Polycarp (69-155AD), Polycarp ambaye inasemekana ni mwanafunzi wa Yohana wa Zebedayo, hakukubali wala kuikataa injili hii kama haliwahi kumsikia Polycarp akisema kuwa hii ni injili ya Yohana. Polycarp alikuwa ni mtu hodari na mahiri sana. Yeye alikuwa ameweza kuihifadhi injili yote kichwani kwake. Kama vile tunavyo hifadhi waislam Qur’an. Irenaeus aliwahi kumsikia Polycarp akisema kuwa;
“…nilisikiliza maneno haya kwa uangalifu mkubwa na kwa rehma zake Mungu niliyaandika yote si kwenye karatasi tu bali hata kwenye moyo wangu, na kwa kipindi kirefu nilijenga tabia ya kuyasoma mara kwa mara”
Lakini ni kitu cha ajabu sana kwa askofu huyu, kwani hakuwahi kuthibitisha ukweli wa injili hii ya Yohana. Aliogopa kuwa kama akisema kweli kitakacho mpata ni mauti ya kuchomwa moto adharani. Na hii ndio ilikuwa adhabu maarufu kwa wakati huo.
Wanatheologia wanadai kuwa injili ya kwanza kuandikwa ni ya Mathayo. Lakini wataalamu hivi leo wanatuambia injili ya kwanza kabisa ni ya Marko na si Mathayo. Baadae ndo zikafuata injili ya Mathayo na Luka na mwisho injili ya Yohana. Injili hizi hazitokani na wanfunzi wa Bwana Yesu ni mapokeo ya mdomo kwa mdomo tu kutoka kwa watu tofauti tofauti. (Luka 1:1-4).
Injili tatu za mwanzo zina maudhui yanayo fanana, zinaeleza histori matendo na kazi zake Bwana Yesu. Injili ya nne ya Yohana imejikita sana na kutangaza uungu wa bwana Yesu. Kiasi ya kwamba hata wataalamu wa biblia wakaitilia shaka kama tulivyo eleza hapo juu. Wataalamu na wachunguzi wa kijerumani Bwana Karlhudwig Schmidt, Martin Debelius na Puddf Bultmann, ambao walianzisha kitu kinacho itwa uchunguzi makini wa vyanzo vya uandishi wa injili wanasema kwamba injili hizi hazina ushirikiano katika mambo mengi ya msingi. Kuanzia kuzaliwa kwa Bwana Yesu mpaka kunako semakana kuondoka kwake hapa duniani. Injili hizi hazina ushirikiano wa tarehe, muda, na hata mahala. Kila injili inatofautiana na nyingine. Mfano mdogo ni pale aliposurubiwa Nabii Yesu (as). Je ni neno gani la mwisho alilo tamka Bwana Yesu (as). Kabla ajakata roho?
Mathayo na Marko wanakoti maneno kutoka Zaburi 22:2, “…Eloi Eloi lama sabaktan…”, injili ya Luka inasema “…Baba mikononi mwako naiweka roho yangu…”, injili ya Yohana inasema “…imekwisha”.
Grotius msomi maarufu wa enzi zake anasema kuwa Injili ya Yohana ya asili, ilikuwa na sura 20 tu. Sura ya 21 ilikuja kuongezwa baadae na kanisa la Ephosus. Na hata dhehebu la kale la Allogia, kwenye karne ya pili wao hawakuikubali injili hii na kazi zote za Mtakatifu Yohana. Hata waandishi wa kikristo mwanzo hawakukubali aya 11 za mwanzo katika sura ya 8, kwa sababu aya hizi hazipo kwenye biblia ya Syrine Version.
MOYO WA MWANADAMU NDANI YA QURAN TUKUFU
-
MOYO WA MWANADAMU NDANI YA QURAN TUKUFU
*Moyo Wako Una Akili na Hautegemei Ubongo Kufikiri.*
*Imeaminika kwa karne nyingi kwamba moyo ni sawa na pampu tu ...
2 years ago
3 comments/Maoni:
ALLAH AKBAR HII NI ELIMU ILIYO FICHWA BILA SHAKA
Mungu akuzidishie INSHAALLAH kutokana na bidii yako njema
Alhamdulillah, Tunamshukuru MwenyeziMungu na pia tunawashukuru wasomaji wetu wote kwa kupitia na kuzisoma makala zetu, msisite kututumia maoni yenu nasi tutajitahidi kuyafanyia kazi In-shaa-Allah.
Post a Comment