Wanawake Wa Kiingereza Wanarudi Katika Uislamu

Kwa Nini Wanawake Wa Kiingereza Wanarudi Katika Uislamu

Kuenea Kwa Dini Ya Ulimwengu

Idadi isiyowahi kutokea ya Waingereza, takribani wote wakiwa ni wanawake, wanaingia kwa wingi katika Uislamu katika kipindi ambacho kuna migawanyiko mikubwa kabisa ndani ya makanisa ya Anglikana na Roman Catholic.

Tathmini ya mabadiliko haya imesababisha kutabiriwa kuwa Uislamu utakuwa kwa haraka sana na kuja kuwa dini kubwa yenye nguvu katika nchi hii ya Uingereza. “Katika kipindi cha miaka 20 ijayo idadi ya Waingereza watakaosilimu italingana au itashinda idadi ya jamii ya wahamiaji wa Kiislamu walioleta dini hii hapa nchini”, anasema Rose Kendrick, ambaye ni mwalimu wa mafunzo ya dini katika shule maalum ya Hull na mtunzi wa kitabu cha kiada cha muongozo wa Qur’an.

Anasema: “Uislamu ni dini kubwa duniani kama ilivyo kwa Roman Catholic. Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa dini husika ni mali yake”. Uislam pia unaenea kwa kasi kubwa katika bara hili na Amerika kwa ujumla.

Wimbi hili la watu kuingia katika Uislam linatokea licha ya taswira mbaya inayotolewa na vyombo vya habari vya Kimagharibi dhidi ya dini hii. Kwa hakika, kasi ya kuingia katika Uislam imeongezeka tangu kutangazwa kwa kadhia ya Salman Rushdie, vita vya Ghuba na mateso yaliyowapata Waislam wa Bosnia. Inashangaza zaidi kuona kuwa wengi katika Waislamu wapya wa Kiingereza ni wanawake, hasa ikizingatiwa kwamba kuna mtazamo ulioenea katika nchi za Magharibi kuwa Uislam unawatendea vibaya wanawake. Nchini Marekani idadi ya wanawake wanaosilimu ni zaidi ya wanaume kwa zaidi ya mtu mmoja mpaka wanne, na Uingereza wanafikia wingi wa jumla ya kuanzia watu 10,000 mpaka 20,000, wakiunda sehemu ya jamii ya Kiislam ya watu milioni 1 mpaka milioni 1.5.

Wengi katika “waislamu wapya” wa Uingereza wanatoka katika familia za daraja la kati. Miongoni mwao ni Matthew Wilkinson, Kaka mkuu wa zamani wa shule ya Eton aliyekwenda katika chuo Kikuu cha Cambridge, na watoto wawili wa kike na wa kiume wa Mwanasheria Mkuu ambaye ni jaji anayeongoza uchunguzi wa kadhia ya kutuma majeshi nchini Iraq.

Utafiti mdogo uliofanywa na taasisi ya The Islamic Foundation ya mjini Leicester umegundua kuwa wengi wa wale wanaosilimu wana umri wa miaka 30 mpaka 50. Vijana wa Kiislamu wanaonyesha kuwa wanafunzi wanasilimu kwa wingi na kuonyesha msukumo wa kitaaluma katika Uislamu. “Muhammad” alisema, “Nuru ya Uislamu itachomoza huko Magharaibi” nadhani ndicho kinachotokea sasa, anasema Aliya Haeri, mwanasaikolojia mwenye asili ya Kimarekani aliyesilimu miaka 15 iliyopita. Yeye ni mshauri wa taasisi ya Zahra Trust, taasisi inayo jishughulisha na uchapishaji wa kazi za kidini na ni miongoni mwa wazungumzaji mashuhuri wa Kiislamu nchini Uingereza. Anaongeza kusema: “Wazawa wanaosilimu wanaingia katika Uislamu kwa uchangamfu, sio kwa mazoea, wakiepukana na kile kilicho kinyume kiutamaduni. Imani hii safi inajikuta ikiwa ni yenye nguvu na imara zaidi katika nchi za magharibi”.

Baadhi wanasema kuwa mabadiliko haya yanatokana na kuibuka kwa elimu ya kulinganisha dini (mijadala). Vyombo vya habari vya Uingereza, kwa kuelezea kile kinachoelezewa na waislamu kama mashinikizo mabaya yasiyo na kikomo, vimesekana kuchangia mabadiliko hayo. Watu wa magharibi wakiwa wamekatishwa tamaa na jamii yao wenyewe – kuibuka kwa uhalifu uliopindukia, mparaganyiko wa kifamilia, madawa ya kulevya na matumizi ya vileo wamevutiwa sana na umadhubuti na Usalama unaopatikana ndani ya Uislamu. Wengi wao walikuwa wakristo waliopoteza imani kutokana na wasiwasi, mashaka na hali ya kutokuwa na uhakika iliyopo katika kanisa na kutokana na kutofurahishwa na nadharia ya imani ya Utatu na hatua ya kumfanya Yesu kuwa Mungu.

0 comments/Maoni: